Waarabu na Wahindi wanawezaje ku-manage biashara kubwa wakiwa na umri mdogo?

Waarabu na Wahindi wanawezaje ku-manage biashara kubwa wakiwa na umri mdogo?

Yule kijana adi bio ya insta kaweka allys star sasa ukute kawekeza sijui basi ngapi😂 ila all in all watu wa forex wanapata pesa nyingi kwa kufanya mentorship na sio pesa za wao kutoa sokoni forex😂
😂😂😂😂
 
Biashara ya magari ni sawa kabisa baba kaamua kumrithisha mtoto magonjwa ya moyo kama presha na kisukari,hakuna mfanyabiashara yeyote wa mabasi ambaye hana presha ama kisukari!
Nimefanya biashara ya Daladala nikaona ile presha yake sio ya kitoto nikabadili biashara
 
Leta uzoefu wako kwenye biashara ya daladala
 
Shida ziko nyingi sana lakini nadhani hizo nazo tukaziangalie:

1. Wahindi au Waarabu kwao biashara ni uti wa mgongo wa maisha yao na WATOTO WAO WANAKULIA KATIKA KAZI HIZO tofauti na waswahili wengi ambao TUMEKULIA KATIKA UKULIMA NA UFUGAJI halafu unataka kufanya biashara ya kuuza na kununua au service. Kwa hakika watatoboa talented au walioamua kujitoa ila wengi watafeli.

2. Wengi wetu huwatenga watoto wetu na tunavyovifanya kama nyenzo za kujipatia vipato hivyo unakuja kulqzimisha kumfunza mtoto ameshakuwa mkubwa na YEYE ana ndoto zake hivyo LAZIMA AHARIBU.

3. Kujenga nidhamu na kusomesha watoto masomo yanayoendana na kile tulichowakuza nacho au kinafanywa na familia. wewe una biashara ya hapa na pale halafu TOTO linasoma SOCIOLOGY, lazima mvurugane kwa HATAWEZA KUMAINSTREAM BIASHARA YAKO..... Angalia MO DEWJI alichosomeshwa na WAZAZI wake na nafasi alipewa baada ya kumaliza SHULE!!!!

Ongeza na nyingine
Usisahau wengi wa hao wahindi ni second au third generation! Sie wengi ni first generation katika Biashara, maana yake tumesimamisha Biashara wakati tushafika 50s na kama ulivyosema Watoto washakua, hawakukulia katika Biashara kama Mo! Ona kama Nakiete wanaenda vizuri sana! Kuna familia za kibongo zimejikita katika family business lakini si first generation!
 
Wahindi hawataki kazi za kuajiriwa.
Si sawa ila wengi wanakuzwa kuingia katika family business! Kabla ya Darasa la kwanza anapangiwa atasoma nini ili akafanye nini badaye! Succession plan. Kuna baadhi ya familia zimeanza Ona hata Watoto wa Mengi
 
Kuna Dogo mmoja anaitwa elikanafx ni mtu wa forex alisema hayo mabasi anashare zake 😂😂😂na yey ni mmiliki huyu kijana na mwanafunzi wa Ontario .
Kusema dogo mmoja ana share zake na hata mimi naweza kusema nna share zangu sasa litapokuja suala la kuambiwa tulete ushahidi hapo ndio inakua ngoma, ila kusema ni rahisi sana
 
Kusema dogo mmoja ana share zake na hata mimi naweza kusema nna share zangu sasa litapokuja suala la kuambiwa tulete ushahidi hapo ndio inakua ngoma, ila kusema ni rahisi sana
😂😂😂Nawajua waarabu ni wabinafsi sana na wabaguzi kweny makampuni yao washirikiane na mtu mweusi kwa nadra sana .
 
Biashara ya magari ni sawa kabisa baba kaamua kumrithisha mtoto magonjwa ya moyo kama presha na kisukari,hakuna mfanyabiashara yeyote wa mabasi ambaye hana presha ama kisukari!
Nimefanya biashara ya Daladala nikaona ile presha yake sio ya kitoto nikabadili biashara
Ukiwa na chuma moja ni lazima uwe na presha, ila ikifikia hatua unazo nyingi hizo presha huwa zinapingua maana hautahusika kwenye kila kitu moja kwa moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashara ya magari ni sawa kabisa baba kaamua kumrithisha mtoto magonjwa ya moyo kama presha na kisukari,hakuna mfanyabiashara yeyote wa mabasi ambaye hana presha ama kisukari!
Nimefanya biashara ya Daladala nikaona ile presha yake sio ya kitoto nikabadili biashara
Ukinunua gari ya mkononi au ukiagiza nje na ikachakalia kwako na wewe si mtunzaji wa magari+ kubadili madereva kila siku, basi hio biashara wewe hauna ujuzi nayo na hautaweza kuwa kwenye hiyo biashara kwa muda mrefu na presha na sukari utaipata tuu.

Biashara ya gari inataka ulijue gari sawa na unaona huyo kijana hapo naye anaendesha lengo ni kuijua gari kiundani zaidi na zaidi.

Mimi naikubali sana hii biashara inalipa saana saaana lakini ndio hapo juu uwe umekamilika kuyajua magari na madereva tabia zao pia.
 
Wakuu Wenzetu Waarabu na Wahindi Wanawaandaa Watoto Wao kuwa na uwezo wa ku manage Biashara kubwa kama hii ya mabus wakiwa vijana wadogo.

Huyu Anaitwa Amran Ally Mohamed Said au Amran Kifaru ndio mmiliki na msimamizi Mkuu wa Mabus ya Ally's Star.

Ally Star ni Mabus yanayofanya Root za Dar To Mwanza, Kuna Mwanza to Tabora, Kuna Mwanza Kahama, Kuna Mwanza To Dom nk.

Mzee Wake Amran Kifaru ameamua kumwachia umiliki na usimamizi Wa Hii Biashara Kubwa huyu Kijana Mdogo Kabisa.

Je, Sisi Tunakosea wapi Kwenye kuwaandaa Watoto wetu kufanya Na Kusimamia miradi mikubwa Kama Hii?

View attachment 2405585
Kuna mengi sana hawa jamaa huwa wanafanya kwenye hizo biashara zao ambayo hayawekwi hadharani, ingawa wengi tunaamini kuwa hawa jamaa wana akili na bidii sana katika kazi. Kila biashara ina siri yake ndiyo maana sio kila muhindi au Mwarabu ni tajiri kama tunavyoaminishana

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Chaga na wakinga wanaweza pia,it's not a rocket science,
 
Shida ziko nyingi sana lakini nadhani hizo nazo tukaziangalie:

1. Wahindi au Waarabu kwao biashara ni uti wa mgongo wa maisha yao na WATOTO WAO WANAKULIA KATIKA KAZI HIZO tofauti na waswahili wengi ambao TUMEKULIA KATIKA UKULIMA NA UFUGAJI halafu unataka kufanya biashara ya kuuza na kununua au service. Kwa hakika watatoboa talented au walioamua kujitoa ila wengi watafeli.

2. Wengi wetu huwatenga watoto wetu na tunavyovifanya kama nyenzo za kujipatia vipato hivyo unakuja kulqzimisha kumfunza mtoto ameshakuwa mkubwa na YEYE ana ndoto zake hivyo LAZIMA AHARIBU.

3. Kujenga nidhamu na kusomesha watoto masomo yanayoendana na kile tulichowakuza nacho au kinafanywa na familia. wewe una biashara ya hapa na pale halafu TOTO linasoma SOCIOLOGY, lazima mvurugane kwa HATAWEZA KUMAINSTREAM BIASHARA YAKO..... Angalia MO DEWJI alichosomeshwa na WAZAZI wake na nafasi alipewa baada ya kumaliza SHULE!!!
KWANZA HAO WAZAZI WENYE HIZO HELA KWA WAAFRICA NIWACACHE SANA NA BADO FACTORS ZAKO ZINACHANGIA SANA mzazi anauza mifugo ili mtoto akasomee ualimu
 
Yuko makini

Hebu ona yeye ndie bosi mkuu wa Ally Star lakini Mwangalie kavaa uniform ya madereva ya wanaoendesha basi.

Yawezakana Siku hiyo.dereva alikuwa na udhuru kafiwa,anaumwa labda akaona ashike mwenyewe

Angalia machoni alivyo na umaskini akiwa usukani wa bus

Nampongeza kwa Kweli.Ally Star ana mania ya mabasi na mallori kuweza kuendesha kampuni kubwa kama Ally Star kwa umri wake anastahili pongezi sana
Dogo kabla ya kupeww kampuni kwanza anaingia garage ya faza kujua masuala ya ufundi wa mabasi, akishakwiva humo huanza kupewa basi kadhaa azisimamie kwa muda ili ajifunze mlolongo mzima wa biashara na changamoto zake kisha huanza kutumwa safari za china kwenda kununua magari,spare n.k akishakwiva katika safari za biashara za kimataifa na usimamizi wa mabasi kadhaa hapa nchini ndio hufikia kukabidhiwa aiendeshe kampuni.

Pia wazee wanahakikisha mtoto wao anaoa akiwa na umri mdogo ili aepukane na uzinzi naufujaji wa pesa.
 
KWANZA HAO WAZAZI WENYE HIZO HELA KWA WAAFRICA NIWACACHE SANA NA BADO FACTORS ZAKO ZINACHANGIA SANA mzazi anauza mifugo ili mtoto akasomee ualimu
Ninachomaanisha hicho kidogo ambacho mzazi anafanya anapaswa kumurithisha mwanae akifahamu vizuri ili kiwe ni miongoni mwa fursa at disposal for future gowth
 
Nchi zote Africa chini ya jangwa la sahara, kuna shida!

Utumwa wa kifikra
-kupenda vya bure
-kupenda shotkat
-ulafi na uasherati (ndo maana ukimwi unaongoza kwenye hili bara 👀)
-hakuna uzalendo
-kutokujiamini (kwa wale walimu na walio vyuoni, mtakubali kabisa kuwa wanachuo wengi hawajiamini, ukiuliza swali kila mtu kimya, ukisema mtu ajitolee kufanya kazi flani kila mtu anakimbia, hili ni janga kubwa kitaifa maana 'wasomi' hawa wanakuja kuwa wa mchongo baadae!)

Kwa sababu gani?

Elimu yetu haitufundishi kuendana na mazingira yetu badala yake inatufanya tegemezi!

Msome mwalimu Nyerere hapa utaelewa:
Mwalimu aliandika kuhusu Elimu Ya Kujitegemea inayomuandaa mtoto kuja kuwa na faida kwa jamii
na sio elimu ya sasa inayompa karatasi la kutangatanga akisaka fedha ya mwisho wa mwezi ambayo ataifuja na kusubiri mwezi mwingine.

Kwa maelezo zaidi:

👇 👇 👇
 
Attachments

Kuna mengi sana hawa jamaa huwa wanafanya kwenye hizo biashara zao ambayo hayawekwi hadharani, ingawa wengi tunaamini kuwa hawa jamaa wana akili na bidii sana katika kazi. Kila biashara ina siri yake ndiyo maana sio kila muhindi au Mwarabu ni tajiri kama tunavyoaminishana

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app

ila ni nadra kukuta omba omba muarabu au muhindi kitaa! tofauti na wabongo
 
Back
Top Bottom