Waalimu tunadharauliwa sana hivi kwanini?

Maji makubwa🤣🤣 poleni Sana, walimu wengi hawana intrinsic
motivation wanafanya kazi ili mradi tu. Ndo maana kila mwalimu anaejiendeleza kielimu anataka aachane na ualimu. Maboss pia huwa grade walimu Kama wanafunzi 🤣🤣
 
Maji makubwa🤣🤣 poleni Sana, walimu wengi hawana intrinsic
motivation wanafanya kazi ili mradi tu. Ndo maana kila mwalimu anaejiendeleza kielimu anataka aachane na ualimu. Maboss pia huwa grade walimu Kama wanafunzi 🤣🤣
hilo ni kweli kaka wanatuona kama mbuzi
 
Tunaua Elimu yetu Kwa kutikuwajali walimu.

Uchaguzi u karibu, onyesheni hasira zenu huko, pia walimu mna HAKI kisheria kugoma kupitia chama chenu Cha wafanyakazi, tumieni njia huyo kukata minyororo iliyowafunga.
Huwa wanatishwa sana kama watoto.Maafisa Elimu na HROs wakiongoza kwa kuwasumbua,kuwanyanyasa,kuwadhulumu na kuwatisha.
 
Kwani serikali si imeweka viwango vya posho public. Mnalia nini?
Kama semina ni siku 5 jumlisha na siku 1 (1/2 +1/2) jumla siku SITA.
Hapo tena unalipwa kulingana na daraja lako .
Sasa munalia nini huku kila kitu kiko wazi?
Kama viwango vya posho viko wazi na anatokea Mtanzania mwenzako (sio mzungu, sio shetani, sio Mungu) anakudhulumu na wewe unakodoa macho maana yake huna akili.
Tahira
 
sh ngapi mkuu tuanzie hapo?
 
sh ngapi mkuu tuanzie hapo?
Kwa junior 100k per day while 250k per day.
Taasisi zingine junior 150k , zingine junior 200k.
Sasa ukilipwa nusu kataa na andika barua kwa katibu mkuu Utumishi wa umma nakala kwa Mkurugenzi wako , nakala CWT, nakala Tamisemi. Halafu kabla hujapost kwa EMS na kwa mtandao mwambie mapema unayemshitaki.
Mavi yatamtoka atakupa pesa yako yote .
 
Tatizo ni walimu wenyewe, wengi wenu hamjitambui unakuta mwalimu ana maisha magumu madeni kibao ila akiskia Bashite yuko hapo wilayani mbio kwenda kujaza uwanja sasa namna hiyo mtaachaje kudharauliwa??
 
Mtalipwa uchaguzi mkuu ukikaribia ili msahau taabu zenu.

Ni vizuri wawabane zaidi ili akili zitoke tumboni na kurejea kichwani.
 
Mpo cheap mno
 
Hongera sana boss kiukweli walimu wengi wamekuwa walimu kwa sababu ya umaskini tu.

Bahati mbaya sana ukiingia huko kutoka nako ni kugumu sana ( comfort zone).

KAMWE UALIMU SIO KAZI YA KUFANYA. NI KAZI YA MASKINI NA WASIO JIWEZA KIUCHUMI. HAWA WATU HAWAWEZI KUIBADILISHA NCHI KAMA WAO WENYEWE WAMESHINDWA KUBADILI MAISHA YAO.
 
Ndio maana mapinduzi ya Elimu kwa kutumia walimu hawa ni ndoto ya Alinacha.

Walimu hufanya kazi ilimradi wapate ugali wao tu intrinsic motivation itatokea wapi kwa mshahara wa 400K month to month.
 
Ndio maana mapinduzi ya Elimu kwa kutumia walimu hawa ni ndoto ya Alinacha.

Walimu hufanya kazi ilimradi wapate ugali wao tu intrinsic motivation itatokea wapi kwa mshahara wa 400K month to month.
Kuna watu na degree zao hawana huo mshahara nyie mnaudharau
 
Kuna watu na degree zao hawana huo mshahara nyie mnaudharau
Hata walimu wasio na ajira wanautamani huo mshahara ILA wakiingia huko ni majuto yasio na mwisho.

Sikiliza utautamani huo mshahara kwa sababu ya umaskini na njaa tu ila kiukweli ni pesa ndogo mno.
 
Mm ni mwalimu ila sifundishi namimi nitakuwa kwenye kundi la masikini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…