Waafrika hatuwezi uongozi, tuwape wazungu nchi zetu watuongoze

Waafrika hatuwezi uongozi, tuwape wazungu nchi zetu watuongoze

Huzuni zaidi ipo Africa kusini.mzungu katawala na kuiweka nchi imekaa Gawiza kiuchumi lakini kuingia mtu mwindo madarakani 1992 nchi imerudi nyuma vibaya sana.wizi wa .ali ya umma kila uongozi.sasa huko bora atawale mzungu kukiko.mtu mwindo.
 
Wapigania UHURU walipigania maslai yao binafsi zaidi kuliko maslai ya waafrika wote kwa kuwahadaa waafrika wawape sapoti wawafukuze wakoloni Ili waafrika wote wale mema ya nchi,kumbe lengo lilikuwa ni wao ndio walambe asali.

Vijana wa kiafrica wanakufa bahari kwa kuzikimbia nchi zao zenye raslimali tele huku vijana wa China wao wakizidi kujazana nchi za kiafrica kwa msaada wa serikali yao kuja kupora raslimali tele ambazo vijana wa kiafrica wao ni vipofu hawana macho ya kuona sababu ya uongozi mbovu.
 
Sio kweli, Socialism haikutufaa kabisa Waafrika, haukuwa mfumo sahihi kwetu katika kipindi chochote
Tatizo kubwa la sisi waafrika ni kuruka stage kwenye zile hatua za maendeleo ya binadamu:
1. Primitive communalism
2. Slavery
3. Feudalism
4. Capitalism
5. Socialism

Kihistoria, jamii zilipohama kutoka stage moja kwenda nyingine, walikua wamekomaa KIAKILI kuona umuhimu wa hayo mabadiliko!

Sisi tulirushwa kutoka hatua ya kwanza mpaka ya 5, huku baadhi ya nchi zikirukia ya 4. Matokeo yake akili zetu bado zipo kati ya hatua ya 2 na ya 3. Viongozi wetu wanachowaza ni "accumulation of wealth" (feudalism) na kuwanyonya wengine kwa manufaa binafsi (slavery).
 
Shida ya Waafrika hatutaki tuongozwe na wenye akili tunataka wale tutakao kwiba pamoja🏃
Unajua kwann viongozi wa kiafrica miradi mingi upenda kuwapa Wachina jibu ni Ili iwe rahisi kuiba nao,Mchina katumwa pesa Afrika wamekuja afrika wamekutana na watawala wezi wamefunga ndoa,Mchina ubalika kuendana na mazingira wakiwa kwao na Ulaya wanajenga kwa standard na uogopa rushwa,wakija Afrika wamekuja kiwandani kabisa kwenye ufisadi wanafunga na ndoa kabisa ya wizi na watawala wa kiafrica.
 
Ccm inasema inaleta maendeleo kwa kasi ya ajabu na maendeleo yanamwagika mwaaaaaa .Pia Shaka anasema ccm Ibaki madarakani milele..

Uzi upewe jina la M Z U N G U.
 
Kuwa na mfumo wa kuendesha nchi kwa miaka 60 then hauna tija, yanini kuendelea nao huku ukijua unakupeleka kuzimu, kama tu Mjerumani alitawala kwa mda mfupi na akajenga miji yote nchini kwa mda mfupi tena bila kutegemea kodi. Sisi tunashindwa nini hali KILA kitu kipo, pesa zipo, masoko sio ya kuuliza ndani na nje,nguvu Kazi tele vijana kibao hawana ajira, raslimali tele zimejaa kuanzia ardhi, maji, madini, nk. Nini SAsa tunashindwa, jibu ni kwamba tumekosa mfumo wa kujisimamia.
 
Siku zote nimekuwa nikijiuliza whats wrong with Africans? Ukirudi nyuma sana ukamsoma Walter Rodney namheshimu huyu msomi wetu wa afrika katika kitabu chake cha how europe underdeveloped Africa. Ameelezea mengi yakiwepo malalamishi mengi tu kama kawaida yetu tukiwalaumu wazungu n.k .

Nikija kusoma habari zetu waafrika na ukisoma pia Heart of darkness utaona sisi waafrika toka miaka na miaka tuna matatizo. Ukiona hivyo havifai nenda kasome the River between, No longer at easy and Things fall apart utaona hata waafrika wenzetu wanakiri tuna tatizo. Miaka na miaka tumekuwa tulilalamika wazungu wametutawala nikawa najiuliza nikitizama huko nyuma ukiangalia kwenye misafara ya utumwa wazungu/waarabu watano wanaswaga msafara wa waafrika wenye nguvu 50 n.k .

Najiuliza hawa babu zetu walikuwa wamerogwa na nani hata ufahamu wao haukuwa na uwezo wa kufunguka na kukataa hali hiyo dhidu ya waarabu na wazungu wachache wenye bunduki kadhaa na viboko? Zaidi nakuja kusikitika kuwa tulikuwa tunauzana sisi kwa sisi hapo ndo nachoka kabisa na kujiuliza kweli sisi si nyani? Sawa miaka hiyo tutaoa excuses nying sana turudi baada ya uhuru.

Nini kimefanyika?

Tumezifisadi nchi zetu na kuwatajilisha wazungu, wahindi, waarabu na sasa wachina. Hapa tunamsingizia nani? Baada ya uhuru nchi zetu zimeendelea kuudhalilisha uafrika ukiangalia mauaji ya Kimbari, ukiangalia Somali, Sudan, Congo, Centre Afrika, Nigeria, Libya, Syria n.k hapa tunaweza kutoa majibu mepesi ya kivivu kuwa wazungu wanatuchonganisha.

Tumeendelea kuuana wenyewe kwa wenyewe na kufisadi nchi zetu. Angalia viongozi wetu walivyojilimbikizia mali wao na familia zao. Akina Mobutu, Ghadaff, Kikwete, Mkapa, Bokassa n.k kana kwamba hawa wataish milele.Lakini haya yamekuwa hayaonekani kama ni tatizo. Ukisoma heart of darkness mwandishi anasema watu wa Congo ni Cannibal na ni kweli watu wa Congo walikuwa wanakula mbilikimo ni habari za kweli.

Huku Tanzania wanaua watu wenye albinism ili washinde kwenye chaguzi na pia kupata utajiri. Waafrika tulikosea nini tukapata laana hii? Ukiona watanzania wanapigana na kutaka kuuana kwa kutetea uarabu na uzungu utajisikia kichefu chefu. Bado waafrka hatujakua thamani ya ubinadamu na katika hili hatuoni vibaya kumwaga damu ya walio kinyume na mitizamo yetu ya kisiasa. Nenda Burundi, wanaokufa ni warundi hawa waafrika. Nenda Congo nenda Syria, Egypt n.k majibu mepesi utaambiwa wazungu wanatugombanisha.Waafrika ni kama ng'ombe tu hatuna tunaloweza amua.

Tunaswagwa tu kokote atakapo mwenye kutuchunga. Pengine wazungu wanajuta kwa kututawala miaka hiyo kwa kuwa walisababisha hata ndugu zao wafe, kumbe wangejikalia kwao na kuendelea kuchukua madini, mafuta na mazao yetu wakiwa wametulia tu sebuleni na ofisini mwao huku wanakunywa wine.

Mbona sasa tunawapelekea mpaka Twiga? Madini na kila watakacho. Ni hatari sana na aibu kuwa na akili za kiafrika. Na wazungu hawatak waone wanapatikana watu wenye akili kama zao.

Wanataka wapatikane wenye akili za kiafrika ili waafrika waendelee kuwa malofa.

Kuna sehemu tulikosea turudi nyuma sana kujichunguza.tujirekebishe.
 
Tanzanian yetu IPO imara na inasonga mbele kwa Kasi kubwa Sana chini ya uongozi wa mh Rais mama Samia suluhu Hassani, mh Rais inaipaisha nchi kimaendeleo kwa kujenga Miundombinu mbalimbali inayorahisisha maisha ya watanzania, Ndio maana unaona Tanzania ikiheshimika kwa Sasa na kupokea watalii na wawekezaji wengi Sana,

Diplomasia yetu imeimarishwa Sana na mh Rais mama Samia, Ndio maana unaona milango mingi inafunguka kwetu
 
Kuna kitu nimekitafakari sana, kwanini sisi Afrika hatuna maendeleo? Nikaja kutambua kuwa, viongozi wetu wengi wa Afrika hawana ufahamu kuhusu uongozi wa ulimwengu, ndiyo maana tupo nyuma kwa kila kitu.

Hivi fikiria ka inchi kama Qatar kanatuzidi uchumi sisi! Palipo na ukweli lazima pasemwe, Afrika tuwape tena wazungu nchi zetu watuongoze kwa mara ya pili ili tupate akili vizuri, maana inaonekana tuliomba uhuru wakati bado vichwani mwetu hatuna ufahamu.

Sisi Kongo 2023 tunaanza na Moise Katumbi!
Kama tunavyofanya kwenye makampuni mengi na yakafanikiwa
 
Kimbari, ukiangalia Somali, Sudan, Congo, Centre Afrika, Nigeria, Libya, Syria n.k hapa tunaweza kutoa majibu mepesi ya kivivu kuwa wazungu wanatuchonganisha
Iweka na Tanzania, uganda, rwanda
 
Tumeendelea kuuana wenyewe kwa wenyewe na kufisadi nchi zetu. Angalia viongozi wetu walivyojilimbikizia mali wao na familia zao. Akina Mobutu, Ghadaff, Kikwete, Mkapa, Bokassa n.k kana kwamba hawa wataish milele.Lakini haya yamekuwa hayaonekani kama ni tatizo.
Asante sana kwa uzi mzuri.
Afrikans nj matatizo
 
Kuna kitu nimekitafakari sana, kwanini sisi Afrika hatuna maendeleo? Nikaja kutambua kuwa, viongozi wetu wengi wa Afrika hawana ufahamu kuhusu uongozi wa ulimwengu, ndiyo maana tupo nyuma kwa kila kitu.

Hivi fikiria ka inchi kama Qatar kanatuzidi uchumi sisi! Palipo na ukweli lazima pasemwe, Afrika tuwape tena wazungu nchi zetu watuongoze kwa mara ya pili ili tupate akili vizuri, maana inaonekana tuliomba uhuru wakati bado vichwani mwetu hatuna ufahamu.

Sisi Kongo 2023 tunaanza na Moise Katumbi!
Mkishakula makande na kuvuta bangi chooni mnaaamua tu kuandika mnachotaka. Sasa kama una elimu hata ya Sekondari imekusaidia nini?

Hapo ulipo unaamini kuwa nchi za Ulaya na America hazina matatizo?
 
Huku Tanzania wanaua watu wenye albinism ili washinde kwenye chaguzi na pia kupata utajiri. Waafrika tulikosea nini tukapata laana hii? Ukiona watanzania wanapigana na kutaka kuuana kwa kutetea uarabu na uzungu utajisikia kichefu chefu. Bado waafrka hatujakua thamani ya ubinadamu na katika hili hatuoni vibaya kumwaga damu ya walio kinyume na mitizamo yetu ya kisiasa. Nenda Burundi, wanaokufa ni warundi hawa waafrika. Nenda Congo nenda Syria, Egypt n.k majibu mepesi utaambiwa wazungu wanatugombanisha.Waafrika ni kama ng'ombe tu hatuna tunaloweza amua.
Sababu ya Madaraka. Hata hapa bongo ukikaza kiwaudhi wanaondoka na koromeo lako fastaa.
 
Mkishakula makande na kuvuta bangi chooni mnaaamua tu kuandika mnachotaka. Sasa kama una elimu hata ya Sekondari imekusaidia nini?

Hapo ulipo unaamini kuwa nchi za Ulaya na America hazina matatizo?
Ukweli usemwe bwana. Afrika ni kichefu chefu. Unajua kwanini tz pesa zimeyeyuka? Mzigo mkubwa ulitumika kwenye uchaguzi 2020 na tuliwambia kitakachifata baada ya hapo ni kilio sasa imethibitika.
 
Au tufanye kama walivyofanya waarabu wao sekta nyingi za uzalishaji wamewakabidhi foreigner ndio wanasimamia wao wanapokea tu asilimia zao na nchi zao zinaenda kwa maendeleo. Wanaoijenga emirates sio waarabu.

Walioijenga Korea kusini, Singapore, Malaysia, Taiwan, Hongkong, Japan ni foreigners. So sisi waafrika sio wa kwanza kutumia mfumo huu wa kuajiri foreigners kusimamia uchumi na maendeleo ya nchi na maendeleo yameonekana.
Hizi ulizoandika ni pumba tu kama unadhani Tanzania imesimama palepale tokea uhuru. Nisikulaumu pengine wewe umezaliwa baada ya mwaka 2000
 
Kuna kitu nimekitafakari sana, kwanini sisi Afrika hatuna maendeleo? Nikaja kutambua kuwa, viongozi wetu wengi wa Afrika hawana ufahamu kuhusu uongozi wa ulimwengu, ndiyo maana tupo nyuma kwa kila kitu.

Hivi fikiria ka inchi kama Qatar kanatuzidi uchumi sisi! Palipo na ukweli lazima pasemwe, Afrika tuwape tena wazungu nchi zetu watuongoze kwa mara ya pili ili tupate akili vizuri, maana inaonekana tuliomba uhuru wakati bado vichwani mwetu hatuna ufahamu.

Sisi Kongo 2023 tunaanza na Moise Katumbi!
Africa hatuna viongozi tunawatawala tupu, mafisadi, undugu, utapeli, wizi, ushirikina, kujuana na upendeleo wa kijinga.
 
Ukweli usemwe bwana. Afrika ni kichefu chefu. Unajua kwanini tz pesa zimeyeyuka? Mzigo mkubwa ulitumika kwenye uchaguzi 2020 na tuliwambia kitakachifata baada ya hapo ni kilio sasa imethibitika.
Ndiyo maana dikteta aliamua kufa mapema sn
 
Kuna kitu nimekitafakari sana, kwanini sisi Afrika hatuna maendeleo? Nikaja kutambua kuwa, viongozi wetu wengi wa Afrika hawana ufahamu kuhusu uongozi wa ulimwengu, ndiyo maana tupo nyuma kwa kila kitu.

Hivi fikiria ka inchi kama Qatar kanatuzidi uchumi sisi! Palipo na ukweli lazima pasemwe, Afrika tuwape tena wazungu nchi zetu watuongoze kwa mara ya pili ili tupate akili vizuri, maana inaonekana tuliomba uhuru wakati bado vichwani mwetu hatuna ufahamu.

Sisi Kongo 2023 tunaanza na Moise Katumbi!
Zambia na Ghana wamewahi kuwa na viongozi wazungu,kuna jipya walifanya?
 
Back
Top Bottom