Waafrika wanajiona kama wanaonewa muda wote. (Inferiority)

Waafrika wanajiona kama wanaonewa muda wote. (Inferiority)

Acehood

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,653
Reaction score
2,792
Toka juzi nafuatilia matukio yanayotokea huko Ukraine kupitia Twitter, ila kuba hili suala la waafrika kujiona kama wanaonewa hasa kupewa hifadhi na access kwenye safe zones inasikitisha sana.

Kuna clips zinasambaa mojawapo ni waafrika hasa wanaijeria wanalalamika hawaruhusiwi kuingia Poland wakitishiwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Poland Lakini ukiangalia ile video clip inaonyesha ni mchanganyiko wa races mbalimbali. Lakini sababu kubwa ambayo ina mashiko ni kwamba kuna foleni kubwa ila waafrika wengi wanapiga kelele kulalamika wakiamini hawatoruhusiwa kabla hata ya zamu zao kufika.

Nyingine nimeona kuna video clip ya mama na mtoto wake mdogo wa miezi kadhaa (African) naye analalamika kwamba amekwama sehemu na hasaidiwi kupelekwa sehemu nzuri kisa tu yeye ni african na wakati huohuo kuna races zingine wako na watoto wadogo sana eneo hilo.

Waafrika tuache kujiweka kwenye kundi moja na wenye uhitaji wa huduma maalumu kama walemavu n.k. Black race isiwe sababu ya kumwagiwa maji bahati mbaya na white race ukaona ni racial discrimination.

"I tried so hard and got so far, but in the end it doesn't even matter".
 
Futa huu uzi usibishe kitu ambacho hujafatilia vizuri anko sawa
Soma huyo muukraine mwenyewe anapinga wanachofanya askari wao..
Yaani miafrika cjui tutapata akili lini
20220227_133610.jpg
 
Yaanu watu wasilalamike kwa sababu wataonekana inferior?
Soma hiyo hapo juu sio mwaafrika aliyeandika.
Kama kuna ubaguzi kwa sababu ya race basi ni lazima ulalamikiwe.
Na kwa tuliowahi kupita Ukraine au Poland tunajua wazi kuna ubaguzi.
 
Alisikika mshamba mmoja wa Kisiju ambaye hajawahi hata kufika Misri,

Ungejua Ubaguzi kwa Waafrica usingeandika hayo.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Yaanu watu wasilalamike kwa sababu wataonekana inferior?
Soma hiyo hapi juu sio mwaafrika aliyeandika.
Kama kuna ubaguzi kwa sababu ya race basi ni lazima ulalamikiwe.
Na kwa tuliowahi kupita Ukraine au Poland tunajua wazi kuna ubaguzi.
Ubaguzi kamwe hautoisha kama kuna umasikini.
njia ya kuumaliza ni waafrika wajenge kwao na sio kukimbila kwa watu waliojenga kwao kwa shida alafu mwafrika kwa uvivu wake anakimbia kwao anaenda kula bure kwa watu.

Lazima ubaguliwe tu.
 
Mleta uzi anatoa usia kwa watu wa asili ya Afrika wasilalamike.Wafe kiume(bila kelele,kama wafuasi wa Kibwetere).Ukimya hoyeeee!
 
Wakati mwingine ni Ujanja ujanja ili wawe favoured na watengeneze attention. Kama tu mtu anapotumia uyatima kusaidiwa kwenye jamii.
Au kwa vile sina baba, au kwa vile sina mama ndo maana hamnipi kazi? Hapo anatokea mtu si mumpe tu huyo yaishee?
 
Ubaguzi hauletwi na umaskini.Ni dhana kwamba whites wanajiona wao ni superior.
Tuende na dhana kwamba waafrika wabaki kwao ili wasibaguliwe!
Wamerekani weusi wanabaguliwa kwa nini wakati wapo Marekani kwa muda mrefu na wametoa mchango mkubwa wa kuijenga Amerika?
Hii superiority complex ya whites ni dhana pana ambayo hata yule white hohehahe anajiona ana thamani kuliko weusi kwa sababu tu ya white card. Yaani kuzaliwa white.Anaamini kabisa yupo superior kuliko blacks.
Suluhisho la kila race ibaki kwao haipo realistic kwenye dunia ya sasa kwa sababu whites wanakuja Afrika tunawapokea na kuwakirimu na ndio hulka ya kibinaadamu.
Ukiona una chembe chembe za kiubaguzi basi jiangalie kwenye kioo kuna kitu hakipo sawa.
Tofauti ni layer ya ngozi tu.Sisi wote ni wanadamu.
 
Hayo makasiriko hayaondoi ukweli kuwa waafrika tunajiweka wadhaifu mbele ya reces nyingine. Na ndio maana tunahisi kuonewa like we're victims of everything.
 
Wakati mwingine ni Ujanja ujanja ili wawe favoured na watengeneze attention. Kama tu mtu anapotumia uyatima kusaidiwa kwenye jamii.
Au kwa vile sina baba, au kwa vile sina mama ndo maana hamnipi kazi? Hapo anatokea mtu si mumpe tu huyo yaishee?
Kweli kabisa mkuu
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Ubaguzi hauletwi na umaskini.Ni dhana kwamba whites wanajiona wao ni superior.
Tuende na dhana kwamba waafrika wabaki kwao ili wasibaguliwe!
Wamerekani weusi wanabaguliwa kwa nini wakati wapo Marekani kwa muda mrefu na wametoa mchango mkubwa wa kuijenga Amerika?
Hii superiority complex ya whites ni dhana pana ambayo hata yule white hohehahe anajiona ana thamani kuliko weusi kwa sababu tu ya white card. Yaani kuzaliwa white.Anaamini kabisa yupo superior kuliko blacks.
Suluhisho la kila race ibaki kwao haipo realistic kwenye dunia ya sasa kwa sababu whites wanakuja Afrika tunawapokea na kuwakirimu na ndio hulka ya kibinaadamu.
Ukiona una chembe chembe za kiubaguzi basi jiangalie kwenye kioo kuna kitu hakipo sawa.
Tofauti ni layer ya ngozi tu.Sisi wote ni wanadamu.
Ndicho nilichomaanisha mkuu ila kuna watu wanatoa comment Kwa mihemko.

Sisi waafrika tukiendelea kujiona inferior na tunaendelea kujazana ulaya hii kitu haiwezi isha
 
Kwanini na wao wakubali kubaguliwa?
Kwanini hao waafrika wasiwabague na wao.

Hii ndio shida ya umasikini.
Mbona hata sisi tunawabagua Sana wazungu sehemu za huduma wakija kutalii. Kuanzia ferry to zanzibar, viingilio mbugani, kulala hotel zetu kuna bei tofauti ya mwafrika na Mzungu. Mzungu ulipa zaidi. Hata bei ya tax airport to city center Mzungu atalipa laki moja mswahili atalipa elf 30 kwa umbali sawa yaani kilometa 10.
 
Back
Top Bottom