Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata kwa kuangalia kwa macho tu unaona ni sawa au huwa huangalii mpira?Kwa mujibu wa msemaji wa Azam FC, ZakaZakazi, ukubwa wa dimba (pitch) la Azam Complex ni sawa kabisa na ule wa Benjamin Mkapa.
Aliyaongea hayo alipokua anatoa ufafanuzi na kushangazwa na uamuzi wa CAF kuwazuia NAMUNGO kutumia uwanja wa Azam katika mechi za makundi za kombe la shirikisho barani Afrika.
Hilo ulilosema lipo wazi uwanja uliotumika haufai hata kwa mechi za nusu fainaliKwanza nawapongeza kamati mahususi kwa ajili ya Uandaaji wa Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Federation Cup. Hakika kila mwaka kuna maendeleo kadri ambavyo linazidi kusonga mbele. Hakika mnazidi kufanya soka la Tanzania lizidi kupiga hatua mkishirikiana na TFF.
Lakini pamoja na jitihada nyingi, kuna kasoro ambazo lazima mzitatue ili kufanya mashindano yenyewe yalete hisia na msisimko wa aina yake.
Moja, ni uchaguzi wa uwanja maalum kwa ajili ya kupigia mchezo wa fainali. Logic yenu ya kuchagua viwanja katika mikoa ambayo hazina timu Ligi Kuu ili kuleta chachu ya maendeleo ya soka katika mikoa husika ni nzuri sana.
Lakini, lazima tukubaliane na ukweli kuwa mechi ya fainali inakutanisha timu bora katika mashindano hayo. Na kwa kuwa ni mechi ya kuhitimisha mashindano husika, lazima tuzingatie ubora wa pitch, ukubwa wa pitch na uwezo wa kubeba mashabiki.
Kwa siku ya leo, mechi ilikuwa ya hovyo na isiyovutia kabisa. Kwa mtu ambaye huenda labda haijui Simba na Yanga, kufungulia chaneli angelijua ni mechi ya timu za mtaani tu.
Hakuna mipira ya kueleweka. Ni butua butua tu. Uwanja umebana sana. Mipango ya mwalimu inafeli na matumizi ya nguvu yanazidi katika kupigania mpira. Mchezo unakosa ladha
Mpaka inawapa wachezaji shida kupimia kiwango cha force cha kupiga mipira. Mara nyingi mchezaji anapiga mpira akidhani itafika mahali fulani, lakini inazidi kiwango. Kama ulimuangalia Chama, kona mbili zote zinafika karibu na kona ya upande mwingine.
Mechi ya fainali ichezwe katika viwanja vikubwa na vyenye uwezo wa kubeba idadi ya mashabiki wengi. Watazamaji 20k kwa mechi ya watani wa jadi ni ndogo sana.
Boresheni mashindano na hakika yataizidi kuvutia.
Mwisho, naipongeza sana timu ya Mabingwa Simba SC kwa kutwaa tena kombe hili. Hakika tunastahili tena na tena.
Kwahio chie watu wa lindi na ntwara chio watanzaniaKwa kuongezea, wangetenga viwanja kwa kanda na kisha wao wakaiboresha pitch kwa kushirikiana na TFF.
Mfano wachague Dar, Dodoma,Mbeya, Tabora, Arusha na Mwanza.
Zinatisha sana hizo sehemu ku host fainali msimo mmoja hadi mwingine.
Njia sahihi ni kupima mkuu, sio kuangalia. Kama wao waliopima wanasema vipo sawa, anayeangalia kwa macho hapaswi kuwapinga.Hata kwa kuangalia kwa macho tu unaona ni sawa au huwa huangalii mpira?
Hata kwa kuangalia kwa macho tu unaona ni sawa au huwa huangalii mpira?