Waandishi wa Habari Tanzania mna matatizo gani?

Waandishi wa Habari Tanzania mna matatizo gani?

View attachment 2909686

Maswali chechefu:
1. Je, gazeti la "Mwanahabari" ni la nani?
2. Je, mwandishi aliyemtaja Naibu Waziri Mkuu, Mhe Dotto Biteko, kama "BITOKE" alikuwa anamuwaza muigizaji EBITOKE?
3. Je, gazeti hili halina Mhariri?
4. Je, gazeti hili linajua kuwa linapaswa kumuomba radhi Mhe Biteko & "Bongolanderz" kwa ujumla ?

NB:
(a) Rais Mkapa:
"Huwa sipendi kuhojiwa na waandishi wa hapa nchini kwavile hawafanyi utafiti na wanauliza maswali ya hovyo yasiyo na msingi"

(b) Rais Kikwete:
"Waandishi wengi wa Tanzania ni makanjanja. Wapo ambao hawajasomea na wengine hawana weledi. Siku hizi mtoto akimaliza "Form 4" akakosa kazi kote, mzazi wake anamwambia "Huna namna, inabidi tu uwe Mwandishi wa habari". Hii si sahihi kwani uandishi wa habari ni "fourth estate". Ni kitu cha muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa"

(c) CJ Nyalali
"Waandishi wengi wanakosea sana uandikaji wa masuala ya kesi mahakamani na mara nyingi wanapotosha. Wahariri wahakikishe wanaleta mahakamani waandishi wenye uelewa kwani magazeti yao yanaweza kuchukuliwa hatua".

(d) Samwel Sitta
"Waandishi wawe makini kufuatilia Bunge. Uandishi wa upotoshaji habari za Bunge huko mbeleni unaweza kupelekea Wenye magazeti kuitwa na kuchukuliwa hatua na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge".

(e) Prof. Kabudi
"Mimi niliwahi kuwa Mwandishi wa habari. Waandishi wa enzi zetu ni tofauti kabisa na waandishi wa sasa. Waandishi wengi siku hizi wana uwezo mdogo. Siwabagazi kwani huo ndio ukweli. Kiongozi ukiongea leo, utashangaa kesho magazeti manne yana kichwa cha habari kinachofanana! Wanadeseana! Enzi zetu, Mhariri alikuwa anakuna kichwa kuwaza atokee "angle" gani. Aidha, siku hizi Kiongozi akitoa mada, waandishi hawawezi kabisa kuandika "Summary". Wanasubiri Kiongozi akiwa anatoka ukumbini kwenda kwenye gari lake na kuanza kumkibilia kama kibaka kisha wanamwambia "Mzee, Umesahau kutupa "Press Release". Hii si sawa. Tubadilike
"​
Kina Pasco
 
Sasa sisi tunaojifunza kwa kutumia simu zetu za macho mawili tuende wapi kama mnatuzibia?
 
Hayo ni makosa ya Sub-Editors sio,mwandishi wa habari husika,maana Sub-Editors ndio moyo wa media house maana hao ndo wenye jukuku la uhariri wa sarufi.

Lakini lazima tuwe wawazi tasnia ya habari kwa sasa hapa nchini ina shida kubwa sana.Na hili linachangizwa na kuibuka kwa "Citizen journalism" na hapa ndipo weredi na taaluma ya uandishi wa habari inatakiwa kuonesha umahiri wake.Media industry imejaa wasio na sifa ya kuwa journalists,ndio maana sasa ni ngumu kupata Investigative news.

Hata Interpretative reports sasa ni tia maji tia maji tu,Kuna angle nyingi za kuwasilisha kwa umma,lakini waandishi wamebaki kwenye yellow journalism.
 
Taaluma ya uandishi wa habari ni moja kati ya taaluma ambayo inatakiwa kufanyiwa reform hapa nchini vinginevyo itaendelea kuwa namba moja kwenye taaluma zilizopoteza weledi wa kazi na hii ni kutokana na mambo yafuatayo

1. Kuajiriwa kwa watangazaji na waandishi ambao hawajasomea kazi hiyo

2. Kuwepo kwa wahariri wavivu na wenye uelewa mdogo wa maudhui wanayo hariri.

3. Uwepo wa social media na online channels ambazo yoyote anaweza ku-post habari hii inaongeza chance ya upotoshaji kwani habari inatengenezwa kwa kuzingatia kupata likes na comment jambo ambalo linapelekea upotoshaji.

4. Serikali yenyewe ni tatizo na ina mchango wake katika kuibomoa taaluma hii kwani imekuwa ikitoa maelekezo ya nini kifanyike kwa vyombo vya habari, Bahati mbaya maelekezo yenyewe ni ya kichawa zaidi yaani kama vile kazi ya vyombo vya habari ni kuisifu serikali na kuimba mapambio kwa Rais. This is shame kwa wizara husika. BADILIKENI!
Umenena yaliyo kweli kabisa.Tasnia ya habari ni kaa la moto ndani ya taifa hili,Wamiliki wa vyombo vingi wamekuwa sehemu ya kuharibu weredi wa waandishi ule wa ku-report Objective,Leo mtu akiwa maarufu kwenye social media kesho unasikia ni mwajiliwa wa media x.

Haki ya matangazo imefanya vyombo vingi vya habari kuwa makasuku kwa serikali.
 
Huenda walichoandika ndio kimejaza mioyo yao.
Nadhani ndio hivyo. Kuna gazeti huko Uingereza, The Sun, lipo tayari kotoa taarifa za uongo kumuhusu mtu mwenye wadhifa au mwenye hadhi katika jamii. Kwa kufanya hivyo, gazeti hili ambalo ni la udaku, huuza nakala nyingi sana huko nchini Uingereza. Wako tayari kulipa kiasi chochote cha pesa ambayo Mahakama itadai wamlipe yule waliyemharibia hadhi yake kama fidia. Sina uhakika kama hili gazeti nalo ni la udaku.
 
Nadhani ndicho hivyo. Kuna gazeti huko Uingereza, The Sun, lipo tayari kotoa taarifa za uongo kumuhusu mtu mwenye wadhifa au mwenye hadhi katika jamii. Kwa kufanya hivyo, gazeti hili ambalo ni la udaku, huuza nakala nyingi sana huko nchini Uingereza. Wako tayari kulipa kiasi chochote cha pesa ambayo Mahakama itadai wamlipe yule waliyemharibia hadhi yake kama fidia. Sina uhakika kama hili gazeti nalo ni la udaku.
The Sun wanweza fanya prpaganda mpaka waziri mkuu anajiuzulu.
Hili bado halijawa tabloid ama kipeperushi cha kijani.
 
Back
Top Bottom