Waafrika hatukupaswa kutumia kalenda moja na wazungu. Sisi tuko nyuma ya wazungu kwa miaka 300

Waafrika hatukupaswa kutumia kalenda moja na wazungu. Sisi tuko nyuma ya wazungu kwa miaka 300

Una ji underestimate mkuu, acha upuuzi kuwatukuza weupe.
Jikubali
Unakwepa uhalisia wakati ni reality wazungu wametuzidi.

Kama unasema tunaji "underestimate"

Nieleze ni mambo gani waafrika tumeweza kufanya wenyewe pasipo usaidizi wowote ule wa kitaalamu au kifedha kutoka kwa wazungu.

Walau katika nyanja za kiviwanda, kiafya, kisayansi na kiteknolojia.

Simu yenyewe unayo tumia hapa ni ya mzungu.

Waafrika wamegundua nini kinacho tumika Worldwide leo hii?
 
Hii thread ni... damn it! Inshort katika ulichoandika hakuna sababu significant ya kufanya Africa kutumia calendar tofauti na inayotumiwa na dunia nzima. Hata kama ingekuwepo bado ingekuwa ni useless na kupoteza muda but mostly ni kuprove kwa kiasi mtu aliyekuja na idea kama hiyo ni mpuuzi asiye na akili na nia yake ni kufanya Waafrica wote waonekane vichwa maji.

Alafu kazi ya calendar sio kupima nani yuko wapi bali ni kupima kwa umoja dunia iko wapi, ni mostly for history precision na kutochanganyana kwamba vita ya dunia kati ya Africa na Marekani ilotokea 2000 au 1100. Na kingine dunia imekuwa ndogo kutokana na utandawazi na technology, sasa kubadilisha calendar kutakufanya uwe nyuma zaidi sababu utashindwa kujua kwa kiasi gani mmekuwa nyuma kulinganisha na wengine.

Kiufupi hii threads ni... ahh! Whatever!
 
Wazungu ni kina nani ?

Earliest Civilization among others ilikuwa Mesopotamia Civilization, Egyptian Civilization, Indus Valley Civilization, and Chinese Civilization. Hata ukichunguza mabaki ya huku kuna sehemu nyingi Africa ugunduzi na matumizi ya chuma, pottery n.k. yalifanyika.... Watu kama kina Mansa Khankan Mussa ni among the earliest wealthiest leaders...

Kwahio kabla haujahukumu jaribu kufanya upembuzi yakinifu...; western countries walichofanikiwa ni adaptation na kuchukua ugunduzi wa huku na kule na kuboresha; Pia industrial revolution ya huko bara la ulaya lilifanya wapige hatua ya kasi zaidi na hio haiwezi kuwa credited na watu wa sehemu fulani tu....

If I have seen further than others is by standing on the Shoulders of the Giants.......;
 
Hata hai wazungu wapo nyuma miaka elf tatu dhidi ya ulimwengu usioonekana.
Upo uwezekano mkubwa sana.

Hatahivyo niongeze tu....

Bongo Dili,

Hii dhana kwamba "Tuna Laana" au "Tanakufa na Magonjwa" na narratives zingine, zilitokana na barua zao wenyewe. It came from their correspondance.

Ilikuwa hivi: Wakiwa wana taarafiana kuhusu yanayojiri, walikuwa wakisema au kuwaambia wenzao Ulaya "Tunakufa na magonjwa huku"
Na walikufa wengi kweli, (RIP)kwa sababu walikuja bila ya madawa yao, it was their Genuine concern ya maisha yao, sio ya Waafrika.

Na Wengine walikuwa wakilalamika kwamba "Tuna laana"
Hayo yaliandikwa na vijana wengi tu waliotumwa kuja kufanya tafiti za kuzamia huku na kwa sababu ya mauaji ya halaiki waliyofanya wakifanya yafiti hizo and so on, na ile guilt, ndio iliwapeleka kusema "Tuna laana" the rest is history na walikuja kupindisha.
Na walivyoona narrative hiyo inawapa athari chanya, wakaacha iwe hivyo. U

Ushahidi upo, tafuteni mtapata, waliyokuwa wakifanya.
 
Wazungu walifanya Utu tu wa Kibinadamu wa kutuacha tujitawale.
Wangependa hadi hii leo wangeendelea kututawala.
Nafikiri suala la wazungu kutupatia uhuru lilikua na manufaa zaidi kwao kuliko kuendelea kututawala.

Unajua kumtawala mtu directly ina gharama kubwa sana kuliko kumpa "uhuru" ajitawale mwenyewe, huku wewe ukiendelea kuvuna kila unachotaka kutoka kwake kwa bei unayoitaka wewe au bure kabisa.
 
Hii naileta bila salamu!
Karne ya 17 na 18 wazungu ndipo walipogundua teknolojia nyingi.
Vitu ambavyo wazungu walivumbua Karne ya 17 -18 mpaka sasa Waafrika hatujagundua mithili ya hivyo. Tunapeleka watoto shule Ili waweze kutumia vitu ambavyo wazungu walivumbua miaka zaidi ya 300 nyuma .
Teknolojia ya kamera na picha mgando Wazungu waliigundua miaka karibu mia 4 iliyopita , imeboreshwa na kuboreshwa zaidi na itazidi kuboreshwa lakini sisi kazi yetu ni kuanzisha vyuo vya kufundishana namna ya kutumia.
Ingini za magari/mitambo ziligundulika miaka mingi imepita sisi kazi yetu ni kufungua vyuo vya kufundishana namna ya kuzitumia au kubadilisha kifaa kilichokufa kwenye hiyo engine.
Sasa Waafrika tuwe na kalenda yetu ambayo itatupa mwongozo wa wapi tuanzie.
Leo hii kuna vyuo vya kufundishana namna ya kutengeneza ingini za ndege, kiuhalisia sio kutengeneza bali ni kufanya service na kubadilisha vifaa vidogo vidogo.
Sasa ni vurugu mechi , tumepokea mambo ya Karne ya 21 ambayo kwa uhalisia sisi tuko huko Karne ya 15-16.
Mabadiliko yeyote yanapatikana kwa kusoma. Hata hivyo tuna changamoto ya mitaala bandia.

Kwa uoni wangu kama taifa tuwekeze kwa kuanzia kufundishwa masomo mawili tu kuanzia darasa la kwanza.

Hesabati, lugha (kizungu, kichina) yawe compasary.

Sekondary yaongezwe masomo mawili yafundishwe kwa vitendo kwa 80%

Computer na mechatronics

Sambamba iwepo sera ya kupunguza importation na kwa kuanzia vyombo vya umeme vya jikoni
 
Wazungu walifanya Utu tu wa Kibinadamu wa kutuacha tujitawale.
Wangependa hadi hii leo wangeendelea kututawala.
Tena utu wa kinafki coz waliona kuendesha makoloni hailipi so wakageukia ukoloni wa remote control.Leo hii anayeweza kupambana na waliokua wakoloni wake ni mmarekani tu ila sisi wengine hatuna jeuri.
 
Wazungu tumewafundisha mbinu za Kivita.Vita za misituni.... Camouflage.

Wao walikuwa wanakimbizana tu na kukatana mapanga bila mipangilio.

Walivyotokea kwetu ndio walijua hawajui.

Kuna movie moja inaonesha mtu wa stone age anavyohangaika kukamata samaki, kaingia kwenye maji ya kina kifupi na rundo la mawe ya kupopolea samaki wanaokatiza karibu...
 
Hivi mkuu wakoloni wote waliotutawala wakaamua kuwa leo hii kila mmoja arudi kutawala koloni lake Afrika tutawafanya nini?
Kwa kweli nikisema najua, nitakuwa nadanganya.

Hatahivyo ninachojua, we are fighting(Resisting) for lack of a better word... kuna vitu tunafanya, mfano tunaunda Umoja kama vile AU....ni matokeo ya resistance. Our collective efforts.

Itoshe, kwa sasa hawawezi kufanya hivyo kwa sababu za Kiuchumi. Watafilisika

Sababu nyingine, watashindwa kutawala kwa amani nchini mwao kwa sababu dunia ya sasa ni ya mchanganyiko wa watu, na hivyo wanaweza kupata upinzani wa ndani ambao utafanya jambo hilo kuwa counter intuitive(swahili kapuni hapo)

Ila basi, bado wanaendelea kufanya hivyo,(dominating) kupitia njia zingine kama za kiuchumi na kijamii.
 
Hii naileta bila salamu!
Karne ya 17 na 18 wazungu ndipo walipogundua teknolojia nyingi.
Vitu ambavyo wazungu walivumbua Karne ya 17 -18 mpaka sasa Waafrika hatujagundua mithili ya hivyo. Tunapeleka watoto shule Ili waweze kutumia vitu ambavyo wazungu walivumbua miaka zaidi ya 300 nyuma .
Teknolojia ya kamera na picha mgando Wazungu waliigundua miaka karibu mia 4 iliyopita , imeboreshwa na kuboreshwa zaidi na itazidi kuboreshwa lakini sisi kazi yetu ni kuanzisha vyuo vya kufundishana namna ya kutumia.
Ingini za magari/mitambo ziligundulika miaka mingi imepita sisi kazi yetu ni kufungua vyuo vya kufundishana namna ya kuzitumia au kubadilisha kifaa kilichokufa kwenye hiyo engine.
Sasa Waafrika tuwe na kalenda yetu ambayo itatupa mwongozo wa wapi tuanzie.
Leo hii kuna vyuo vya kufundishana namna ya kutengeneza ingini za ndege, kiuhalisia sio kutengeneza bali ni kufanya service na kubadilisha vifaa vidogo vidogo.
Sasa ni vurugu mechi , tumepokea mambo ya Karne ya 21 ambayo kwa uhalisia sisi tuko huko Karne ya 15-16.
Ni kweli kabisa tupo nyuma sana na wazungu.
 
Hadi leo Umeme na Maji tu ya Uhakika katika mji Mkuu wa biashara Daresalam ni kwamba tumeshindwa.
Tunaweza nini sasa zaidi ya kupata A za mchongo darani ?
Na kuvaa suti
Ha ha. Unaweza kutumia JF na A za Darasani.

Na unaweza ona umeme ni kila kitu lakini ukitizama kwa Undani, imemletea umasikini mtu wa Kawaida.

Halafu nimecheka kidogo, sasa kuvaa suti si ndii wanasema "Ustaarabu" Miaka ya Nyuma ulaya walikuwa wakicheza kambumbu na suti Lol
 
Back
Top Bottom