FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Baada ya nchi za Kiafrika Mali, Burkina Faso na Niger kutengwa na Waafrika wenzao ndani ya umoja wa ECOWAS na kutiwa adabu ya kufungiwa biashara zote, kufungiwa umeme na huduma zote za kibinadamu hadi chakula.
Wametengwa baada ya nchi hizo kupinduwa serikali zilizokuwa zinajineemesha kwa kundi la watu fulani tu na wakoloni waliokuwa wakiwadanganya kuwa wanaweza kuwalinda daima.
Cha ajabu, nchi za Kiafrika kama Nigeria na zote wanaowazunguka zilikutana na kuamuwa kuwatenga wenzao kwa kuwasikiliza wakoloni.
Katika sherehe za miaka 48 ya Morocco Mfalme Mohamed wa Morocco akatangaza kuzibeba nchi hizo zilizotengwa nankuwekewa vikwazo kwa hali na mali, na potelea mbali nchi zingine zote zilizowatenga zifanye zinavyotaka.
Amewaruhusu watumie bandari zake, Barabara na Raiway na amejitolea kujenga reli, barabra za kuwafikisha bandarini. Pia amewaambia na kuwaahidi kuwa chochote wanachohitaji wasihangaike, hao ni ndugu zake. Bila kuongea, ameonesha kuwa uzalendo wa Afrika haupo kwenye rangi zetu bali kwenye nia na mioyo yetu.
Viongozi wa nchi hizo walitokwa na machozi baada ya Mfalme wa Morocco kutangaza hayo bila kuombwa wala kutowa dalili za awali. Wanasema hawajategemea.
mengine zaidi jionee mwenyewe:
View: https://youtu.be/Eva9vB5Cexo?si=MC3nny7LL4Z6fnKM