Waandishi wa Habari Tanzania mna matatizo gani?

Kina Pasco
 
Sasa sisi tunaojifunza kwa kutumia simu zetu za macho mawili tuende wapi kama mnatuzibia?
 
Hayo ni makosa ya Sub-Editors sio,mwandishi wa habari husika,maana Sub-Editors ndio moyo wa media house maana hao ndo wenye jukuku la uhariri wa sarufi.

Lakini lazima tuwe wawazi tasnia ya habari kwa sasa hapa nchini ina shida kubwa sana.Na hili linachangizwa na kuibuka kwa "Citizen journalism" na hapa ndipo weredi na taaluma ya uandishi wa habari inatakiwa kuonesha umahiri wake.Media industry imejaa wasio na sifa ya kuwa journalists,ndio maana sasa ni ngumu kupata Investigative news.

Hata Interpretative reports sasa ni tia maji tia maji tu,Kuna angle nyingi za kuwasilisha kwa umma,lakini waandishi wamebaki kwenye yellow journalism.
 
Umenena yaliyo kweli kabisa.Tasnia ya habari ni kaa la moto ndani ya taifa hili,Wamiliki wa vyombo vingi wamekuwa sehemu ya kuharibu weredi wa waandishi ule wa ku-report Objective,Leo mtu akiwa maarufu kwenye social media kesho unasikia ni mwajiliwa wa media x.

Haki ya matangazo imefanya vyombo vingi vya habari kuwa makasuku kwa serikali.
 
Huenda walichoandika ndio kimejaza mioyo yao.
Nadhani ndio hivyo. Kuna gazeti huko Uingereza, The Sun, lipo tayari kotoa taarifa za uongo kumuhusu mtu mwenye wadhifa au mwenye hadhi katika jamii. Kwa kufanya hivyo, gazeti hili ambalo ni la udaku, huuza nakala nyingi sana huko nchini Uingereza. Wako tayari kulipa kiasi chochote cha pesa ambayo Mahakama itadai wamlipe yule waliyemharibia hadhi yake kama fidia. Sina uhakika kama hili gazeti nalo ni la udaku.
 
The Sun wanweza fanya prpaganda mpaka waziri mkuu anajiuzulu.
Hili bado halijawa tabloid ama kipeperushi cha kijani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…