Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kila mara na kila wakati tumekuwa tukisema hapa JF, uislamu hauwezi kuwaunganisha waarabu na haujawahi kuwaunganisha waarabu (kwa sababu waarabu sio waumini wazuri wa kiislamu japokuwa hutumia uislamu kama utamaduni wao wa kujitambulisha, kujisambaza duniani na kufunikia mambo yao).
Ni rahisi sana kwa siasa na maslahi ya kiuchumi kuwaunganisha waarabu kuliko dini.
Kwa mfano tangu vita vya mashariki ya kati vilipuke 7 Oktoba, mpaka leo hii hakuna taifa lolote la kiarabu lililojitoa kimasomaso kuwaunga mkono kivita HAMAS. Jamaa wameendelea kutembezewa kichapo kutoka kwa Israel mpaka kupelekea karibu ukanda wote wa Gaza kufutika.
Sasa kimbembe kimemkuta Iran, kachokozwa na Israel kwa maafisa na makamanda wake kuuwawa kwa mabomu yaliyosambaratisha ubalozi wake kule Syria. Iran akachimba mkwara mzito, akajiandaa fresh kwa wiki mbili akaanza kufyatua makombora ya masafa ya mbali (Drones, cruise, missiles) zaidi ya 300 kuelekea maeneo mahususi ndani ya Israel lakini karibu yote yakizuiwa kirahisi kabisa huku nchi za kiarabu zenye misingi ya kiislamu kama Jordan na Saudi Arabia zikihusika kuisaidia Israel isiguswe na kombora lolote la Iran.
Kama vita hii itaendelea, huenda Israel ikatumia anga na ardhi ya nchi za kiarabu kuitandika Iran.
Zile fikra za watu weusi kuukumbatia uarabu kwa kigezo cha kudumisha umoja wa kiimani baina ya waumini wa kiislamu taratibu zinaanza kupungua na huko baadaye huenda zikafutika.