Waandishi wa Azam fanyeni utafiti kabla kuongea kitu

Waandishi wa Azam fanyeni utafiti kabla kuongea kitu

fimboyaukwaju

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2020
Posts
6,699
Reaction score
9,323
Jana nilikuwa namuangalia Patric Nyembela, mtangazaji wa azam akimuhoji Ahmed Ally, kwenye night gala ya Chan. Kwenye mahojiano hayo, alifanya rejea kwamba kuna mtu mmoja huko Iraq alikuwa na kauli ya vituko sana, na akamtaja mtu huyo kuwa ni Chemical Ally, sio sahihi.

Chemical Ally alikuwa ni muuaji mkubwa na alikuwa anaua kwa silaha za kemikali, ndio akapewa jina hilo, mtu aliyekuwa na kauli za vituko, comical sahaf ambae ndiye aliyekuwa waziri wa habari wa iraq. Nawashauri watangazani wa azam fanyeni utafiti kabla hamjaongea kitu
 
Naunga mkono hoja. Na hili limekuwa
Jana nilikuwa namuangalia patric nyembela,mtangazaji wa azam akimuhoji ahmed ally,kwenye night gala ya chan.Kwenye mahojiano hayo,alifanya rejea kwamba kuna mtu mmoja huko Iraq alikuwa na kauli ya vituko sana,na akamtaja mtu huyo kuwa ni chemical ally,sio sahihi.Chemical Ally alikuwa ni muuaji mkubwa na alikuwa anaua kwa silaha za kemikali,ndio akapewa jina hilo,mtu aliyekuwa na kauli za vituko,comical sahaf ambae ndiye aliyekuwa waziri wa habari wa iraq.Nawashauri watangazani wa azam fanyeni utafiti kabla hamjaongea kitu
Naunga mkono hoja. Na hili limekuwa tatizo kubwa Kwa waandishi na watangazaji. Ni kweli Alli Hassan Al-Majid (Chemical Alli) ni tofauti na Mohamed Saeed Al-Sahhaf (Comical Alli). Tofauti yao iko hapo wanapochanganya "Chemical na Comical). Comical Alli (Alli mchekeshaji) jina hilo la utani alipewa na vyombo vya magharibi wakiwa wametohowa Alli toka kwenye Al-Sahhaf lakini hawakumuita Comical Sahhaf.
 
Back
Top Bottom