Waacheni Warudi Lakini Wasitutoe Kwenye Reli: Je, Hii ni Mkakati wa CCM Kudhoofisha CHADEMA?

Waacheni Warudi Lakini Wasitutoe Kwenye Reli: Je, Hii ni Mkakati wa CCM Kudhoofisha CHADEMA?

Wimbi kubwa la hivi karibuni la wanachama na viongozi wanaorejea CHADEMA linapaswa kutazamwa kwa tahadhari kubwa ya kisiasa.

Ingawa hatua hii inaongeza idadi ya wanachama, kuna uwezekano mkubwa ikawa ni mpango mkakati uliosukwa na CCM ili kupandikiza mamluki, kukusanya siri za ndani, na kudhoofisha nguvu ya upinzani kuelekea uchaguzi.

Kurudi kwao kunaweza kuleta migogoro mipya ya kuwania madaraka na kuwavunja moyo wanachama waaminifu waliosimama imara na kukabiliana na dhoruba wakati wa vipindi kigumu cha chama.

Ili kuzuia mtego huu na kutosukumwa nje ya reli, CHADEMA inahitaji kuweka mifumo madhubuti ya kuchuja wanaorejea (vetting) na kuwapa muda mrefu wa matazamio kabla ya kuwakabidhi nyadhifa zozote za uongozi.

Agenda kuu za chama kama kudai Katiba Mpya na mageuzi ya kiuchumi hazitakiwi kuyumba wala kubadilika ili tu kuwafurahisha wageni hao wapya.

Lengo liwe ni kuwapokea kama wanachama wa kawaida huku kipaumbele, ulinzi, na heshima kubwa zikibaki kwa wale waliokipigania chama bila kukisaliti
Chadema imekuwa imara baada ya uchaguzi mkuu wake,si ya kuvunjika tena.
 
Hao dawa yao ni ndogo sana. Wabaki kuwa ''wanachama walio kwenye probation'' wasipewe uongozi au say yoyote kwenye chama. Wasiruhusiwe kuwania uongozi wala kupiga kura kuchagua viongozi mpaka muda wa probation utakapoisha. Hatari kubwa ipo sasa hivi kwa sababu CCM inatafuta chama kinachokubalika na wananchi na jumuia ya kimataifa (CHADEMA), ili kiwarubuni, kiwape nafasi chache za uongozi na mauaji ya 29/10 yasahaulike. Kwa kifupi wanataka kufanya kama walivyoua upinzani wa Zanzibar kwa kuwapa baadhi ya wapinzani ''ving'ora''.
Una hoja. Usipuuzwe!
 
Kuna tofauti kati ya kulaumu/kushambulia na kutoa tahadhari mbele ya inayoweza kuwa hatari.Tofautisha.
Unaweza kutoa tahadhari huku unatisha,unalaumu na kushambulia.Unayafanya hayo yote kwa kisingizio cha kutoa tahadhari.Acheni demokrasia ifanye kazi yake
 
Unaweza kutoa tahadhari huku unatisha,unalaumu na kushambulia.Unayafanya hayo yote kwa kisingizio cha kutoa tahadhari.Acheni demokrasia ifanye kazi yake
Wewe kichwa chako ni kigumu sana kuelewa jinsi dunia inavyojitikisa kwenye muhimili wake.Nyuzi zinazokufaa wewe ni uchambuzi wa visimi tu.Tulia.
 
Chandema itasambaratika kwa kutokea ndani ya chama kwa kukubali kupokea hawa maspay
 
Yericko hatakiwi kurudi chadema!!!🦷🛑 inatakiwa hata akirudi afungiwe miaka 10 kushiriki kwenye shughuli zozote za chama, nyang'au yule😎
 
Wimbi kubwa la hivi karibuni la wanachama na viongozi wanaorejea CHADEMA linapaswa kutazamwa kwa tahadhari kubwa ya kisiasa.

Ingawa hatua hii inaongeza idadi ya wanachama, kuna uwezekano mkubwa ikawa ni mpango mkakati uliosukwa na CCM ili kupandikiza mamluki, kukusanya siri za ndani, na kudhoofisha nguvu ya upinzani kuelekea uchaguzi.

Kurudi kwao kunaweza kuleta migogoro mipya ya kuwania madaraka na kuwavunja moyo wanachama waaminifu waliosimama imara na kukabiliana na dhoruba wakati wa vipindi kigumu cha chama.

Ili kuzuia mtego huu na kutosukumwa nje ya reli, CHADEMA inahitaji kuweka mifumo madhubuti ya kuchuja wanaorejea (vetting) na kuwapa muda mrefu wa matazamio kabla ya kuwakabidhi nyadhifa zozote za uongozi.

Agenda kuu za chama kama kudai Katiba Mpya na mageuzi ya kiuchumi hazitakiwi kuyumba wala kubadilika ili tu kuwafurahisha wageni hao wapya.

Lengo liwe ni kuwapokea kama wanachama wa kawaida huku kipaumbele, ulinzi, na heshima kubwa zikibaki kwa wale waliokipigania chama bila kukisaliti
majita hamueleweki, mtu akihama mnalalamika na kumtusi na akitaka kurudi bado mnalalamika na kumtusi. watu wa hovyo sana nyie.
 
Wa chaumma ambao hatuwataki ni mwalimu,mrema, James Mbowe, Yeriko Nyerere,Catherine Ruge, kigaila,mchome na wale vimbelembele wote.
chama cha siasa sio kikundi cha wanaharakati. kama Lowasa alikubaliwa na Lisu basi kila aliyewahi kuwa mwanachama wa chadema akahama anaruhusiwa kurudi kundini.
 
Ni makosa makubwa sana kuwashambulia watu waliohama chama fulani kisha wakarejea chama hicho,kwani kuhama na kurejea ni haki yao ya kikatiba.Hii lugha ya kuwaita ni wasaliti ndio usaliti wenyewe kwa demokrasia
kuna wajinga wanapenda kuimba wimbo wa demokrasia lakini wanashindwa kuishi misingi ya demokrasia.
 
Mimi nasema wote hawa ni watoto wa family moja chadema walikengeuka na Sasa wamegundua Kama walipotea ni wakati wa kuwasamehe Kisha tutengeneze chama imara .
 
Back
Top Bottom