Waacheni Warudi Lakini Wasitutoe Kwenye Reli: Je, Hii ni Mkakati wa CCM Kudhoofisha CHADEMA?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Wimbi kubwa la hivi karibuni la wanachama na viongozi wanaorejea CHADEMA linapaswa kutazamwa kwa tahadhari kubwa ya kisiasa.

Ingawa hatua hii inaongeza idadi ya wanachama, kuna uwezekano mkubwa ikawa ni mpango mkakati uliosukwa na CCM ili kupandikiza mamluki, kukusanya siri za ndani, na kudhoofisha nguvu ya upinzani kuelekea uchaguzi.

Kurudi kwao kunaweza kuleta migogoro mipya ya kuwania madaraka na kuwavunja moyo wanachama waaminifu waliosimama imara na kukabiliana na dhoruba wakati wa vipindi kigumu cha chama.

Ili kuzuia mtego huu na kutosukumwa nje ya reli, CHADEMA inahitaji kuweka mifumo madhubuti ya kuchuja wanaorejea (vetting) na kuwapa muda mrefu wa matazamio kabla ya kuwakabidhi nyadhifa zozote za uongozi.

Agenda kuu za chama kama kudai Katiba Mpya na mageuzi ya kiuchumi hazitakiwi kuyumba wala kubadilika ili tu kuwafurahisha wageni hao wapya.

Lengo liwe ni kuwapokea kama wanachama wa kawaida huku kipaumbele, ulinzi, na heshima kubwa zikibaki kwa wale waliokipigania chama bila kukisaliti
 
tahadhari gani hizo gentleman wakati wanaorudi moja kwa moja wanakua wajumbe maalumu wa kamati kuu chadema taifa?

chadema iliwahi kujifunza nini au kuchukua tahadhari gani kwa mfano gentleman kwenye suala la kuyala matapishi yake? hakutakua na vetting wala muda wa matazamiao. Akina selasini, msigwa n.k wote ni direct kamati kuu taifa,

chadema ina ombwe la uongozi kwasasa,
na haina agenda kabisa za kusimamia. kamwe haina ubavu wa kumkataa yeyote yule anaerejea ndani ya chama hicho kutoka popote.

Na daima,
inachojidanganya sana chadema siku zote ni kwamba,
inaamini wanaorudi chadema kutoka vyama vingine vya siasa, labda wanakuja na kitu very special,
na lakini pia wanajidanga zaidi kwamba eti watu hao wana agenda ambazo zinaweza kuisaidia chadema walau kua na cha kusema kwa wananchi, kitu ambacho ni nonsense ya kiwango cha juu sana katika siasa hususan za Tanzania :pulpTRAVOLTA:
 
Kuna maamuzi yanachukuliwa hunifanya niwaze.
Sawa CHADEMA sio kikundi cha wanaharakati ni chama cha siasa

Ila kwa nini huwa kina soft spot n
Kwa rejects wa CCM

Kuna kitu hakipo sawa ila ni suala la muda kama yalioibuliwa na No reforms, no election
 
1779798625489.jpg
 
Wimbi kubwa la hivi karibuni la wanachama na viongozi wanaorejea CHADEMA linapaswa kutazamwa kwa tahadhari kubwa ya kisiasa. Ingawa hatua hii inaongeza idadi ya wanachama, kuna uwezekano mkubwa ikawa ni mpango mkakati uliosukwa na CCM ili kupandikiza mamluki, kukusanya siri za ndani, na kudhoofisha nguvu ya upinzani kuelekea uchaguzi. Kurudi kwao kunaweza kuleta migogoro mipya ya kuwania madaraka na kuwavunja moyo wanachama waaminifu waliosimama imara na kukabiliana na dhoruba wakati wa vipindi kigumu cha chama.Ili kuzuia mtego huu na kutosukumwa nje ya reli, CHADEMA inahitaji kuweka mifumo madhubuti ya kuchuja wanaorejea (vetting) na kuwapa muda mrefu wa matazamio kabla ya kuwakabidhi nyadhifa zozote za uongozi. Agenda kuu za chama kama kudai Katiba Mpya na mageuzi ya kiuchumi hazitakiwi kuyumba wala kubadilika ili tu kuwafurahisha wageni hao wapya. Lengo liwe ni kuwapokea kama wanachama wa kawaida huku kipaumbele, ulinzi, na heshima kubwa zikibaki kwa wale waliokipigania chama bila kukisaliti
Ni makosa makubwa sana kuwashambulia watu waliohama chama fulani kisha wakarejea chama hicho,kwani kuhama na kurejea ni haki yao ya kikatiba.Hii lugha ya kuwaita ni wasaliti ndio usaliti wenyewe kwa demokrasia
 
Wimbi kubwa la hivi karibuni la wanachama na viongozi wanaorejea CHADEMA linapaswa kutazamwa kwa tahadhari kubwa ya kisiasa. Ingawa hatua hii inaongeza idadi ya wanachama, kuna uwezekano mkubwa ikawa ni mpango mkakati uliosukwa na CCM ili kupandikiza mamluki, kukusanya siri za ndani, na kudhoofisha nguvu ya upinzani kuelekea uchaguzi. Kurudi kwao kunaweza kuleta migogoro mipya ya kuwania madaraka na kuwavunja moyo wanachama waaminifu waliosimama imara na kukabiliana na dhoruba wakati wa vipindi kigumu cha chama.Ili kuzuia mtego huu na kutosukumwa nje ya reli, CHADEMA inahitaji kuweka mifumo madhubuti ya kuchuja wanaorejea (vetting) na kuwapa muda mrefu wa matazamio kabla ya kuwakabidhi nyadhifa zozote za uongozi. Agenda kuu za chama kama kudai Katiba Mpya na mageuzi ya kiuchumi hazitakiwi kuyumba wala kubadilika ili tu kuwafurahisha wageni hao wapya. Lengo liwe ni kuwapokea kama wanachama wa kawaida huku kipaumbele, ulinzi, na heshima kubwa zikibaki kwa wale waliokipigania chama bila kukisaliti
Walijaribu kuifungula Chadema kupima upepo, wameona wingi wa watu kwenye mikutano inawatisha, wamekuja na plani ya Msigwa na Selasini,

Cha kujiuliza mbona hawakurudi kipindi CDM imefunguwa kufanya siasa, tusubiri tuone,

Pia Mshana Kuna yule Mpare mwenzio Mchome aliepangishiwa apartment na msajili nae atataka kurudi,
 
Wimbi kubwa la hivi karibuni la wanachama na viongozi wanaorejea CHADEMA linapaswa kutazamwa kwa tahadhari kubwa ya kisiasa.

Ingawa hatua hii inaongeza idadi ya wanachama, kuna uwezekano mkubwa ikawa ni mpango mkakati uliosukwa na CCM ili kupandikiza mamluki, kukusanya siri za ndani, na kudhoofisha nguvu ya upinzani kuelekea uchaguzi.

Kurudi kwao kunaweza kuleta migogoro mipya ya kuwania madaraka na kuwavunja moyo wanachama waaminifu waliosimama imara na kukabiliana na dhoruba wakati wa vipindi kigumu cha chama.

Ili kuzuia mtego huu na kutosukumwa nje ya reli, CHADEMA inahitaji kuweka mifumo madhubuti ya kuchuja wanaorejea (vetting) na kuwapa muda mrefu wa matazamio kabla ya kuwakabidhi nyadhifa zozote za uongozi.

Agenda kuu za chama kama kudai Katiba Mpya na mageuzi ya kiuchumi hazitakiwi kuyumba wala kubadilika ili tu kuwafurahisha wageni hao wapya.

Lengo liwe ni kuwapokea kama wanachama wa kawaida huku kipaumbele, ulinzi, na heshima kubwa zikibaki kwa wale waliokipigania chama bila kukisaliti
Siasa ni mchezo wa hesabu/ siasa ni mchezo mchafu.

Ndio maana wakati mwingine:

Wapokelewe lakini wasipewe nafasi kubwa haraka.

Wapokelewe chini ya uangalizi Maalum wa kisiasa.

Tuwape muda wa kuthibitisha utii wao kwanza. Mfano Peter msigwa..

Wengine watumike zaidi kama “symbol” ya kuongeza nguvu ya chama kuliko kupewa siri nzito za chama au kuwekwa kamati kuu ama kamati tendaji mfano huyo SELASINI
Kwa uchache sanaa

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom