Waandishi wa habari waache kuidhalilisha dini safi ya Uislam. Aliyeiba nguruwe sio "Imam" kwa maana alichokifanya ni kinyume na miongozo ya dini yake

Waandishi wa habari waache kuidhalilisha dini safi ya Uislam. Aliyeiba nguruwe sio "Imam" kwa maana alichokifanya ni kinyume na miongozo ya dini yake

Status
Not open for further replies.
Uimamu wake ni Uislamu au Uimamu wake ni cheo chake katika jamii yake..
Iman ni kiongozi wa kidini na sio wa kijamii. Kiongozi wa kijamaa ianongozi wote lakini wa kidini anaongoza watu kadhaa wa imani yake.
 
Ulichofanya wewe ni kutusaidia sisi, tu-perceive uimamu wa muhalifu una uhusiano na Uislamu wake.. Ila inawezekana katika habari hiyo lengo la kuweka Uimamu ni kumtambua muhalifu kwa cheo chake katika jamii.
Akimtambua mhalifu kwa uongozi wake wa kidini inasaidia nini kama sio kudhalilisha wengine wenye nafasi kama yake katika dini husika?
 
Mara ngapi kwenye vyombo vya habari viongozi wa kidini wa dini ya kikristo wanaripotiwa kwenye vyombo vya habari kwa nyadhifa zao pale wanapofanya matendo maovu kwenye jamii? Mbona sijawahi kuona wakristo wakilalamika kwamba wamedhalilishwa. Mfano "Padri akutwa gesti na mwanafunzi", Mchungaji au Askofu ampa mimba muumini etc. Lengo la kuripoti wadhifa wa kiongozi wa dini ni kuonyesha umuhimu wake katika jamii tofauti na matendo yake machafu ambayo jamii haitegemei mtu kama huyo kuyafanya maana yeye ndiye anatakiwa kuyakemea. Kama wangeandika muislam aiba nguruwe kweli hata mimi ningeona haina maana ni kuchonganisha watu imani za watu wengine. HAKUNA JIPYA HAPO.
 
Akimtambua mhalifu kwa uongozi wake wa kidini inasaidia nini kama sio kudhalilisha wengine wenye nafasi kama yake katika dini husika?
Imam ni cheo chake hajamsingizia!! Pia ni sawa na mtu kuitwa "Dr.Fulani" huo udaktari ni wa kwake yeye na ni utambulisho wake hauna uhusiano na madaktari wote duniani.

Kuhusu kudhalilisha Uislamu ni suala la wewe ulivyo itafsiri hiyo habari.. Na ndo maana nasisitiza siku zote taarifa ya habari haiwezi kuwa na utambuzi uliokuwa sawa kwa kila mtu lazima tutatofautiana.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji28]
Masuala ya CCM mim siyajui kabisa mkuu. I am sorry for that.
 
Huyo mwanahabari ndio amedhalilisha nafasi ya kiongozi wa dini, na sasa Imam wote wataanza kuonekana kama wezi wa nguruwe.
Wewe naye umeamua kukolezea tu wakati mwingine jia la mtu huambatana na wadhifa wake ili kumbainisha bayana. Ni kawaida mtu kumsikia akisema mkuu wa kituo cha polisi X ndugu....., afikishwa mahakamani kujibu tuhuma kadhaa. Mbona poa tu. Na hii imekaa vizuri kweli kweli. Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Akimtambua mhalifu kwa uongozi wake wa kidini inasaidia nini kama sio kudhalilisha wengine wenye nafasi kama yake katika dini husika?
Hajasema maimamu wote ni wezi..!! Kwa uzi wako nimeshatambua wewe ni wa imani gani. Uwe wazi tu kuwa, kinachokukwaza ni huyo mheshimiwa kutuhumiwa kubeba bidhaa ambayo kwa imani yake hata kuigusa tu hiyo malighafi ni haraam so kuiiba itakuwa kaenda extra mile. Najua mtanikumbuka kwa mema siyo kwa mabaya.
 
Je, ni sahihi kuwaita Bokoharama kuwa ni "magaidi wa kiislam" ilhali uislamu unakataza uhalifu wa ugaidi?...
Je, ni sahihi kuwaita al shabaab kuwa ni "magaidi wa kiislam"?
Hivi unazungumza nini Omera??? Kwahiyo hayo makundi ya kigaidi yanaua kwa misingi ya dini ipi yakhee?

Watu wanaenda kujilipua wakisema Allah Akbar au Takibiir bado unapandisha tu kanzu hapa jamvini
 
Kwanini uhalifu alioufanya Salum Yusuph wa kwenda kuiba nguruwe uhusishwe na nafasi ya ungozi wa kidini (Imam) ilhali kitendo hicho (wizi) sio muongozo sahihi wa dini ya kiislam?
Huu ni udhalilishaji mkubwa sana kwa waislamu. Watanzania wote ni ndugu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom