Waafrika tulipotoshwa kuhusu Chifu Mangungo wa Msovero sio mjinga, Watanzania tuiombe familia yake msamaha na tumuenzi kama shujaa wa uwekezaji

Waafrika tulipotoshwa kuhusu Chifu Mangungo wa Msovero sio mjinga, Watanzania tuiombe familia yake msamaha na tumuenzi kama shujaa wa uwekezaji

Mangungo alikuwa more intelligent than some of our member of parliament particularly from rulling party
 
Mtoa mada umechemka vibaya sana. Kwanza tambua ya kwamba hilo jina la mwekezaji sijui wawekezaji yamekuja sasahiv kwa kuzingatia mutual benefits za kibiashara lakini enzi hizo za ukoloni hakukuwa na terminology mkoloni simply unaona mpaka hapo Dkt Karl Peters alikuwa ni mkoloni persee aliyeamua kutumia njia ya kumlaghai Mangungo kwasababu aliona ni njia rahisi na ni effective zaidi.

References zinadai katika makubaliano hayo, mostly kulikuwa na kuhadaiwa kwa kiongozi wetu wa kimila yani Chief Mangungo kwani alitia wino kukubali mkataba uliokuwa na mda mrefu zaidi (historia zinasema ni zaidi ya miaka 100) ina mana bila kupata uhuru wetu mpka leo hii tungekuwa chini ya huo mkataba. Chief Mangungo hakuelewa lugha ya kingereza nashangaa ni wapi unasema alikuwa na mkalimani anaemtafria, really???? Huyo mkalimani yeye alisomea wapi hicho kingereza???

History zinadai kuwa Mangungo kusaini mkataba ule japo hakuuelewa ilikuwa ni kutokana na kuuhofia utawala wa wajerumani kwani kwa hakika kabisa kama angeamua kuugomea ni wazi angrlazimika kuingia kwenye battlefield na mjerumani kitu ambacho alitafakari akaona hakiwezi hivo ndipo akaamua kusain kama submission ya mapema kwa wakoloni. Ikumbukwe pia enzi hizo stories za kuingia kwa wakoloni maeneo tofauti tofauti ya Africa hususani tanyanyika yalikuwa yanafamika hivyo baadhi ya watawala walikuwa na taarifa za uwezo wa wakoloni kivita kama ukiamua kwenda nao against hivyo machifu wengine walianza kuingiwa na woga wa kupambana nao.

Katika kusamarize, ni kwamba chief mangungo hakusaini kwa kuridhia au hiari ni kwamba aliwahofia wajerumani. Karl Peters alikuwa ni moja ya wakoloni wa kijerumani katili sana kipindi hicho hadi kuna maeneo mengine alifamika kama "mkono wa damu" so ni wazi machief kama mangungo walimu underfier kuingia nao frontline kwenye uwanja wa mapambano. Muhimu zaidi ni kwamba usijaribu kumtetea chief wetu kwa kosa alilolifanya. Ukweli ni kwamba alifanya kosa japo ni kwa shinikizo la kuwahofia wajerumani na nguvu zao kipindi hicho. Tuwe tunajifunza kwa mistakes za wazee wetu ili tusije kurudia makosa yale ktk karne hii ambayo sisi vizazi vyao tuna uelewa na pia tuna uhuru wa kuamua kushirikiana au kutoshirikiana kwenye mikataba mbali mbali ya kimaendeleo. Sasa inashangaza sana bado karne hii tunaingia tena mikataba ya miaka sijui 100, sijui 99 dah inafikirisha sana kwakweli.
 
Chifu mangungo hakuwa mjinga, watanzania tulipotoshwa, tunapaswa kuiomba familia yake msamaha

Kwa miaka mingi sana chifu mangungo ameendelea kuonekana kama mfano wa kiongozi mjinga hasa pale linapotokea swala la mikataba. Lakini je Mangungo alikuwa mjinga kweli?

Chifu mangungo ni nani?

Naomba ninukuu kidogo kipande cha historia fupi kuhusu chifu Mangungo kutoka katika uzi wa ndugu humu Jf KILABA

"Mangungo simultaneously for all his people and Dr. Peters for alt his present and future associates hereby concluded a treaty of Eternal Friendship.

Mangungo offers all his territory with all its civil appurtenances to Dr. Karl Peters, as the representative of the Society for German Colonization, for the exclusive and universal utilization for German colonization.

Dr. Karl Peters, in the name of the Society for German Colonization declares his willingness to take over the territory of the Sultan Mangungo with all rights for German Colonization subject to any existing suzerainty of Mwenyi Sagara.

In pursuance thereof, Sultan Mangungo hereby cedes all the territory of Msovero, belonging to him by inheritance or otherwise for all time, to Dr. Karl Peters, making over to him at the same time all his rights.

Dr. Karl Peters in the name of the Society for German Colonization undertakes to give special...attention to Msovero when colonizing Usagara.

This treaty has been communicated to the Sultan Mangungo by the interpreter Ramzan in a clear manner and has been signed by both sides, with the observation of the formalities valid in Usagara the Sultan on direct enquiry having declared that he was not in anyway dependent upon the Sultan of Zanzibar, and that he did not even know the existence of the latter.

Sgd. Dr. KARL PETERS
Sgd. MANGUNGO

This contract has been executed legally and made valid for all time before a great number of witnesses, we testify herewith:
Kwagakinga (mark);
Sultan Mangungo’s son of Golola (mark);
Sultan Mangungo’s second son of Draman (mark);
Graf Pfeil August Otto;
Mark of the intepreter Ramazan etc.
Dr. Karl Juhlke.
Msovero Usagara November 29, 1884.

Kwa tafsiri isiyo rasmi, kwa Kiswahili unasomeka hivi:
Mangungo, Sultan wa Msovero katika Mwenyisagara, na Dk. Karl Peters. Mangungo sambamba na watu wake wote na Dk. Peters kwa niaba yake na washirika wake wengine wajao kwa pamoja wanaweka mkataba wa Urafiki wa Kudumu.

Mangungo amekubali kutoa himaya yake yote pamoja na watu wake na hadhi yake kwa Dk. Karl Peters, kama mwakilishi wa Umoja wa Ukoloni wa Kijerumani (Society for German Colonization), kwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja ya koloni la Kijerumani.

Dk. Karl Peters, kwa niaba ya jina la Umoja wa Ukoloni wa Ujermani anatangaza dhamira yake ya kuitwaa himaya yote ya Sultan Mangungo na haki zote kwa ajili ya Koloni la Ujerumani inayohusisha kila kona na amali za Mwenyi Sagara.

Katika kutekeleza hilo, Sultan Mangungo anakabidhi himaya yote ya Msovero, inayomilikiwa na yeye mwenyewe kwa urithi au kwa namna yoyote ile kwa nyakati zote, kwa Dk. Karl Peters, na wakati huo huo kumkabidhi haki zake zote.

Dk. Karl Peters kwa niaba ya Umoja wa Ukoloni wa Kijerumani anakusudia kuweka mkazo maalum kwa eneo la Msovero wakati wa kuitawala Usagara.

Mkataba huu umewasilishwa kwa Sultan Mangungo na mkalimani Ramzan katika dhana ya wazi kabisa na umesainiwa na pande zote, kwa kuzingatia taratibu zilizopo katika Usagara, Sultan baada ya kuhojiwa moja kwa moja alikiri kwamba hakuwa na ushirika ama kutegemea kwa namna yoyote Sultan wa Zanzibar, na kwamba hakuwa hata akimfahamu.

Imesainiwa. Dk. KARL PETERS
Imesainiwa. MANGUNGO

Mkataba huu umefanyika kihalali kabisa na umehuishwa kwa nyakati zote mbele za mashahidi wengi, ambao tunakiri hapa:
Kwagakinga (dole gumba);
Golola mtoto wa Sultan Mangungo (dole gumba);
Draman mtoto wa pili wa Sultan Mangungo (dole gumba);
Graf Pfeil August Otto.
Dole gumba la mkalimani Ramazan etc.
Dk. Karl Juhlke.
Msovero Usagara Novemba 29, 1884.



KWANINI MANGUNGO ALIONEKANA MJINGA?

Historia ilipoandikwa baada ya kupata uhuru , iliwahesabu watu wote waliopambana na wazungu kama mashujaa mfano Mkwawa. Bila kujali utawala wa hao machifu kama ulikuwa wa haki au laa. Historia haikutazama watawala hawa machifu kama watu walio pambania madaraka yao bali inawahesabu kama mashujaa kwa kuwa ilipambana tu mzungu.

Baada ya uhuru watu walisoma hadithi kama "KIBANGA AMPIGA MKOLONI". waliosoma kwa kipindi hicho walimuona Kibanga kama shujaa kwa kumpiga mzungu ( mkoloni). Lakini je Kibanga wa mwaka 1960 bado ni shujaa leo hii au ataonekana anafukuza "WAWEKEZAJI" ?

Kwahiyo kama KIBANGA alionekana shujaa kwa kumpinga mkoloni kipindi cha kutaka kujitawala ni wazi historia yoyote iliyoandikwa kwa kipindi hiko ingemtazama mtu yeyote yule aliyeshirikiana na wakoloni kipindi wanaingia Afrika kama mtu mjinga na msaliti kwa jamii yake.


KWANINI NASEMA MANGUNGO SIO MJINGA?


Kilichotokea kati ya Mangungo na machifu wengine waliopigana na wazungu ni uelewa tu. Mangungo aliona mbali ambapo wengine hawakuona kwa kipindi kile. MANGUNGO aliwaona wazungu kama wawekezaji mapema sana kuliko machifu wenzake. Kile alichokifanya Mangungo kuwaona wazungu kama wawekezaji ndio hiki tunakiona leo na sisi kuwa wazungu wanauwezo wa kuwekeza katika nchi zetu za kiafrika na uchumi ukakua.

JE MANGUNGO ALIAHIDIWA NINI KWA WAZUNGU?

Binafsi naamini tofauti na mkataba wa kuichukua ardhi na kiutawala tunaoambiwa kuwa ndio huo MANGUNGO alisaini lakini inaonesha wazi kwamba Mangungo alielezwa kuwa kama wazungu watalichukua eneo basi watakuja na mamba yafuatayo ;

mashine ( matreka) za kilimo kama treka nk

Ujenzi wa hospital za kisasa kwa (kipindi hicho)

Ujenzi wa shule

Ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula

Ujenzi wa barabara

Ujenzi wa mabwawa ya kuzalisha umeme

Ujenzi wa reli ya kisasa kwa wakati huo

Ujenzi wa madaraja katika maeneo yasiyopitika kipindi cha masika

Upatikanaji wa huduma za maji safi .

Je upi unaweza kuwa uthibitisho wa hizo ahadi hadi kupelekea MANGUNGO kukubali?

Ukilitazama vizuri hilo eneo la Msovero ambalo ndio inaelezwa kuchukua eneo kubwa la KILOSA ya leo utagundua yafuatayo.

Maeneo mengi ya wilaya hiyo yana mashamba makubwa ya mkonge yaliyolimwa na mwekezaji wa Mangungo. Kuanzia Msowero ya leo , Gairo, Kimamba, Ludewa, Kilosa mjini ya leo, Chanzuru, Kivungu, Zombo , Mikumi, Kilangali , Malangali ,Ngaite, Melela Mvomero inayopakana na kilosa , ILONGA had maeneo ya dumila nk

Hayo ni maeneo machache sana yanayoonesha mwekezaji alitekeleza kweli ahadi yake ya kuinua kilimo.

Maeneo ya Kilosa mengi yalijegwa hospital. Mfano hospital ya Kilosa , Kimamba , vituo vya afya kama maeneo ya Ludewa , Mkata , na vingine ambavyo vilijegwa na wajerumani . Hivyo vitu havikuwepo kabla ya mkataba wa MANGUNGO.

Uwepo wa barabara kama ya kutoka Kilosa hadi Mikumi kupitia Zombo, barabara ya kutoka Kilosa hadi Morogoro mjini kupitia Mkata na ile kupitia Ludewa ni ushahidi tosha kuwa mwekezaji alifanya yale aliyoahidi mbele ya chifu Mangungo.

Uwepo wa njia ya reli inayopita tokea Morogoro mjini pale kichangani na kupita maeneo kama Mkata, Kimamba, Kilosa mjini ya sasa, Mkadage huko hadi Pwaga na kuingia Mpwapwa hii inaonedha jinsi gani mkataba wa chifu Mangungo na machifu wa kiluguru na wa kizingua ulizaa matunda kwa maeneo yao kiuwekezaji.

Uwepo wa shule ya KIZUNGUZI (kizu boys)

Ajira kwa vijana Uwepo wa huduma za malazi kwa wafanyakazi. Ajira ilipatikana kwa manamba japo mshahara haukuwa mkubwa lakini ukibadili thamani ya mshahara wa kipindi hicho unafanana na baadhi ya mishahara ya baadhi ya watu wanaolipwa hivi leo. Si kwamba hata hivi leo watu hawalalamiki udogo wa mishahara.

Nyumba za watumishi zilijegwa kila kwenye stesheni , kwenye kila kituo chao cha kukusanyia mikonge mfano Kimamba, ludewa , Chanzuru Msiwero , Kivungu nk. Hapa inaonesha ni jinsi gani mkataba aliosaini abwana mangungo haukuwa mbaya kama tunavyoaminishana leo hii.


Bado kama hayo hayatoshi ukipita maeneo ya Ilonga utaona jinsi wajerumani walivyopaendeleza katika kilimo na vituo vya utafiti wa kilimo walijenga ( hapa mtanikosoa kama walijenga wajerumani au waingereza).


Kwa wale watu walio bahatika kuishi Sagara ya zamani au Kilosa ya leo wanaweza kuwa mashahidi . Mji wa kilosa wa leo unaoneka ni mji uliokuwa wa kifahari enzi ya wawekezaji wa Mangungo ( ambao waliitwa wakoloni hapo awali) kabla ya kubadilishwa jina tena na kuitwa wawekezaji kama alivyowaita Mangungo na kizazi cha sasa . Kilosa ulikuwa mji kimbilio la wageni toka mikoa mbali mbali Tanzania. Usifikiri katika "engo" ya manamba kupata mchanganyiko wa kabila katika eneo la kilosa bali hata huduma ziliwavuta vijana wa zamani kwenda kuishi Kilosa.

Je kunyonywa kiuchumi ndio kunatufanya tumuone Mangungo alikuwa mjinga?


Binafsi namuona Bwana Mangungo kama kiongozi aliyeuona uwekezaji tangu mapema. Kwani kama kuhusu kunyonywa bado hadi leo kama taifa bado tuna mikataba mingi ya kinyonyaji isiyoacha alama kwa taifa kuliko ile ya msovero iliyoacha hata reli ,magofu ya nyumba na hospital.
Wapo watakaosema ujinga wa Mangungo ni kuiachia ardhi kwa wazungu kulima pamba na mikonge huku wenyeji kuishi kwa njaa. Binafsi naamini kwa nyakati hizo kulikuwa na watu wachache sana wenye uwezo wa kulima mamia ya ekari kama wawekezaji. Wengi walilima kujikimu kwani ni miaka zaidi ya 70s sasa tangu Mzungu atuachie ardhi yetu lakini kuna maeneo tangu kuumbwa kwa dunia hayajawahi kulimwa na wazawa. Vijana wanashinda kwenye vituo vya kubeti huku redio zikihamasisha nguvu ya buku katika kushinda kamali. Kwa mawazo kama hayo hatuoni kama bwana Mangungo aluoba mbali kuingia mikataba na wawekezaji?

Wapo watakaosema ujinga ni kuwa alisaini bila kuelewa chochote . Binafsi naona si kweli, kwani kama ni kweli Mangungo alisaini kitu asichoelewa historia ingeonesha kutokea mgogoro baina ya mwekezaji na Mangungo. Katika hali ya kawaida mtu akwambie muingie makubaliano ya kulichukua eneo lako lote la ardi na kiutawala na ukakubali bila kumuuliza shughuri atakazofanyia eneo lako. Pili, mkata ulisainiwa kisha Karl na wenzake wakaondoka kurudi Ujerumani . Kama wangekuwa ni walaghai basi pale waliporudi kutekeleza uwekezaji wao lazima pangetokea ugomvi na kutoelewana. Maana katika hali ya kawaida ukimpa mtu eneo alime au akae alafu ghafla unamwona anakuja na fundi wake wanajenga nyumba , hospitali, reli bila kwenda kuwahoji.

MANGUNGO ALIKUWA KIONGOZI MWANADIPLOMASIA

Kwajinsi sasa jamii ya Kiafrika inavyomsifu kiongozi mwenye mahusiano mazuri na wazungu kama kiongozi bora na mwanadiplomasia basi ni wazi Mangungo alikuwa nguli zaidi kama mwanadiplomasia wa mwanzoni kabisa.

NINI WITO WANGU KWA JAMII

Niwakati sasa wa jamii yetu kubadili mtazamo juu ya chifu Mangungo kwa kumchukulia kama kiongozi mjinga na kumwona kama kiongozi wa mwanzoni kuhamasisha uwekezaji nchini. Kumwona Mangungo kama kiongozi mjinga kumeifanya hata familia yake isijulikane leo hii ksma zinavyojulikana familia za ma chifu wengine. Kwakuwa sasa viongozi wetu wamerudi kule kule kuwapokea wazungu na kufanya nao shughuri za maendeleo kama ujenzi wa miundombinu ya maji , barabara, reli, hospitali, na shule jambo ambalo hata Mangungo ndilo alilifanya kwa ustadi basi hatuna budi kumuenzi Mangungo kama mwasisi wa uwekezaji nchini.
Natamani sasa hata familia yake iliyobaki tuiombe msamaha kama taifa kwakuwa tulilewa mvinyo wa uhuru kiasi ya kuwaona waliopinga kushirikiana na wazungu kuwa ndio MASHUJAA.

Nawasaliim
Hospitali ya BELEGA nadhani nayo iko ndani.
Km ni hivyo basi nami naunga mkono hoja.
Mangungo hakuwa akijua kusoma lkn mkataba wake ulikuwa na manufaa makubwa kwa jamii ukilinganisha na hii ya bandari,uwindaji,madini na rasilimali zingine inayosainiwa na VIONGOZI WANAOJUA KUSOMA MPAKA KICHINA LKN NI ZAIDI YA ULAGHAI.

NAMI NATOA WITO KWA SERIKALI NA JAMII KWA UJUMLA KWAMBA ZILE KUMBUKUMBU HASI ZILIZO ANDIKWA IWE NI KWENYE VITABU VYA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA SHULENI KUMHUSU SULTAN MANGUNGO ZIFUTWE NA KUANDIKWA UPYA.

SULTAN MANGUNGO alikuwa na uchungu na jamii aliyokuwa akiiongoza kuzidi hawa viongozi wa leo ambao hiyo mikataba wanayo saini ni kwa manufaa yao binafsi na siyo jamii.

Nasema hivyo kwa sababu naamini ni jambo ambalo haliwezekani familia ya Mangungo pekee kutibiwa hospitalini,kutmia barabara,kutumia reli na mengineyo.
 
Mtoa mada umechemka vibaya sana. Kwanza tambua ya kwamba hilo jina la mwekezaji sijui wawekezaji yamekuja sasahiv kwa kuzingatia mutual benefits za kibiashara lakini enzi hizo za ukoloni hakukuwa na terminology mkoloni simply unaona mpaka hapo Dkt Karl Peters alikuwa ni mkoloni persee aliyeamua kutumia njia ya kumlaghai Mangungo kwasababu aliona ni njia rahisi na ni effective zaidi.

References zinadai katika makubaliano hayo, mostly kulikuwa na kuhadaiwa kwa kiongozi wetu wa kimila yani Chief Mangungo kwani alitia wino kukubali mkataba uliokuwa na mda mrefu zaidi (historia zinasema ni zaidi ya miaka 100) ina mana bila kupata uhuru wetu mpka leo hii tungekuwa chini ya huo mkataba. Chief Mangungo hakuelewa lugha ya kingereza nashangaa ni wapi unasema alikuwa na mkalimani anaemtafria, really???? Huyo mkalimani yeye alisomea wapi hicho kingereza???

History zinadai kuwa Mangungo kusaini mkataba ule japo hakuuelewa ilikuwa ni kutokana na kuuhofia utawala wa wajerumani kwani kwa hakika kabisa kama angeamua kuugomea ni wazi angrlazimika kuingia kwenye battlefield na mjerumani kitu ambacho alitafakari akaona hakiwezi hivo ndipo akaamua kusain kama submission ya mapema kwa wakoloni. Ikumbukwe pia enzi hizo stories za kuingia kwa wakoloni maeneo tofauti tofauti ya Africa hususani tanyanyika yalikuwa yanafamika hivyo baadhi ya watawala walikuwa na taarifa za uwezo wa wakoloni kivita kama ukiamua kwenda nao against hivyo machifu wengine walianza kuingiwa na woga wa kupambana nao.

Katika kusamarize, ni kwamba chief mangungo hakusaini kwa kuridhia au hiari ni kwamba aliwahofia wajerumani. Karl Peters alikuwa ni moja ya wakoloni wa kijerumani katili sana kipindi hicho hadi kuna maeneo mengine alifamika kama "mkono wa damu" so ni wazi machief kama mangungo walimu underfier kuingia nao frontline kwenye uwanja wa mapambano. Muhimu zaidi ni kwamba usijaribu kumtetea chief wetu kwa kosa alilolifanya. Ukweli ni kwamba alifanya kosa japo ni kwa shinikizo la kuwahofia wajerumani na nguvu zao kipindi hicho. Tuwe tunajifunza kwa mistakes za wazee wetu ili tusije kurudia makosa yale ktk karne hii ambayo sisi vizazi vyao tuna uelewa na pia tuna uhuru wa kuamua kushirikiana au kutoshirikiana kwenye mikataba mbali mbali ya kimaendeleo. Sasa inashangaza sana bado karne hii tunaingia tena mikataba ya miaka sijui 100, sijui 99 dah inafikirisha sana kwakweli.
Viongozi wa sasa wenyewe wana tofauti gani na mangu ikiondoa kujua kusoma na kuandika?
 
Sikweli bali aling'aka kwenye mambo machache ya uonevu kama kodi nakutopewa madara makubwa kiutendaji. Yaani utawala . Hii inatokea hata leo hii .Unaweza kuingia makubaliano Na mtu kwenye jambo fulani lakini akaingia tamaa baada ya kupata. Lakini si kweli kwamba alisaini kitu asichokijua 100%
Ina maana watu wengi hawaja kuelewa?

Nimepita huko kiasi na nimekuelewa sana.
 
Up
Ipo hivyo hadi leo hakuna uwekezaji wenye taswira la kumnufaisha mwenye mali 100%. Sasa mtu kaja kuwekeza ili malighafi ziende ulaya unategemea reli aijenge vipi kama sio kuelekea bandarini?

Kitu kizuri pia Mangungo alikuwa muwaz kuishirikisha jamii na familia yake katika mikata ya wazi tofauti na leo viongoz wanasaini mikataba ya siri
Upewe maua yako mkuu.
 
Nachangia kutokana na ulichoeleza, sijawahi kufika maeneo yote uliyoainisha.

Kwa mtazamo wangu na ulichoandika, mjerumani alikuwa akijinufaisha yeye. Chifu Mangyngo alifaidika binafsi na familia yake? Sijui.

Ila kwa watu wengine, ndio walikuwa manamba au watumwa. Kama kulijengwa hospitali, barabara na viwanda, vyote ni kuhakikisha uzalishaji wa uhakika kumnufaisha mjerumani. Sikuona ukieleza mambo ya shule, kama zilijengwa. Ila umetaja mambo ya shule katika mambo unayohisi aliahidiwa chifu.

Tukiangalia miundombinu iliyowekwa, chifu anaweza kusifiwa, japo kiuhalisia, inaonekana miundombinu yote, ilikuwa kwa lengo la kurahisisha shughuli na maisha ya mjerumani na kujitajirisha.

Na ukiangalia mazingira ya eneo lake kulinganisha na sehemu walikowapinga wakoloni, utasema kuna maendeleo ya vitu, kutokana na miundombinu hiyo iliyokuwa ikisaidia wizi wa mjerumani.
Je, Yule aliyeuza gesi yetu yote kwa wachina yupo kundi gani?

Aliyeuza loliondo kwa waarabu wa othello sisi kama nchi tumefaidika nini?

Aliyempa bilionea Fredkin ekari 6,000,000 za ardhi kule Arusha kwa miaka 99 sisi tunafaidika nini?
 
Back
Top Bottom