Waafrika ni muda sasa wa kurudia kuabudu Mizimu yetu

 
Waafrika wamekuwa masikini kwa sababu ya kuendekeza mizimu
 
Duniani watu wanakwenda kwenye UJAHILIA .Wanaotaka kwenda kuabudi MIZUMU lkn itabidi hata nguo musivae tena nguo zimeletwa na waarabu pamoja na dini .
 
Toa iyo avata ndo tubishane
Hahaha avatar isikutishe maana mie ni mtu wa mixa,,,, na tena sipo kwenye huu ukristo wa wamagharibi ambao umejaa upotoshaji,,,, huyo ni kirill wa urusi wa kanisa la mashariki nachanganya mizimu na ukristo wenu maana nimeona nao ni ibada ya mizimu tu sema kwakua wamepewa majjna ya kizungu wanaitwa saints/watakatifu basi mkaridhika mie mababu zangu na mizimu ya kwetu nao ni watakatifu na nawaomba kama mnavyoomba hao watakatifu wa kizungu sababu najua mtu mweusi alimjua mungu kabla hata kuletewa hizo dini za wageni na sikikuu zenu za kidini nazitumia kama sikukuu/matambiko kwa wazee
 
Sasa mkuu Exodus 22:2
Inazungumzia kuhusu kuua mwizi.

Ni hivi kuna Murder na Killing hivyo ni vitu viwili tofauti, mahakamani unaweza kwenda na umeua na ukaachiwa huru...
 
Kumbe ni mtu wa misa 🤣🤣sasa kumbe hadi kanisani unaendaga kumbe
 
Ujui ulicho kiandika sababu mpaka sasa robo tatu ya watu bado waabudu mizimu na binadamu wenye hela robo tu ya watu ndio wanao muabudu muumba wa kweli

Tofaoti iliopo kwa zama hizi na zakale babu zetu walijiweka wazi bila kuficha zama izi watu wanajificha kwenye dini lakini wacho kiabudu wanakuja wao

Enzi za mkwawa na mwana marundi ubaguzi ulikuwepo tena mbaya zaidi ya huu
 
Hata hivyo kiuhalisia bora hali ilivyo sasa, lakini tukisema turudi kwenye dini zetu hali ingekuwa mbaya, makabila karibu 120 Kila mmoja na dini yake imagine, Leo hii watu wa makabila mbalimbali wanaweza kupatana kwasababu ni wakristo au waislamu, Bora kuwe na pande mbili zinazozozana ambapo kutuliza migongano inaweza kuwa rahisi kuliko kuwa na dini 120 ambazo kukitokea migongano hasa ikiwa kwenye Karne hii ya sayansi na teknolojia na uwazi plus kujitambua kutazuka balaa kubwa ambalo ili liishe lazima dini karibu 100 zihusike in which is impossible.

Hata kiutawala itakuwa ni ngumu mno. Kumbuka dini zetu zile zinakwenda sambamba na makabila au ukabila hivyo jambo baya kutokea miongoni mwa makabila ni dakika sifuri tu tena hapo hujasema influence ya mataifa makubwa kwenye kutuchanganya vizuri kiutamaduni.

Kwa kuwa wengi wetu TZ hatujitambui hizi dini mbili kubwa zinatosha kabisa, dini zaidi ya 100 Kwa jamii isiyojitambua ni mzigo mzito mno. Fikiria mtu anasema kuwa wenye dini Yao aidha wayahudi au waarabu wanauana so what?, kwani sisi Babu zetu na dini zao walikuwa hawauani aidha kutoa makafara ya watu au hata zile vita za makundi ya kikabila, kule kaskazini mbona walikuwa wanapigana hadi machifu wa kabila moja na kuuana kabila moja licha ya hizo dini za mizimu kuwepo.

Hivyo, mapigano kama Yale ya mashariki ya kati dini zinakuwa ni kama kisingizio tu. Watu wana mahangaiko Yao hapa duniani wanaamua kuuana tu, waache wauane maana Kila mmoja ana EGO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…