Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa

Kwanini Rais Mstaafu Mkapa alikuwa hawakubali nyie waandishi wa Habari wa Tanzania,
Utusaidie na hilo Pasco
Kwa kuwa na mimi ni mwandishi, naomba nitoe mchango wangu katika hili, pasco anaweza kuja kujibu pia kwa maana limeelekezwa kwake.
Jambo kubwa lililomfanya Mkapa awadharau waandishi wakati ule ni kushindwa kukutana na mwandishi ambaye alimuuliza maswali magumu ambayo yangemlazimisha atoe majibu na masuala nyeti. Kusema kweli, waandishi wengi, huwa hawajiandia vya kutosha wakati wanapokwenda kufanya mahojiano na mtu, matokeo yake, huuliza maswali mepesi, ambayo ni rahisi kuyafikiria. Mkapa aliwalinganisha waandishi hao na akina Tim Sebastiani ambao walikuwa wakifanya utafiti wa masuala nyeti kabla hawajakutana naye kiasi cha kumuuliza maswali ambayo yalimuudhi kweli kweli Mkapa.
 
Mkuu SMU, kila nchi dunia nzima zinakata bahasha kwa waandishi kutegemeana na mahitaji na malengo ya hizo bahasha. Nitakafika topic ya bahasha zipi ni rushwa na zipi sio rushwa ndipo mtakapogundua kumbe mpaka Ikulu wanakata bahasha!.

Hilo la ID linasumbua, mimi ni Pasco wa jf ila Pascal Mayalla nae mwenywe yumo humu jf, haijalishi tunafanana vipi, kwa sheria zetu jf mimi nabaki Pasco wa jf na ndio nilochoomba uhuru huo uheshimiwe bila name calling kama zilizo makala za Mzee na Lula ni watu wawili tofauti.
 
Reactions: SMU
Nimezunguka Afrika Mashariki na nikuhakikishie kuwa suala hili la bahasha si kwa waandishi wa Tanzania tu. Nimelikuta Kenya na Uganda pia (bahati mbaya sijafanikiwa kufika Rwanda).
Tena, wakati kuna mazingira hapa Tanzania bahasha hufanywa kama suala la siri, huko kwa wenzetu hali ni mbaya zaidi kwani kuna waandishi ambao wamefikia hatua ya kuona bahasha kuwa ni haki yao
 
mkuu ni the same person, ila pasco wa JF anataka sheria za JF zifuatwe, hapa kuna pasco wa JF, nje ya hapo ni Pascal Mayalla,
ina maana kwenye mijadala ya hapa JF mchukulie km Pasco wa JF.
Mkuu Zumbemkuu, kumtaja memba wa jf na kumfananisha na member mwingine ni name calling na adhabu yake ni ban!.
 
mkuu ni the same person, ila pasco wa JF anataka sheria za JF zifuatwe, hapa kuna pasco wa JF, nje ya hapo ni Pascal Mayalla,
ina maana kwenye mijadala ya hapa JF mchukulie km Pasco wa JF.
Strange! Kwa record za JF, wote hao wawili ni members wa JF!

Kama na yeye anakubali kuwa ni mtu mmoja then its very absurd kutegemea watu wam treat kitofauti. Sheria/kanuni hiyo ya JF inakuwa na maana zaidi kwa member ambaye hajajifunua. Ni sawa na Dr Slaa, Zitto etc wa JF wategemee members humu wasiwahusishe na uhalisia wao huko nje ya JF.
 
Kusema ukweli ni rushwa. Mi natumika pahala fulani na tunadili na jamii iliyonyuma kimaendeleo na kusaidia mambo fulani huko maeneo ya vijijini. Tulishawahi kuwa tunapata ugeni mkubwa sana kutôka huko kwa wazungu na wakati mwingine hata waziri mkuu au mabalozi wa nchi kadhaa na hata wa mashirika makubwa. Mwanzo hatukuwa tunafahamu kuwa kuchukua habari ni kazi yao na hawahitaji bahasha japo msosi na maji ni vya kumwaga. Huko nitumikako hakuna njia ya kuchakachua hela kwa ajili hizo hata. Walikuja mara ya kwanza na wakafanya kazi but jioni kama kawa, bahasha. Haikupatikana na habari hazikutoka. Tukumbuke wafadhiri wengi ni mabishoronga, wanafuatilia kama waliandikwa au la. Nafikiri ni moja ya kutangaza nchi zao. Iliwabidi ubalozi fulani kutuma hizo mlungula tuwape ili habari zitoke. Mara nyingine ikawa the same. Hadi sasa shirika ilibidi litafute njia ya kubudget kila likiwa na ugeni kama ule ili washkaji walipwe. Je kama wanakofanyia kazi wanalipwa na huku wanataka za nini kama si mlungula?
Na ndiyo style za walio wachache siku hizi kuwafuata wenye maskandal na kuwachimba mkwara wa kuwaandika endapo wasingetoa chochote. Imemkuta ndugu yangu mara nyingi sana hiyo, japo jamaa hanaga scandal na huwa hawajali. Wanatunga zao wanaandika jamaa wala hashtuki. Bahasha ni rushwa kama zingine, kwa tafsiri yangu.
 

Pasco, najua unawatetea vijana wako lakini habari ile hawakuiandika kwa kuwa sikutoa bahasha!!! Kwa nini majira waliiandika tena front page kama haikuwa na uzito? Inabidi tufike mahali tuikatae tabia hii. Au ndio msemo kwamba mbuzi ula kwa urefu wa kamba yake? Waandishi hawana pa kukwapua hivyo bahasha ni muhimu!!!!!. Next time wala sitakwenda hapo maelezo, nitawaita vijana wachache kwenye kijiwe niwakabidhi bahasha na kuwaeleza niliyo nayo. Najua wataandika kuliko kwenda maelezo halafu wanakuja waandishi karibu 60 na bado unalazimika kuwapa bahasha wote hao.

Tunajifunza kutokana na makosa.

Tiba
 
Mkuu SMU, kila nchi dunia nzima zinakata bahasha kwa waandishi kutegemeana na mahitaji na malengo ya hizo bahasha. Nitakafika topic ya bahasha zipi ni rushwa na zipi sio rushwa ndipo mtakapogundua kumbe mpaka Ikulu wanakata bahasha!..
Kama hiyo ndio best practice katika taaluma hiyo basi itakuwa ni kuwaonea tu waandishi wa Tz kuwategemea wafanye vinginevyo.


Nakuelewa mkuu ila nilichotaka kusema ni wewe mwenyewe usifanye vitu vinavyowaletea watu ugumu wa kutofautisha the two.
Halafu "Pascal Mayalla" yeye kakaa kimya tu huku akimwachia "Pasco" aokoe jahazi..Lolz! Kama suala hili ni muhimu sana unaweza kufikiria kubadili ID kimyakimya pia.
 
Kwako Pasco wa JF! Nini maana ya waandishi uchwara? hili neno nimeshalisikia sana.

Pasco inaelekea ni muandishi uchwara bila ya kupewa bahasha habari hazitoki. Pasco hata ujitetea vipi wewe ni mla rushwa uliyekubuhu kwa vibahasha vya mafisadi, kila ukiona mada ya Lowassa hapa unaitetea kwa nguvu zako zote kumbe unapokea vibahasha kutoka kwa huyo muhujumu nchi na wewe pia unaihujumu na kuidhalilisha kazi ya uwana habari.
 
Mkuu Papa, inaonekana kana kwamba una wasi wasi kuwa suala la bahasha limetawala sana kwenye utendaji wa vyombo vya habari. hali haiko hivyo. Ni kweli kuwa 'msihko' unatolewa sana lakini haujatawala utendaji. Bado tupo ambao tunafanya kazi kwa kuzingatia maadili kwa kiasi kikubwa. Kilichopo ni kuwa kuna mazingira ambayo waandishi wenye njaa hutumia nafasi zao kujipatia vipato vya ziada. Na katika mazingira mengine, 'sources' wa habari huendekeza bahasha kwa sababu wanaamini kwua kwa kutumia bahasha wanajihakikishia habari zao kutumika kwenye vyombo vya habari.
Lakini pia niseme kuwa suala la bahasha si tu katika vyombo vya habari. Hivi sasa limegeuka kuwa suala la kimfumo zaidi kwa sababu kwenye fani nyingi sana suala hili limeingia ingawa sehemu nyingine bahasha hutolewa kwa namna nyingine na kwa siri kubwa
 
Nyangomboli, kwa ushauri tu ni vema ukafahamiana na wahariri wa hao waandishi ambao mnawatumia. Ni kweli waandishi wanaweza kuwa wanajenga tabia hiyo ya kutoandika habari kama hawapewi mshiko, lakini kama ukiwa unafahamiana na mhariri (si lazima mfahamiane physically-hata kwa kutafuta namba yake ya simu na kuzungumza naye) unaweza ukatatua sehemu ya tatizo lako. Ninavyofahamu wahariri wengi huwa hawaendekezi sana masuala hayo ya bahasha (ingawa wapo wanaohusudu). Mimi mwenyewe nawasauidia watu wengi tu wanaopatwa na matatizo kama hayo kwa waandishi
 
Kwako Pasco wa JF! Nini maana ya waandishi uchwara? hili neno nimeshalisikia sana.
Mkuu Ndallo, waandishi uchwala ni wale wanaojifanya waandishi lakini sii waandishi chochote si lolote na wapo wa aina mbili. Aina ya kwanza ni wale waliovamia fani baadaye wakajikuta hawawezi bali wanang'ang'ania uandishi huku wanachoandika hakina mashiko. Waandishi uchwala wa pili ni wale ambao walikuwa waandishi wakajikuta hawana kazi hivyo kuvizia matukio mbalimbali kuwinda bahasha for survival, hawa ndio huitwa makanjanja!.
 
Mkuu Peter Nyanje, asante kunisaidia kuelimisha kuhusu hii mada. Gazeti lako ndilo linaloheshimika number 1 Tanzania kwa sasa. Ukiona popote panapungua nisaidie kujazia.
 

Halafu mwandishi bila aibu ana justify kupokea bahasha! Ndo maana kila kukicha anajitangaza wazi ni msemaji mkuu wa Rais ajaye! Njaa hizi zitaua watu. We have stopped being creative,halafu tunataka kuishi maisha ya juu, na hela hatuna. Kwanini tusinunuliwe na kuwekwa mfukoni. Worse of all we naively believe we have the power to turn the direction of events in Tanzania at our hands! What a good day dreaming! Kweli kuna makanjanja...
 
3. Jee kuna uhalali wa waandishi kupokea bahasha hizo au kuzidai?.

Jibu ni ndio, kwa zile bahasha ambazo ni halali. Naomba nitaileta justification baada ya kusema bahasha zipi ni halali na baasha zipi ni rushwa!. Sasa zile bahasha za halali za kupokea hizi ni halali tena hata kudaiwa. Na kwa zile bahasha ambazo ni favour, takrima, bakhshish na asante hizi haziombwi wala hazidaiwi, huletwa tuu na wahusika pia naunga mkono bahasha hizi zipokelewe!.

Bahasha mbaya ni zile za rushwa na hizi ndio hata mimi nazipinga!.
 
naomba kujua huu utaratibu ni wa kimataifa au ni wa waandishi wa TZ pekee yake?
 
4. Jee ni bahasha zipi sio rushwa?.
Nilianza uandishi zamamani enzi za redio ni moja tuu, RTD na magazeti mawili tuu ya Daily News na Uhuru. Wakati huo mimi nilikuwa RTD. Ofisi ilikuwa na magari hivyo tunapelekwa kusubiriwa na kurudishwa. Ukiwa na tukio lako, unaleta gari yako ina pick waandishi na kuwarudisha. Enzi hizo hakuna bahasha!. Ukiwa na safari nje ya mkoa unaleta barua kuwa utangarimia waandishi, hivyo unawalipia usafiri chakula na malazi na kuwarudisha bila bila!.

Vyombo vya habari vilipofumka na kuwa vingi, sasa ikawa sii rahisi kuwapelekea usafiri vyombo vyote na pia matukio ya habari ni mengi, si rahisi kila chombo kupeleka waandishi wake kila mahali, hapa sasa ndio zikaanza bahasha za mwanzo za halali.

Hivyo ukiwa na habari yako ili waandishi waweze kufika, lazima uwapatie usafiri na kwa vile vyombo viko vingi huo usafiri kupita kote utapoteza muda mrefu, then wewe mwenye tukio lako unawapa go ahead waandishi kujitegemea kwa usafiri na wewe utawarudishia naili yao na kuwaongezea nauli ya kurudia na huu ndio mwanzo wa bahasha ambazo ni genuine.

Hivyo bahasha ya usafiri hii ndio bahasha ya kwanza genuine na halali ambayo mwandishi anapewa. Kwa vile vyombo vyenye usafiri wake sio lazima kupewa bahasha za naili. TBC ni miongoni mwa media zenye usafiri wake na mara kibao waandishi wa TBC na baadhi ya media wakimaliza kazi hutimka bila kusubiri bahasha
 
naomba kujua huu utaratibu ni wa kimataifa au ni wa waandishi wa TZ pekee yake?
Mkuu The Boss, bahasha ni dunia nzima mpaka Ikulu inatembeza bahasha, hiyo PCCB yenyewe na mpaka Polisi wanatembeza bahasha halali kama wanavyotembezewa!.
 

Je hao watoa vibahasha wananufaika na nini kama unavyosema ni zawadi, haiwezekani kila siku hao watu wanakupeni vibahasha kwa kazi mnazolipwa na waajiri wenu au makampuni yenu. Au ndio tuiite posho?

Pasco najua utavitetea vibahasha kwa nguvu zako zote ndio vinavyokunufaisha katika kupunguza makali ya maisha lakini ujue hiyo ndio Rushwa ambayo sisi Watanzania walalahoi tunaipiga vita kwa nguvu zote. Hivi umeshapokea vibahasha vingapi kutoka kwa Lowassa? na Je hizo pesa wanazitoa wapi hao wanaokupa hizo bahasha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…