Waandishi wetu bhana! Kapewa tip Tanesco vibarua wanalipwa 15,000 kwa mwezi kaileta redioni kama ilivyo

Waandishi wetu bhana! Kapewa tip Tanesco vibarua wanalipwa 15,000 kwa mwezi kaileta redioni kama ilivyo

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mwandishi wa Wasafi ambae jina sijalipata, kapata tip huko mtaani vibarua wa Tanesco wanalipwa elfu 15 kwa mwezi nae kaibeba kama ilivyo kaja nayo redioni bila hata kufanya kitafiti kidogo.

Angejiuliza tu 15,000 ukiigawa kwa siku 30 unapata jero kila siku, tenahapo akadai na NSSF wanaikata. Huyu mtu alipe nauli kiasi gani, mchana ale nini nk. na aende na utaratibu huo wa maisha kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Pamoja na mtangazaji mwenzake, Zembwela kujaribu kukosoa malipo hayo hayawezekani bado akashikilia

Sasa hivi kuna huu ujinga wa kukimbilia kutrendisha habari.......kwamba uwe wa kwanza kusema jambo fulani ili kupata wasikilizaji/watazamaji wengi na 'uvume'. Ndo maana siku hz wasikilizaji wanapotea sana; vinabaki visharobaro vya kusikiliza muziki tu.
 
Tena alivyo pimbi anajiuliza, "sijui elfu 15 au laki na nusu, ngoja nitamuuliza vizuri". Sasa si upimbi huu?!!!! Kama hakusikia vizuri kwanini amekimbilia kurusha?!!
 
media za bongo zipo kwa lengo la kuvutia wasikilizaji au watazamaji yaani wao kazi yao ni kupiga pesa tofauti na uhalisia wa media kuwa ni kukomboa kwa kuelimisha,wao huleta mada ZA kipumbavu na mara nyingi hata vipindi hufanana sababu ya kuiga iga.

fuku fuku wa umbea
 
Tena alivyo pimbi anajiuliza, "sijui elfu 15 au laki na nusu, ngoja nitamuuliza vizuri". Sasa si upimbi huu?!!!! Kama hakusikia vizuri kwanini amekimbilia kurusha?!!
Hao makanjanja wengi sana. Mradi anatangaza hata kama hajui anachosema kina maana gani
 
Ndiyo maana watu wanasema hao wanapiga makelele tu hawana hoja!
 
LABDA PER DAY
Yes, na maelezo yake yanaonesha malalamiko yao makubwa zaidi sio kipato bali wamekaa kwenye probation zaidi ya muda unaotakiwa. Kikubwa wanachohitaji ni kupewa ajira ya kudumu.. Kashindwa kuzing'amua na kuunganisha taarifa zake vizuri kuleta hoja iliyojitosheleza..
 
Kakurupuka sana.. elfu 15 kwa mwezi wasikwenda hata kufanya hicho kibarua
 
Mwandishi wa Wasafi ambae jina sijalipata, kapata tip huko mtaani vibarua wa Tanesco wanalipwa elfu 15 kwa mwezi nae kaibeba kama ilivyo kaja nayo redioni bila hata kufanya kitafiti kidogo.

Angejiuliza tu 15,000 ukiigawa kwa siku 30 unapata jero kila siku, tenahapo akadai na NSSF wanaikata. Huyu mtu alipe nauli kiasi gani, mchana ale nini nk. na aende na utaratibu huo wa maisha kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Pamoja na mtangazaji mwenzake, Zembwela kujaribu kukosoa malipo hayo hayawezekani bado akashikilia

Hawa ndo ilitakiwa didy kuwapitia kuliko pdiddy kuwafumua kina Ice cube, snoop, dr Dre na Jay Z.

babukijana
 
Back
Top Bottom