Jamaa ameiweka sana kitaalamu. Baada ya football kuna muingiliano wa kimaisha lazima uwepo.
Haohao Saudi ilibidi wapindishe sheria ili Ronaldo aweze kuishi na mwanamke ambaye hawana ndoa.
Nchi kama England wamewapa nafasi watu weusi kuingia kwenye jamii yao ndiyo maana ni nchi iliyopiga hatua kisoka. Wanachukua talents zote kwenye timu ya taifa bila ubaguzi wa rangi.
Soka ni maisha, kukiwa na dosari yoyote kwenye ligi: uvunjifu wa haki za binadamu, ubaguzi wa rangi n.k. inapunguza nafasi ya wachezaji wengi kwenda huko.
Mfano kama Italy ingekuwa siyo ligi bora Europe wachezaji wengi weusi wasingeenda.
Ili Saudi wafike levels za ligi kama England kuna vitu watapaswa kufanya na hawataweza.