Waacheni Warudi Lakini Wasitutoe Kwenye Reli: Je, Hii ni Mkakati wa CCM Kudhoofisha CHADEMA?

Selasini sidhani kama ni wa kutiliwa sana mashaka maana alikua na ugomvi na mwamba...

Na zaidi alihamia chama chake cha zamani na sio CCM kama tarumbeta Msigwa.

N.B.HAO WA CHAUMMA NDIO WA KUA NAO MAKINI SANA SANA.
Wa chaumma ambao hatuwataki ni mwalimu,mrema, James Mbowe, Yeriko Nyerere,Catherine Ruge, kigaila,mchome na wale vimbelembele wote.
 
Msigwa na Selasini ni watu wa kuwa macho nao sana, kuna kitu hakipo sawa
Ni makosa makubwa sana kuwashambulia watu waliohama chama fulani kisha wakarejea chama hicho,kwani kuhama na kurejea ni haki yao ya kikatiba.Hii lugha ya kuwaita ni wasaliti ndio usaliti wenyewe kwa demokrasia
Nimeandika mtazamo wangu nawe umeandika wako.. Hadhira ndio hakimu wa haki
 
Pia Mshana Kuna yule Mpare mwenzio Mchome aliepangishiwa apartment na msajili nae atataka kurudi,😂😂list ni ndefu
 
Inasikitisha sana,

Ila huwezi jua kama chadema waliweka project ya kupandikiza watu vyama vingine wakirejea kunashida?
 
Kama ccm ilishindwa kukidhoofisha chadema wakati na baada ya uchaguzi wa mwenyekiti Lissu sidhani kama wataweza kukidhoofisha chama kwa kutumia misukule ya ccm.
 
Hao dawa yao ni ndogo sana. Wabaki kuwa ''wanachama walio kwenye probation'' wasipewe uongozi au say yoyote kwenye chama. Wasiruhusiwe kuwania uongozi wala kupiga kura kuchagua viongozi mpaka muda wa probation utakapoisha. Hatari kubwa ipo sasa hivi kwa sababu CCM inatafuta chama kinachokubalika na wananchi na jumuia ya kimataifa (CHADEMA), ili kiwarubuni, kiwape nafasi chache za uongozi na mauaji ya 29/10 yasahaulike. Kwa kifupi wanataka kufanya kama walivyoua upinzani wa Zanzibar kwa kuwapa baadhi ya wapinzani ''ving'ora''.
 
Ni makosa makubwa sana kuwashambulia watu waliohama chama fulani kisha wakarejea chama hicho,kwani kuhama na kurejea ni haki yao ya kikatiba.Hii lugha ya kuwaita ni wasaliti ndio usaliti wenyewe kwa demokrasia
Kuna tofauti kati ya kulaumu/kushambulia na kutoa tahadhari mbele ya inayoweza kuwa hatari.Tofautisha.
 
Walihama sababu ni njaa na tamaa ya madaraka si wavumilifu, kiufupi ni wasaliti.
 
Swali la kujiuliza kabla wa kuwapokea hawa watu ni .
1. Kwanini hawakutaka kuludi wakati chama kimefungiwa kufanya shughuli zake?? (Wanasema wanamapenzi na chama wakati wa raha tu?

2. Kwa Nini wanaludi kwa mkupuo mmoja kana kwamba walikaa kikao wakakubaliana sasa tuludi?

3. Huu uludiji unataka kufanana kama ule wa enzi za magufuli wa kuunga juhudi( pia walihama kwa mkupuo mkupuo baada ya vikao vya kununuliwa.

*Hapana hapo viongozi kuweni makini.
 
Selasini sidhani kama ni wa kutiliwa sana mashaka maana alikua na ugomvi na mwamba...

Na zaidi alihamia chama chake cha zamani na sio CCM kama tarumbeta Msigwa.

N.B.HAO WA CHAUMMA NDIO WA KUA NAO MAKINI SANA SANA.
Huyo Selasini si ndio alitumika na msajili kumpora chama Mbatia? Nakumbuka Selasini wakati wa Magufuli yeye na Mwambie walikuwa wanapingana na misimamo ya cdm ndani ya number ili kumfurahisha Magufuli. Isitishe Selasini ana historia ya kuleta migogoro kwa vyama anavyokuwepo. Hao wajinga wanaorudi wasipewe nafasi yoyote ya uongozi.
 
Kabisa, wameona cdm bado iko mioyoni mwa watu ndio wanataka kurudi. Mimi naona kabisa wanarudi kukivuruga chama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…