U
Upo sahihi. Lakini tufundisahane kuzaa watoto tunaowamudu kwa malezi. Tusifikie hatua ya kuwa na idaid kubwa ya watoto ambao tunaanza kuomba misaada ya kuwahudumia.. Mija ya sababu ya Mataifa ya Magharibi kugharimia miradi ya kupanga uzazi ni kutusaidia nchi kuwamudu wananchi wake kihuduma. Tunatembeza bakuli na wakitushauri nini cha kufanya ili tuweze kujitegemea tunaleta hoja kama hizi. Mtu inazaa watoto kumi na mbili wakipishana miaka miwili halafu unashindwa kuwapeleka shule, kuwalisha, kuwavisha na wanarudi kuwa wakora mitaani. Iko haja ya kuwaelimisha watu wetu kuwa ni haki yao kuzaa lakini idadi ya watoto watakoweza kuwahudumia - si kuwaambia wafyatue watoto tu ili mradi unaweza kuwalisha. Dunia ya leo huduma kwa mtoto si kumlisha tu, inataka apate elimu - tena elimu iliyo bora ni si bora elimu, anhitaji atibiwe matibabu bora anapougua, na malezi ya kimaadili kwa ukaribu kutoka kwa wazazi. Kuna familia baba ana watoto wengi kiasi cha wengine hawajui hata majina - mtu kama huyu atawapa saa ngapi malezi ya maadili watoto ambao hawajui hata majina sawa na madarasa yet kwenye shule zetu za bure Mwalimu anawatoto wengi kiasi cha kutowajua mmoj mmoja suala ambalo ni muhimu sana katika malezi.
Kama hatuatki kusaidiwa basi tuwe na mpango wetu wenyewe kama waafrika wa jinsi ya kudhibit kuzaliana - au kwa ufupi kuzaa watoto wasiokusudiwa. Familia zetu nyingi zinazaa watoto wa bahati mbaya - wazazi hawakukaa wakakubaliana kuwa sasa tuzae mto wa kumi na moja, weigni wanatokea kwa bahati mbaya.