Waarabu hawajawahi kuwashinda Wayahudi Tangu Siku ya kwanza Ibrahim alivyokanyaga Ardhi ya Kanaani

Waarabu hawajawahi kuwashinda Wayahudi Tangu Siku ya kwanza Ibrahim alivyokanyaga Ardhi ya Kanaani

Nimeshamwambia kwenye comment yangu hizi mada anazojaribu kuzileta sio size yake na hajui kama hajui akishakunywa sungur A anaandika vitu asivyovijua alafu humu kuna wAtu wapo kama vichwA vyao ni madumu,weka gongo dumu sawa,weka oil dumu sawa,weka maji dumu hewala,yaani yamekubali kufikiriwA na kusemewa kwa niaba yaO,Jf siku hizi Ovyo kabisa.
Tatizo wajinga wenye access na internet wamekuwa wengi sana siku hizi, hivyo unakuta wanaandika maujinga yao tu online.

Zamani waliokuwa na access ya internet walikuwa wachache ila wanaojielewa/walioelimika..
 
Lakini hao wayahudi ndo jamii iliyo kaa na utumwani kuliko jamii yoyote hapa duniani.
Hichi kiburi walicho nacho sasa hivi wameanza kukipata miaka 75 tu iliyo pita baada ya kupata masponsa wa kuwaweka hapo mashariki ya kati kimkakati na masilahi ya uingereza na Marekani.

Alafu huu uadui kati ya waarabu na wayahudi ni wakubuni kwa ajili ya masilahi ya kikundi fulani kwa sababu mwarabu na myahudi hawajawahi kuwa maadui.
Katika historia hakuna sehemu yeyote ambayo waarabu walisha watesa au kuwauwa wayahudi.
Bali wenye historia ya kutesa na kuuwa wayahudi ni wazungu ambao leo wanajifanya eti ndo marafiki wao.

Wakati wazungu wakiwatesa na kuwauwa wayahudi huko barani Ulaya wakati huo wayahudi walikuwa wakiishi kwa amani kwenye nchi za kiarabu.
 
Kama Kuna mtu ambaye anafikiri kuwa Muarabu atamshinda Myahudi basi atakuwa anamatarajio yasiyowezekana
Muarabu ni nani? Nachojua Abraham alitokea Iraq na pia Yakobo alioa uarabuni huko mesopotamia so watoto wa Yakobo wana vinasaba vya uarabu!! Cha ajabu unasema Waarabu vs Wayahudi?

Embu kajifunze upya history ya middle east. Waarabu na wayahudi wote ni Semites tu!! Maana hata Abraham alikua na watoto wengine baada ya isaka je nao ni wayahudi? Na kama sio wayahudi je hawana haki ya urithi wa Abraham?
 
Huna ulijualo..
Soma historia ili UJUE na uache kujidanganya na kudanganya mambulula wenzako..

Kwa kukusaidia tu, nenda ugoogle kitu kinaitwa RASHIDUN CALIPHATE, Hapa soma kwa nini wayahudi mpaka leo wanamchukia sana Mtume Muhammad (SAW).

Kwenye hii Rashidun Caliphate, pia msome sahaba/khalifa anaitwa Omar Al Khattab jinsi alivyoukamata mji wa Jerusalem kutoka kwa makafiri, pia tafuta ujue kwa nini Wayahudi mpaka leo hii wanamkumbuka na wanamuheshimu sana huyu mtu..

Halafu ukitoka hapo msome mtu anayeitwa Salahuddin Al Ayyubi, soma jinsi alivyoutwaa mji wa Jerusalem na jinsi alivyoulinda dhidi ya maadui wa kikafiri. Soma na jinsi alivyoteketeza kwa moto jeshi zima la makafiri walipotaka kuuchukua mji wa Jerusalem.

Soma uelimike uache kudanganya Mambulula wenzako..

Wewe ndio unatakiwa usome uelimike hiyo miaka ya kuanzia 300AD Mpaka 1000AD Nchi ya Israel na viunga vyake ikiwemo Jerusalem haikuwa chini ya Utawala wa Mayahudi ilikuwa chini ya Dola la Rumi, chini ya Catholic church

Sasa hao Sahaba wa Mtume hawakuwahi kukuta Utawala wa Mayahudi katika Eneo hilo.

Wewe ndio unatakiwa kusoma vizuri hiyo hadithi yako.

Muarabu hajawahi kuwa tishio kwa Myahudi na hatakuja kuwahi kuwa tishio kwa Myahudi

Ni sawa na useme, kipindi Wayahudi wapo uhamishoni huku na huko duniani ikiwemo nchi za Ulaya, Afrika ya kaskazini na baadhi ya Maeneo ya Asia huku wachache wakiwa hapo Kanaani(ambapo wanepaita Palestine) useme Waarabu ni nchi yao na waliwahi kuwashinda wayahudi jambo ambalo sio sahihi.
 
Kwema Wakuu!

Kwa wasioelewa haya mambo wanaweza Kuona ni mapya lakini hakuna jipya hata Moja. Mengi ni marudio.

Tangu Ibrahim akanyage Hapo Kanaani Muarabu na jamii za Mashariki ya Kati hazijawahi kuwashinda Mayahudi.

Ikumbukwe Kuwa Mayahudi ndio yalikabidhiwa Mkoba na Ibrahim ambao Mkoba huo Ibrahim aliutoa kwa Babu yake aitwaye Nuhu, kisha Nuhu aliutoa kwa Babu yake Aitwaye Henoko, kisha Henoko aliutoa Mkoba huo kwa Babu yake aitwaye ADAMU, Kisha Adamu alipewa na aliyemuumba.

Mayahudi yana Siri nyingi sana za huu ulimwengu mbali na Mikoba yaliyopewa.
Kuyashinda ni kazi ngumu Sana.

Hapo waarabu watapiga Mark time sana na watachapika vilivyo.

Kuna watu wanawataja Wachina kama suluhu ya huu ulimwengu lakini China kinasaba ametoka kwa HAMU, Yaani China na Waafrika wanaundugu hivyo haitarajiwi hivi mapema kama china atashika Utawala wa huu ulimwengu

Kama Kuna mtu ambaye anafikiri kuwa Muarabu atamshinda Myahudi basi atakuwa anamatarajio yasiyowezekana.

Muarabu amezidiwa kwenye Maeneo nyeti na Myahudi hata kile wanachojivunia ambao ni huo uislam umeathiriwa vilivyo na uyahudi kuliko jambo lolote lile.

Waajemi yaani Iran walishawahi kuwachukua baadhi ya mayahudi utumwani, ngoja tuone

Ngoja tuone huko Lebanon nini huko Mashariki ya Kati.

Mlale unono
Ila huwa kuna mambo yana mchanganyo.
Ila Jews na Muslims ni kithibitisho cha ugomvi wa kudumu wa wanandugu in reference to Bible.
So najiulizaga Mungu kwanini karuhusu mapigano ya wanandugu? Au ndo hayo mambo yanaingia mpaka kwa vizazi vyetu sasa🙆
 
Muarabu ni nani? Nachojua Abraham alitokea Iraq na pia Yakobo alioa uarabuni huko mesopotamia so watoto wa Yakobo wana vinasaba vya uarabu!! Cha ajabu unasema Waarabu vs Wayahudi?
Muarabu ni mtu yeyote ambaye amezaliwa na anaasili ya Maeneo ya Yemen, Saudia Arabia, Qatar, Oman hao ndio Waarabu OG ingawaje walitawanyika wengine kwenda Maeneo ya karibu.

Yakobo alioa Waebrania wenzao. Ndugu za Mama yake aitwaye Rebecca. Waebrania sio Waarabu. Wapo mpaka leo na kiebrania kipo mpaka leo na kinazungumzwa na Waisrael(Wayahudi) ingawaje kiebrania na kiaramu vinaendana

Embu kajifunze upya history ya middle east. Waarabu na wayahudi wote ni Semites tu!! Maana hata Abraham alikua na watoto wengine baada ya isaka je nao ni wayahudi? Na kama sio wayahudi je hawana haki ya urithi wa Abraham?

Waarabu na Wayahudi wote DNA ni Kutoka kwa Shemu (Semites) lakini Kila mmoja Babu yake, Wayahudi Babu yao ni Ibrahim ambaye ni muebrania, kutaka kwa Eber mtoto wa Shemu, mtoto wa Nuhu.
Waarabu wao sio Waebrania ila Kuna jamii ya kiarabu ambayo inadamu ya Waebrania kutokana na Ishmael(muebrania) kuoa Muarabu baada ya kulowea katika ukanda na jangwa la Arabia huko.
Inasemekana Muhamad ndio anavinasaba kutoka huko.

Kuhusu suala la urithi, Kila mtoto alipewa Maeneo ya kurithi.
 
Ila huwa kuna mambo yana mchanganyo.
Ila Jews na Muslims ni kithibitisho cha ugomvi wa kudumu wa wanandugu in reference to Bible.
So najiulizaga Mungu kwanini karuhusu mapigano ya wanandugu? Au ndo hayo mambo yanaingia mpaka kwa vizazi vyetu sasa🙆

Ukiona hivyo Kuna mmoja kamtapeli mwenzake.
 
Vipi Mohammed Ali wa Ottoman? Au vipi 1st and 2nd crusades? Uko empty kwenye history

Mkuu hao unaowataja ni mwaka gani na walikuta Utawala gani hapo Israel?
Utawala wa Ottoman Empire hao Waturuki haukukuta Dola la wayahudi hapo Kanaani, walikuta tayari hilo eneo limekaliwa na tawala mbalimbali ikiwemo Tawala la Roma, tawala za maswahaba wa Muhammad, , hao ottoman walikuta eneo zima la Israel Wayahudi hawazidi Asilimia 10. Wengi walikuwa uhamishoni
 
Nimeshamwambia kwenye comment yangu hizi mada anazojaribu kuzileta sio size yake na hajui kama hajui akishakunywa sungur A anaandika vitu asivyovijua alafu humu kuna wAtu wapo kama vichwA vyao ni madumu,weka gongo dumu sawa,weka oil dumu sawa,weka maji dumu hewala,yaani yamekubali kufikiriwA na kusemewa kwa niaba yaO,Jf siku hizi Ovyo kabisa.

Nasubiri hiyo history yako uiweke hapa
 
Wewe ndio unatakiwa usome uelimike hiyo miaka ya kuanzia 300AD Mpaka 1000AD Nchi ya Israel na viunga vyake ikiwemo Jerusalem haikuwa chini ya Utawala wa Mayahudi ilikuwa chini ya Dola la Rumi, chini ya Catholic church

Sasa hao Sahaba wa Mtume hawakuwahi kukuta Utawala wa Mayahudi katika Eneo hilo.

Wewe ndio unatakiwa kusoma vizuri hiyo hadithi yako.

Muarabu hajawahi kuwa tishio kwa Myahudi na hatakuja kuwahi kuwa tishio kwa Myahudi

Ni sawa na useme, kipindi Wayahudi wapo uhamishoni huku na huko duniani ikiwemo nchi za Ulaya, Afrika ya kaskazini na baadhi ya Maeneo ya Asia huku wachache wakiwa hapo Kanaani(ambapo wanepaita Palestine) useme Waarabu ni nchi yao na waliwahi kuwashinda wayahudi jambo ambalo sio sahihi.
Kwahiyo Biblia inaposema wayahudi walitandikwa hadi wakatekwa kupelekwa Babylon ya kale na Assyria walikua wanadanganya?
 
Mkuu hao unaowataja ni mwaka gani na walikuta Utawala gani hapo Israel?
Utawala wa Ottoman Empire hao Waturuki haukukuta Dola la wayahudi hapo Kanaani, walikuta tayari hilo eneo limekaliwa na tawala mbalimbali ikiwemo Tawala la Roma, tawala za maswahaba wa Muhammad, , hao ottoman walikuta eneo zima la Israel Wayahudi hawazidi Asilimia 10. Wengi walikuwa uhamishoni
Usikimbie kwani kwenye biblia dola ya wayahudi ilimalizwa na nani hadi wakaenda utumwani miaka maelfu? Hao Babylonia walivamia Jerusalem mwaka 587 kabla ya kristo na wakauteketeza mji wakaondoka na wayahudi. Sasa sijui kwa definition yako watu wakutoka Iraq/Syria ya miaka hiyo ni waarabu au sio waarabu?
 
Unaongea kitu ambacho hujui ,yaani chukulia mfano wa juzi tu kabla ya viata ya pili ya dunia 1945, wayahudi hawana nguvu ya kupigana kama wangekuwa kweli wanayo nguvu wangempiga Adolf Hitler, wale pale n wazungu ili wapo jewish rab ndani ya ile nchi hata iran wapo .
Hitler tu kaua zaidi ya milion 6 ya wayahudi 😀 😀 .

SIx days war imepigwa 1967 baada ya wazungu kuwa miongoni wa wengi katika taifa lile .Pia, jaribu kuunganisha historia hayo mataifa mengi ni ya juzi haypo kwenye maandiko , ukienda kimaandika hata Iran ni miongoni mwa jews.

Narudia tena wale ni wazungu , wayahudi wameteswa wakiwa hawana ngvu miaka ya 1940 walikuwa bado dhaifu hawana muelekeo ...Yule Netanyhulu ni settler kutoka poland ndio amekaza pale ...Wayahudi wanaish vzuri na jamii za pale sio hawa wazungu
 
Usikimbie kwani kwenye biblia dola ya wayahudi ilimalizwa na nani hadi wakaenda utumwani miaka maelfu? Hao Babylonia walivamia Jerusalem mwaka 587 kabla ya kristo na wakauteketeza mji wakaondoka na wayahudi. Sasa sijui kwa definition yako watu wakutoka Iraq/Syria ya miaka hiyo ni waarabu au sio waarabu?
Hamna anachojua atakuchanganya kwa sababu majina ya sasa hapo zamani hayakuwepo kabisa .
 
Yakobo alioa Waebrania wenzao. Ndugu za Mama yake aitwaye Rebecca. Waebrania sio Waarabu. Wapo mpaka leo na kiebrania kipo mpaka leo na kinazungumzwa na Waisrael(Wayahudi) ingawaje kiebrania na kiaramu vinaendana
Yakobo alizaa na wanawake wanne sasa hao vijakazi aliozaa nao walikua waebrania? hao watoto aliozaa kupitia vijakazi ni vinasaba gani?
amezaliwa na anaasili ya Maeneo ya Yemen, Saudia Arabia, Qatar, Oman hao ndio Waarabu OG ingawaje walitawanyika wengine kwenda Maeneo ya karibu.
Hii sio sawa maana jamii zimehama sana, mfano Abraham alitokea Iraq huko ila unasema sio muarabu sasa hapo Oman sijui saudia ndio walitokea kina Ayoub na Nabii Obadiah je nao walikua waarabu?
Waarabu na Wayahudi wote DNA ni Kutoka kwa Shemu (Semites) lakini Kila mmoja Babu yake, Wayahudi Babu yao ni Ibrahim ambaye ni muebrania,
Well and good, Sasa basi Abraham alikua na watoto wengine nje ya isaka je sio waebrania au wayahudi? Na kizazi chao kinatambulikaje? Hawa watoto alizaa na mshangazi anaitwa Keturah wapo watatu!! Au unataka kusema uebrania ulibakia kwa Isaka tu na sio watoto wengine wa Abraham?
Kuhusu suala la urithi, Kila mtoto alipewa Maeneo ya kurithi
Hapana, huwa mnasema wenye ardhi ya Israel ni wayahudi na mnarejea vitabu vya dini kuwa wayahudi ndio wana haki. Sasa nchi ya ahadi alipewa Abraham na yeye ana watoto watano how comes mtu mmoja tu ndio aonekane ni muebrania halisi na wengine wote 4 wanaitwa wavamizi ilihali ni watoto halali wa Abraham? Mungu alitoa ahadi kwa Abraham kwanini wajimilikishe watoto wa mjukuu mmoja tu?
 
wayahudi ndio wana haki. Sasa nchi ya ahadi alipewa Abraham na yeye ana watoto watano how comes mtu mmoja tu ndio aonekane ni muebrania halisi na wengine wote 4 wanaitwa wavamizi ilihali ni watoto halali wa Abraham? Mungu alitoa ahadi kwa Abraham kwanini wajimilikishe watoto wa mjukuu mmoja
Ahadi alipewa Ibrahim ila Yakobo ndiye alikuwa mrithi.

Ndio maana wote Ishmael, Esau n.k, waliondolewa wasilete challenge kwa mrithi aliyekusudiwa(Yakobo)

Lakini hawakuachwa bila kitu, walipewa maeneo.
Ila nje ya lile la ahadi.
 
Yakobo alizaa na wanawake wanne sasa hao vijakazi aliozaa nao walikua waebrania? hao watoto aliozaa kupitia vijakazi ni vinasaba gani?
Hii sio sawa maana jamii zimehama sana, mfano Abraham alitokea Iraq huko ila unasema sio muarabu sasa hapo Oman sijui saudia ndio walitokea kina Ayoub na Nabii Obadiah je nao walikua waarabu?
Wake za Yakobo wote walikuwa watoto wa baba Mmoja Laban.

Ibrahim sio Muarabu, Ibrahim ni muebrania

Ayoub hakuwa muebrania wala Muarabu

Hakuna nabii Muarabu zaidi ya Muhammad

Well and good, Sasa basi Abraham alikua na watoto wengine nje ya isaka je sio waebrania au wayahudi? Na kizazi chao kinatambulikaje? Hawa watoto alizaa na mshangazi anaitwa Keturah wapo watatu!! Au unataka kusema uebrania ulibakia kwa Isaka tu na sio watoto wengine wa Abraham?
Watoto wengine wa Ibrahim walitoa mataifa mengine kama Wamidiani, waishmael, waedomu, n.k

Uebrania ulibaki kwa watoto wa Isaka na Yakobo
Ndio maana mpaka leo hii taifa linaloongea kiebrania ni Waisrael mpaka leo hii. Akiwemo huyo Benjamin Netanyau

Hapana, huwa mnasema wenye ardhi ya Israel ni wayahudi na mnarejea vitabu vya dini kuwa wayahudi ndio wana haki. Sasa nchi ya ahadi alipewa Abraham na yeye ana watoto watano how comes mtu mmoja tu ndio aonekane ni muebrania halisi na wengine wote 4 wanaitwa wavamizi ilihali ni watoto halali wa Abraham? Mungu alitoa ahadi kwa Abraham kwanini wajimilikishe watoto wa mjukuu mmoja tu?

Wanasema hivyo kwa sababu ya sheria za urithi za wakati huo.
Ibrahim alimrithisha Isaka badala ya Ishmael, na watoto wa Ketura.
Isaka akamrithisha Yakobo badala ya Esau.

Masuala ya urithi yanatolewa kisheria ma utashi wa mzazi.

Hivyo kuuliza hao wengine hawana HAKI hiyo ni ishu nyingine kwa sababu hata huku Afrika kulikuwa na tamaduni hizo.
 
Back
Top Bottom