Braza Kede
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 3,840
- 6,844
kama ni kalenda basi afrika kalenda yetu inabidi ianzie miaka ya 60 sio hiyo miaka 300 uko nyuma. miaka 300 nyuma mtu mweusi alikuwa bidhaa akiuzwa sokoni kama unavyonunua nyanya leo.Hii naileta bila salamu!
Karne ya 17 na 18 wazungu ndipo walipogundua teknolojia nyingi.
Vitu ambavyo wazungu walivumbua Karne ya 17 -18 mpaka sasa Waafrika hatujagundua mithili ya hivyo. Tunapeleka watoto shule Ili waweze kutumia vitu ambavyo wazungu walivumbua miaka zaidi ya 300 nyuma .
Teknolojia ya kamera na picha mgando Wazungu waliigundua miaka karibu mia 4 iliyopita , imeboreshwa na kuboreshwa zaidi na itazidi kuboreshwa lakini sisi kazi yetu ni kuanzisha vyuo vya kufundishana namna ya kutumia.
Ingini za magari/mitambo ziligundulika miaka mingi imepita sisi kazi yetu ni kufungua vyuo vya kufundishana namna ya kuzitumia au kubadilisha kifaa kilichokufa kwenye hiyo engine.
Sasa Waafrika tuwe na kalenda yetu ambayo itatupa mwongozo wa wapi tuanzie.
Leo hii kuna vyuo vya kufundishana namna ya kutengeneza ingini za ndege, kiuhalisia sio kutengeneza bali ni kufanya service na kubadilisha vifaa vidogo vidogo.
Sasa ni vurugu mechi , tumepokea mambo ya Karne ya 21 ambayo kwa uhalisia sisi tuko huko Karne ya 15-16.
nchi nyingi za afrika zilipata uhuru wa bendera miaka iyo ya 1960. kipindi icho jamii nyingi ziliishi maporini ndomaana nyerere alifukuza watu waende mijini na karibu na barabara kuu ndo vijiji na hii miji ya leo vikazaliwa.
sisi sio wavumbuzi ndomaana hata leo vile vijiti vya kuchokonolea meno tunaletewa kutoka nje ya nchi. we mwenyewe apo ulipo jikague kuanzia chupi adi mavazi mengne uliyovaa utakuta vyote ni vya nje ya afrika kwa asilimia mia.
waafrika tunachoweza ni mambo ya sanaa yani kuimbaimba, kunengua, ngoma, sarakasi, ulozi, fitina, majungu, kupiga blaabla.
kiasili mwafrika ni kiumbe wa kula bata(starehe) na mitelezo tu hapendi kazi ndomaana hata leo ukienda kwa jamii zinazokaa maporini kama wale wahazabe utakuta ratiba zao ni kwenda kusaka wanyama maporini na kurudi hom kucheza ngoma na kupiga stori. ulaya na marekani weusi ndo mastaa kwenye miziki na burudani kwa ujumla wake. hao ndo sisi.