Waafrika kujikuta tunaishi Afrika Wala si Bahati mbaya,ni sahihi kabisa na tena tushukuru

Waafrika kujikuta tunaishi Afrika Wala si Bahati mbaya,ni sahihi kabisa na tena tushukuru

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2021
Posts
2,753
Reaction score
12,932
Nsikuchoshe na Usinchoshe, Tusichoshane!


Kuna wakati huwa nalaumu sana lakini kwakuwa nina IQ kubwa,nimekuja kugundua sisi waafrika kujikuta tupo kwenye hili Bara la Afrika,ni jambo ambalo inapaswa Tushukuru usiku na mchana!

Bara la Afrika ni bara ambalo linaendana sawia na akili ya mwafrika,yaani hili Bara liliandaliwa Kwa ajili yetu Waafrika kwasababu ni bara ambalo ni chomeka ni kuchomekee,tungeishi Mabara ambayo ingekuwa ni twanga nikutwange sidhani kama Kuna mwafrika angesavaivu!

Hebu fikiria tu Kwa akili ya haraka haraka,Je endapo tungejikuta tunaishi Pale Dubai ambapo ni jangwani,Je Kuna raia angepona?,naamini sote tungekufa Kwa Kiu Cha maji,Kama tunaishi tu hapa Afrika ambapo tumezungukwa na Mito ya kutosha pamoja na maziwa kila mahali lakini bado Kuna watu wanaangamia Kwa Kiu,Je pale Jangwani tungetoboa!

Fikiria tu ya kwamba,tungejikuta tunaishi huko kwenye Mabara yaliyokuwa na Vimbunga vya kutosha,Kuna mtu angetoboa?,kama hapa tu Afrika mvua zikipiga za Upepo kidogo yanakuwa majanga na hakuna msaada wowote ndiyo tungekuwa huko tungetoboa?

Fikiria tu endapo tungekuwa tunaishi kwenye Mabara ambayo Yana baridi Kali na kudondosha barafu,Je tungetoboa?,kwa Tanzania tu hapo Makambako na Makete kwenye Baridi ya kawaida watu walikufa kishenzi na UKIMWI wakiamini kupigana miti ndiyo chanzo Cha nishati ya kuongeza joto na kuondoa baridi,Je tungekuwa kwenye Mabara mengine Hali ingekuwaje?,bila shaka jibu unalo!

Fikiria tu ya kwamba,tumezungukwa na kila aina resources ambazo zinaweza kutupatia chakula ikiwemo Ngano,halafu hapo hapo tunaaagiza Ngano nchi kama Urusi na Ukraine ambazo kijiografia ni kama semi arid,yaani unashindwa kulima Ngano kwenye rutuba tele ambalo umebarikiwa na maji ya kutosha halafu unaagiza Kwa ambao wanailima Kwa taabu,Sasa Jiulize kama hapa tumeshindwa,Je tungeishi huko kwenye semi arid tungetoboa!


Namna unavyoiona Afrika,tafsiri yake ni kwamba,ndivyo akili ya mwafrika ilivyo!
 
Kama mtu hata ikiwa kilaza wakiwago cha juu sana ikipata urais wa dodokea, anapaga team na kikudi cha kumsadia ili ashide wakati kwa akili za kawaida haistaili hata kupitishwa na chama chochote cha siasa.
 
Back
Top Bottom