Waafrika hatuwezi uongozi, tuwape wazungu nchi zetu watuongoze

Waafrika hatuwezi uongozi, tuwape wazungu nchi zetu watuongoze

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Kuna kitu nimekitafakari sana, kwanini sisi Afrika hatuna maendeleo? Nikaja kutambua kuwa, viongozi wetu wengi wa Afrika hawana ufahamu kuhusu uongozi wa ulimwengu, ndiyo maana tupo nyuma kwa kila kitu.

Hivi fikiria ka inchi kama Qatar kanatuzidi uchumi sisi! Palipo na ukweli lazima pasemwe, Afrika tuwape tena wazungu nchi zetu watuongoze kwa mara ya pili ili tupate akili vizuri, maana inaonekana tuliomba uhuru wakati bado vichwani mwetu hatuna ufahamu.

Sisi Kongo 2023 tunaanza na Moise Katumbi!
 
Kuna kitu nimekitafakari saana kwanini sisi africa hatuna maendeleo?

Nikaja kutambuwa kuwa viongozi wetu wengi wa africa hawana ufahamu kuhusu uongozi wa ulimwengu ndo maana tupo nyuma kwa kila kitu..
Tanzania tunaongozwa hata na wagonjwa wa akili
 
"Muafrika hawezi kujitawala"Botha

Afrika ndo bara pekee mtu anapewa uongozi kwa majaribio au kwa bahati nasibu.

Teuzi nyingi hufanywa kwa ajili ya mtu kuwa mtiifu sio uwezo na taaluma.

Afrika wajinga ndo viongozi na werevu ndo wafuasi.

Ni dhambi kubwa Sana kumwambia kiongozi wa Afrika ukweli.
 
Tatizo kubwa la sisi waafrika ni kuruka stage kwenye zile hatua za maendeleo ya binadamu:
1. Primitive communalism
2. Slavery
3. Feudalism
4. Capitalism
5. Socialism

Kihistoria, jamii zilipohama kutoka stage moja kwenda nyingine, walikua wamekomaa KIAKILI kuona umuhimu wa hayo mabadiliko!

Sisi tulirushwa kutoka hatua ya kwanza mpaka ya 5, huku baadhi ya nchi zikirukia ya 4. Matokeo yake akili zetu bado zipo kati ya hatua ya 2 na ya 3. Viongozi wetu wanachowaza ni "accumulation of wealth" (feudalism) na kuwanyonya wengine kwa manufaa binafsi (slavery).
 
Kuna kitu nimekitafakari saana kwanini sisi africa hatuna maendeleo?

Nikaja kutambuwa kuwa viongozi wetu wengi wa africa hawana ufahamu kuhusu uongozi wa ulimwengu ndo maana tupo nyuma kwa kila kitu...
Mawazo gani haya? Mtafute mzungu basi umpe familia yako kwanza.🙏🙏🙏
 
Tatizo kubwa la sisi waafrika ni kuruka stage kwenye zile hatua za maendeleo ya binadamu:
1. Primitive communalism
2. Slavery
3. Feudalism
4. Capitalism
5. Socialism

Kihistoria, jamii zilipohama kutoka stage moja kwenda nyingine, walikua wamekomaa KIAKILI kuona umuhimu wa hayo mabadiliko!

Sisi tulirushwa kutoka hatua ya kwanza mpaka ya 5, huku baadhi ya nchi zikirukia ya 4. Matokeo yake akili zetu bado zipo kati ya hatua ya 2 na ya 3. Viongozi wetu wanachowaza ni "accumulation of wealth" (feudalism) na kuwanyonya wengine kwa manufaa binafsi (slavery).
Post yenye maumivu. Lkn ndio ukweli wenyewe [emoji22]
 
Mwaka 1945,kuna Filed Mashal Jenerali wa kivita ya Uingereza anaitwa Bernard M.... alipingana na wazungu wenzake waliopinga kuwapa UHURU waafrika,kuwaambia.

"waafrika wanataka UHURU wapeni lakini awatafika mbali hawatoweza kujitawala, wataishia kupigana, ufisadi, kuganyika kwa sababu ya tamaa, Ili mwafrika aweze kujitawala inafaa aushinde ubinafsi" ( Bernad M,1945 )
 

Attachments

  • Screenshot_20220824_073904.jpg
    Screenshot_20220824_073904.jpg
    87.9 KB · Views: 7
Kuna kitu nimekitafakari saana kwanini sisi africa hatuna maendeleo?

Nikaja kutambuwa kuwa viongozi wetu wengi wa africa hawana ufahamu kuhusu uongozi wa ulimwengu ndo maana tupo nyuma kwa kila kitu

Hivi fikiria ka inchi kama Qatar kanatuzidi uchumi sisi

Kwa hiyo palipo na ukweli lazima pasemwe Africa tuwape tena wazungu inchi zetu watuongoze kwa mara ya pili ili tupate akili vizuri maana inaonekana tuliomba uhuru uku bado vichwani mwetu hatuna ufahamu

Sisi Kongo 2023 tunaanza na Moise Katumbi
Ungekuwa weye ndiyo kiongozi ungeupokea ushauri wako wa kijinga?
 
Njia sahihi wananchi tungekuwa na uwezo wa maamuzi ni sahihi kama tungeajiri management ya kutuongoza toka nje yaani Raisi na cabinet yake nzima hata kama tutawalipa mishahara mikubwa lakini watufanyie Kazi vizuri ikiwemo kusimamia vizuri kodi zetu. Kama tunaweza ajiri kocha toka nje kwann tusiajiri watu wa kutuongoza toka nje.

Kwa mfumo huu wa uongozi wa kiafrica tusahau kuhusu kuendelea. Afrika uongozi ni ajira binafsi na sio wito wa kuleta mabadiliko chanya kwenye Jamii.

Bado miaka 40 kesho tu Afrika itasherekea jubilee ya UHURU.
 
Au tufanye kama walivyofanya waarabu wao sekta nyingi za uzalishaji wamewakabidhi foreigner ndio wanasimamia wao wanapokea tu asilimia zao na nchi zao zinaenda kwa maendeleo. Wanaoijenga emirates sio waarabu.

Walioijenga Korea kusini, Singapore, Malaysia, Taiwan, Hongkong, Japan ni foreigners. So sisi waafrika sio wa kwanza kutumia mfumo huu wa kuajiri foreigners kusimamia uchumi na maendeleo ya nchi na maendeleo yameonekana.
 
Hivi ninyi watu,leo mmelogwa?Mawazo gani sasa hayo?😂😂😂
Mfumo uliopo SAsa ni miaka 60 SAsa hakuna positive changes, umeshindwa kutuvusha,hauzalishi viongozi wabunifu, kama tunashindwa kutatua changamoto zetu kwa kutumia raslimali tele kwann tusibadili aina ya mfumo wa uongozi.

Una raslimali tele eti watu wako wanakosaje ajira SAsa halafu unajiita kiongozi. Unaendesha na upandaji mafuta duniani, huna akili ya kuzalisha nishati mbadala mbona malighafi tele zimejaa nchini kwako zitumie.

.Unakamua kodi na tozo watu masikini ambao hata tu mlo mmoja kwa siku ni tabu huku raslimali tele zimejaa, mbona mkoloni hakutegemea kodi kuendesha nchi na alituletea maendeleo makubwa Sana?

Eti karne hii watu wako wanaishi kwenye nyumba za nyasi na udongo utadhani panya then unalala na kuamka kwa amani unajiita kiongozi?
 
Back
Top Bottom