Mkuu The Boss, bahasha ni dunia nzima mpaka Ikulu inatembeza bahasha, hiyo PCCB yenyewe na mpaka Polisi wanatembeza bahasha halali kama wanavyotembezewa!.
dunia nzima kivipi?
waandishi wa kenya wanapokea bahasha?
marekani?
uingereza?
south africa?????
Una bahati ndugu yangu, bahati nzuri ni kuwa PCCB wamelala na wanakoroma. Hii aya ni admission of the offense of corrupt transaction. Kupokea na kutoa vyote ni kosa.Mkuu Lunyungu, ni kweli waandishi wa habari hupokea bahasha, na mimi kama mwandishi, nimeishazipokea sana, mpaka sasa mimi ndio nazigawa, ila ukweli halisi wa mambo, sio kweli kila bahasha mwandishi anayopokea ni rushwa!. Ziko bahasha waandishi wanapokea sio rushwa na zipo bahasha kweli ni rushwa. Sasa tuanzie hapa, na mimi nitaendesha hilo somo kidogo kidogo kwa kutoa dozi ndogo ndogo mpaka hatimaye mwisho wa siku tutaelewana na mtatuelewa sisiado tunazungumzia bahasha kama bahasha na hakuna uthibitisho kuwa bahasha hizi ni rushwa!.[/COLO!.
hiyo ni kweli nakubaliana nae,inafikia kipindi mamlaka inapotaka habari zake zisikike na ziandikwe vyema hupitisha bahasha za kukirimu waandishi ama tv,kama ilivyotokea ktk lile sakata la Mauaji ya ARUSHA
Una bahati ndugu yangu, bahati nzuri ni kuwa PCCB wamelala na wanakoroma. Hii aya ni admission of the offense of corrupt transaction. Kupokea na kutoa vyote ni kosa.
Tena wanabahati sana wamewakuta hao PCCB ni toothless au kwa kiswahili wapo butu kisu chao hakikati hata keki, ]
Pasco,Mkuu The Boss, bahasha ni dunia nzima mpaka Ikulu inatembeza bahasha, hiyo PCCB yenyewe na mpaka Polisi wanatembeza bahasha halali kama wanavyotembezewa!.
hakika sikueleweka.mkuu ni the same person, ila pasco wa JF anataka sheria za JF zifuatwe, hapa kuna pasco wa JF, nje ya hapo ni Pascal Mayalla,
ina maana kwenye mijadala ya hapa JF mchukulie km Pasco wa JF.
kwa nchi za nje sina uhakika na ndio maana mfano wangu nimeutoa ndani ya TZ,ukweli upi?
nchi zoote hizo kuna bahasha????
Pasco,
Hapana. Bahasha si dunia nzima. Mimi nimefanya kazi ya uandishi kwa mashirika mawili makubwa ya Kimarekani. Ilikuwa ni marufuku kupokea bahasha ya aina yeyote ile kutoka kwa mtu, shirika, au kampuni yoyote ile unayoripoti juu yake. It is unethical. Huwezi kuchukua hela kutoka kwa mtu au kampuni unayoripoti juu yake. Hapa Marekani wale waandishi habari wanaofuatana na Obama ambao wana "cover" White House, wakisafiri kwenye Air Force one, kampuni yao hupelekewa bill na White House. Hata waandishi habari wa Uingereza nina hakika hawaruhusiwi kuchukua bahasha. Tulichokuwa tunaruhusiwa ni kuhudhuria luncheon, tuseme kama Thabo Mbeki amekaribishwa kutoa mhadhara kwenye taasisi moja ya Kimarekani, sisi waandishi wa habari tunaohudhuria tunashiriki pia kwenye luncheon hizo au dinner, depending kama ni mchana au jioni, na ofisi zetu zinakuwa na taarifa. Lakini hatuwezi kupokea gratuity yeyote kutoka kwa mbunge, senetor, gavana au CEO tunayekwenda kufanya mahojiano naye. It is illegal and unethical.
Kama hayo yanatokea katika third world usiseme ni duniani kote.
Mkuu Mzalendo80, kwa vile ndio kwanza niko kwenye mada ya bahasha zipi ni halali na zipi sii halali, kwenye bahasha halali, pia naelezea uhalali wake, lengo la hizo biashara halali, ni ama usafiri, "transport", ama chakula "lunch" ama posho "allowance", ama ni masurufu "per diem", ama ni maduhuli "imprest" etc. Matumizi ya posho na marupurupu ni halali!, sasa wanaotoa hayo marupurupu wanapata nini, jibu ni nothing, kama wa wabunge wanavyolipwa posho ya laki 200,000 kwa siku, anayewalipa anapata nini?.Je hao watoa vibahasha wananufaika na nini kama unavyosema ni zawadi, haiwezekani kila siku hao watu wanakupeni vibahasha kwa kazi mnazolipwa na waajiri wenu au makampuni yenu. Au ndio tuiite posho?
Pasco najua utavitetea vibahasha kwa nguvu zako zote ndio vinavyokunufaisha katika kupunguza makali ya maisha lakini ujue hiyo ndio Rushwa ambayo sisi Watanzania walalahoi tunaipiga vita kwa nguvu zote. Hivi umeshapokea vibahasha vingapi kutoka kwa Lowassa? na Je hizo pesa wanazitoa wapi hao wanaokupa hizo bahasha?
Naona Tanzania tumekuza culture ya kuhalalisha vitu ambavyo ni kinyume cha maadili. Sasa kama hata TAKUKURU wanatoa bahasha ni nani atakayemfunga paka kengele? Katika uandishi tunafundishwa kabisa na Pasco anajua, kwamba ni unethical kuchukua payments kwa kuandika ripoti za habari. Kwa hiyo haijalishi Pasco ataipambaje, iwe gratuity, au takrima, ni rushwa pure and simple. Tulifundishwa hivyo na ndivyo inatakiwa iwe. Vyombo vya habari vinapaswa kuwa na expense accounts za kulipia usafiri wa waandishi wao ikiwa wanafanya coverage, na vinapaswa kutoa hela ya posho ikiwa mwandishi atashinda nje akitafuta habari. So, Pasco, whichever way you cut it, it amounts to corruption. Just think, how can you write anything critical of a minister or ministry that has given you a stuffed envelope? Na ndio maana wanakimbilia kutoa bahasha kwa sababu wanajua hamtawauliza maswali magumu. Badala ya kuwa waandishi mnakuwa public information officers wa wakubwa hao.
The boss, kama nilivyosema ni dunia mzima, na kwa vile mada zinashuka kidogo kidogo, kotye huko nitafika!. Bahati nzuri nimefanya kazi ya uandishi huko Marekani, Uingereza, Uswisi, Italy, Sweeden, India na most African countries, hivyo sibahatishi bahasha halali zinatembea mwanzo mwisho!, Endelea kuvuta subira nitakufikisha mpaka huko!.dunia nzima kivipi?
waandishi wa kenya wanapokea bahasha?
marekani?
uingereza?
south africa?????
The Boss,asante
ndo maana nimeuliza huu utamaduni ni wa kimataifa au la?
taaluma ya uandishi wa habari ni taaluma universal....haiwezekani waandishi wa TZ
wakajiundia utaratibu wao wa kipekee
naoja hakuna anaenijibu hilo swali.....