Waandaji wa ASFC: Uchaguzi wa Uwanja wa kucheza uwe kwa kuzingatia Ubora na Ukubwa

Mpira wa jana kutokana na ukubwa wa Simba umeangaliwa na Mataifa mbalimbali lakini ubovu wa uwanja mpira uligeuka butuabutua, undava na kukamiana hata kadha ya mpira haikuwepo, next time TFF mechi km hizi zipigwe Taifa tu
 
Mimi naunga mkono juhudi za TFF kupeleka mechi hizi kwenye Mikoa ambayo haina timu za ligi kuu. Lengo ni zuri sana na kiuhalisia limesaidia sana kuleta hamasa ya michezo na mapato kwa wafanyabiashara wa mikoa husika.

Kuhusu pitch ya kuchezea tumeona jinsi uwanja ulivyoenda kupandwa nyasi hivi karibuni na kufanikiwa kuwa vile. Kwakuwa Serekali tayari imehaidi kuleta nyasi bandia na kuboresha viwanja hii hoja inaweza kuwa solved iwapo watakarabati na kuongeza majukwaa ili kuweza kuruhusu kuingia watu wengi.

Kwa ile mechi ya Kigoma ingekuwa wanacheza fainali Biashara na Azam wala tusingeona haya mapungufu ya uwepo wa majukwaa kwa kuwa idadi ya watu uwanjani ingekuwa ndogo. Hivyo point ya mtoa mada inamashiko iwapo timu za Simba na Yanga ndio zitafika fainali.
 
TFF wanaingiza siasa kwenye hii michuano, wajifunze nchi kama UK fainali inachezwa wembley lakini sisi tunapeleka fainali kwenye viwanja vibovu ambavyo haviwezi kubeba watazamaji wa kutosha.
 
Hata kwa kuangalia kwa macho tu unaona ni sawa au huwa huangalii mpira?
 
Hivi viwanja vya CCM kama wamevisahau chama hakikosi ela ya kuviboresha hata kimoja kimoja ili kuendana na nyakati zilizopo kuna vingine kama mbeya pale ule sio uwanja
 
Hilo ulilosema lipo wazi uwanja uliotumika haufai hata kwa mechi za nusu fainali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuongezea, wangetenga viwanja kwa kanda na kisha wao wakaiboresha pitch kwa kushirikiana na TFF.

Mfano wachague Dar, Dodoma,Mbeya, Tabora, Arusha na Mwanza.

Zinatisha sana hizo sehemu ku host fainali msimo mmoja hadi mwingine.
Kwahio chie watu wa lindi na ntwara chio watanzania
 
Bashungwa Nadhani Ajitafakari Haraka Sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…