Waagiza mafuta wasema bila Dola watashindwa kuagiza mafuta

Waagiza mafuta wasema bila Dola watashindwa kuagiza mafuta

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2022
Posts
270
Reaction score
362
Katika kuendelea kuhakikisha bidhaa ya mafuta ya petroli inapatikana kwa uhakika maeneo yote nchini, Chama cha Waagizaji na Wasambazaji Mafuta Tanzania (TAOMAC) wamekutana na Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam tarehe 4 Agosti 2023.

Katika kikao hicho, TAOMAC walitoa taarifa ya mwenendo wa biashara ya mafuta duniani na hapa nchini pamoja na kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya mafuta hususani suala la upatikanaji wa dola za Marekani.

Chama hicho kilifafanua kuwa uhaba wa dola za marekani katika soko la fedha kunapelekea waagizaji kupunguza kiasi cha mafuta wanachoagiza kuepuka kuagiza mzigo na kushindwa kuulipia kwa wakati jambo ambalo linaongeza gharama za uendeshaji wa biashara na kuathiri bei ya mafuta kwa mteja wa mwisho.

Akizungumza katika kikao hicho, Makamu Mwenyekiti wa TAOMAC Ndg. Salim Baabde alisema “biashara yetu inafanyika kwa kutumia Dola za Marekani na inapotokea dola inakuwa adimu sokoni inaathiri moja kwa moja bei ya uagizaji ambayo mwisho wa siku inaathiri bei ya mafuta kwa mtumiaji wa mwisho”.

Aidha walieleza kuwa hali inaweza kuzidi kuwa mbaya iwapo changamoto ya upatikanaji wa dola haitatuliwa kwa haraka, “Tunaiomba Serikali kuongeza nguvu katika kuhakikisha dola zinapatikana kwa kushirikisha benki za biashara ili kuepuka changamoto hii kukuwa zaidi na kuleta athari kubwa” aliongeza Ndugu Baabde.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAOMAC, Ndg. Raphael Mgaya alimhakikishia Mhe. Waziri kuwa pamoja na changamoto hiyo, TAOMAC wataendelea kuagiza mafuta ingawa kwa gharama kubwa ili kuhakikisha nchi inaendelea kupata nishati hiyo muhimu katika hali ya uhakika na endelevu. “Tutaendelea kuhakikisha tunalinda dhamana tuliyopewa na Serikali ya kuhakikisha nchi inakuwa na mafuta wakati wote hata kama ni kwa gharama kubwa” alifafanua Ndg. Mgaya.

Vile vile wamemshukuru Waziri na EWURA kwa ushirikiano ambao wamekuwa wanautoa kwa tasnia hasa katika vipindi vigumu na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali pamoja na kuelimisha umma kuhusu biashara ya mafuta ili kukabiliana na upotoshaji mkubwa hasa mitandaoni kuhusu biashara hii.

Kwa upande wake Waziri Makamba amewashukuru kwa ushirikiano waliutoa kuhakikisha kwamba nchi inapata mafuta muda wote. Waziri Makamba pia alieleza kwamba mlango wake uko wazi wakati wote kwa ajili ya mashauriano. “Sisi hapa Wizarani filosofia yetu ni ile ya open door ambapo yeyote anakaribishwa kwa ajili ya mashauriano na majadiliano”.

Aidha, Waziri Makamba alisisitiza kuwa Serikali inaelewa changamoto ambazo sekta inakabiliana nazo kwa sasa na kuwa hatua madhubuti zimeendelea kuchukuliwa. Aidha Mhe. Makamba alisisitiza umuhimu wa wadau ikiwemo TAOMAC kuendelea kushikamana na kushirikiana ili kuhakikisha upatikanaji wa mafuta kwa uhakika kwa ajili ya ustawi wa nchi na watu wake.

hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Kamishna wa Petroli na Mafuta Ndg. Michael Mjinja, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dr. James Andilile na wataalamu kutoka Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja
 
Katika kuendelea kuhakikisha bidhaa ya mafuta ya petroli inapatikana kwa uhakika maeneo yote nchini, Chama cha Waagizaji na Wasambazaji Mafuta Tanzania (TAOMAC) wamekutana na Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam tarehe 4 Agosti 2023.

Katika kikao hicho, TAOMAC walitoa taarifa ya mwenendo wa biashara ya mafuta duniani na hapa nchini pamoja na kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya mafuta hususani suala la upatikanaji wa dola za Marekani. Chama hicho kilifafanua kuwa uhaba wa dola za marekani katika soko la fedha kunapelekea waagizaji kupunguza kiasi cha mafuta wanachoagiza kuepuka kuagiza mzigo na kushindwa kuulipia kwa wakati jambo ambalo linaongeza gharama za uendeshaji wa biashara na kuathiri bei ya mafuta kwa mteja wa mwisho.

Akizungumza katika kikao hicho, Makamu Mwenyekiti wa TAOMAC Ndg. Salim Baabde alisema “biashara yetu inafanyika kwa kutumia Dola za Marekani na inapotokea dola inakuwa adimu sokoni inaathiri moja kwa moja bei ya uagizaji ambayo mwisho wa siku inaathiri bei ya mafuta kwa mtumiaji wa mwisho”. Aidha walieleza kuwa hali inaweza kuzidi kuwa mbaya iwapo changamoto ya upatikanaji wa dola haitatuliwa kwa haraka, “Tunaiomba Serikali kuongeza nguvu katika kuhakikisha dola zinapatikana kwa kushirikisha benki za biashara ili kuepuka changamoto hii kukuwa zaidi na kuleta athari kubwa” aliongeza Ndugu Baabde.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAOMAC, Ndg. Raphael Mgaya alimhakikishia Mhe. Waziri kuwa pamoja na changamoto hiyo, TAOMAC wataendelea kuagiza mafuta ingawa kwa gharama kubwa ili kuhakikisha nchi inaendelea kupata nishati hiyo muhimu katika hali ya uhakika na endelevu. “Tutaendelea kuhakikisha tunalinda dhamana tuliyopewa na Serikali ya kuhakikisha nchi inakuwa na mafuta wakati wote hata kama ni kwa gharama kubwa” alifafanua Ndg. Mgaya.

Vile vile wamemshukuru Waziri na EWURA kwa ushirikiano ambao wamekuwa wanautoa kwa tasnia hasa katika vipindi vigumu na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali pamoja na kuelimisha umma kuhusu biashara ya mafuta ili kukabiliana na upotoshaji mkubwa hasa mitandaoni kuhusu biashara hii.

Kwa upande wake Waziri Makamba amewashukuru kwa ushirikiano waliutoa kuhakikisha kwamba nchi inapata mafuta muda wote. Waziri Makamba pia alieleza kwamba mlango wake uko wazi wakati wote kwa ajili ya mashauriano. “Sisi hapa Wizarani filosofia yetu ni ile ya open door ambapo yeyote anakaribishwa kwa ajili ya mashauriano na majadiliano”. Aidha, Waziri Makamba alisisitiza kuwa Serikali inaelewa changamoto ambazo sekta inakabiliana nazo kwa sasa na kuwa hatua madhubuti zimeendelea kuchukuliwa. Aidha Mhe. Makamba alisisitiza umuhimu wa wadau ikiwemo TAOMAC kuendelea kushikamana na kushirikiana ili kuhakikisha upatikanaji wa mafuta kwa uhakika kwa ajili ya ustawi wa nchi na watu wake.

hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Kamishna wa Petroli na Mafuta Ndg. Michael Mjinja, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dr. James Andilile na wataalamu kutoka Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja
Wenyewe wenye Dollar zao wanashida na dollar sasa hivi.

Tanzania tu wajinga, tuna dhahabu ya kutosha, tutakosaje mafuta?
 
Uhaba wa dollar ulipotokea Kenya wenyewe wajigamba et wanauchumi imara, aya sasa kiko wapi
 
Kuna wakati nimekuwa nikiwaza, yawezekana tunaviongozi wazuri ila ni waongo?

Au yawezekana viongozi wetu siyo waongo ila ni watu dhaifu na wasiojiamini na wapenda rushwa?

Hivi majuzi, kuruu nzima ya uongozi wizara ya nishati walituhakikishia kuwa, nishati ya mafuta nchini ni nyingi na kuna akiba inayoweza kukidhi mahitaji ndani ya miezi kadhaa, maelezo hayo, yalikuja baada ya nishati hiyo kuadimika kule maeneo ya Ifakara Morogoro,

Haijachukua hata wiki moja, tayari wanatuletea lugha nyingine

Unajiuliza, ni mpaka lini mnyonge atakuwa mfanikishaji wa misheni za viongozi?
 
Tunahangaika na nishati wakati tuna matrillioni ya tani ya gas deposit, tuna makaa ya mawe, tuna hydroelectric power potential kubwa, ngozi nyeusi sijui tulirogwa na nani.
 
Potelea mbali, tuanze kusindika CNG kwa ajili ya kutumika kwenye magari
 
Hawa watu sijui wanatuona mataahira? Wanapiga hela kwa kisingizio cha dollar na sasa wanataka kuhalalisha upigaji, wakae kimya
 
Tunahangaika na nishati wakati tuna matrillioni ya tani ya gas deposit, tuna makaa ya mawe, tuna hydroelectric power potential kubwa, ngozi nyeusi sijui tulirogwa na nani.
10% ndio zinatufikisha huku, nasijui huwa wanafurahia shida zetu duh hii ngozi inatatizo kiukweli
 
Nchi wahuni wengi, wakisikia bei ya mafuta inapanda basi siku hiyo wiki nzima mafuta yanapatikana kwa tabu.Ewura wa kitangaza bei mpya saa sita siku ya siku inayo fuata mafuta ya naanza kupatika kwa wingi sana.

Bi mkubwa anacheka na ndezi,waziri nae mmmmhhhhhh.......... anabebwa na jina la mzee wake, yaaani tabu tubu. Tujiandae na mfumuko mwengine wa chakula,kwani wafanyabiashara wa chakula lazima hili biti la uhaba wa dola na ongezeko la mafuta lazima wapite nalo,japo kipindi hiki chakula kipo kingi.
 
Wenyewe wenye Dollar zao wanashida na dollar sasa hivi.

Tanzania tu wajinga, tuna dhahabu ya kutosha, tutakosaje mafuta?
Sentence fupi lakini Ndefu sanaaa!!
Siri iko hapo!!
Waziri wa Nishati jumlisha Waziri wa Madini Jumlisha waziri wa Fedha Jumlisha Waziri wa Mipango Jumlisha Governor ni sawa na Maisha RAHISI!!

Sisi wafanyabiashara iyo ni sekunde tu.. !
 
Back
Top Bottom