Waarabu kushangilia huku wakipeperusha bendera ya Tanzania inatuma ujumbe gani?

Waarabu kushangilia huku wakipeperusha bendera ya Tanzania inatuma ujumbe gani?

Acheni kupotosha na kudanganya. Hao ni Watanzania madhehebu ya Shia wakiwa katika Umra katika maeneo ya Karbala nchini Iraq. Wanafanya hivyo kila mwaka na hujitambulisha kuwa wao ni Watanzania sawa na wale wanaokwenda kuhiji Mecca na Madina. MSIPOTOSHE !!!
Sasa hapo upotoshaji uko wapi? Nimeamini kilicho semwa ni cha kiimani na kipo sawa.
 
Mleta mada una akili za kijinga sana,ni umasikini wa akili yako ndio umekufanya kupost hii thd ambayo wala huwajui hao wanaoimba kwenye hiyo clip wala hujui hata wanaimba nini,

Hiyo ni ibada ya washia wakiwa kwenye mji wao mtakatibu wa Karbala Iraq,na hua wanaenda kwenye mji wao mtakatifu wa Najaf kila mwaka ambako ndio lipo kaburi la Iman Husayn,hii ibada hufanyika kila mwaka ambayo kwao ni Hija hiyo,

Hiyo ibada hua wanaimba kwa lugha ya kishia huku wakijipiga vifua,hiyo lugha sio kiarabu wala hao watu sio waarabu,

Hao waumini ni wabongo,wameamua tu kubeba bendera ya nchi yao,ni kama wewe uende kuangalia mechi ya kombe la Dunia kisha upeperushe bendera ya nchi yako,

Wewe Mama unaishi maisha ya mateso sana kwa chuki zako za kijinga na ukosefu wa elimu pia huna uwezo wa kufikiri na kuchambua mambo kabla ya kukurupuka na kuja kutupia hapa uchafu wako.
Halafu nchi hii kuna watu wa ajabu sana, kwani hakuna waarabu wa Tanzania? hakuna wahindi wa Tanzania? hakuna waajemi wa Tanzania? kuna waarabu wengi sana wa Tanzania. Tusianze kutaka kufungua makaburi hapa kuna watu wana majina ya kitutsi na kihutu wengi tu lakini wa Tanzania, tena kule kwa wazee wa waraka majina mengi ya Kihutu na Tustsi.
 
Back
Top Bottom