Wa 2000 watasema haya ni mabomu ya kivita ya zamani

Dah mkuu, yaani zote zinaonekana ni 'brand new' kabisa, wewe ni kiboko!

Hata kama ni picha tu, zilihifadhiwa wapi kuonekana katika ubora huu takribani miaka 50 iliyopita!

Hizo mbili za juu kabisa, radio National yenye jalada na hiyo radio casette memory Q zimenikumbusha mbali, kama miaka 45 iliyopita'ivi!

Hiyo Memory Q niliwahi kuimiliki, niliinunua mpya kabisa kwa bei ya Tshs 2,000 mwaka 1980 na nilitamba nayo vibaya mno!
 
Perfume 😅, yeah!! Mkuu kumbe we ni mzee mpenda mapini Makali kama mimi aise.
Haha!, sijazeeka ila nahisi ni kama bahati nimekuwa kwenye kipindi ambacho hizi ngoma zilikuwa zinawika na labda niseme mi napenda sana muziki so hivyo ikawa rahisi zaidi kuzipenda na kuzijua hizi ngoma!.
Napenda muziki ila zaidi napenda muziki wa zamani!.
 
Mkuu hata Mimi zile ngoma za pale first generation z ya bongo flava nazipenda sana hasa nyota ya msechu na amini, baby candy ya Dully, Robo saa ya amini, jambo jambo ya Rnb n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…