Waarabu wangepewa uwezo wa maarifa na silaha kama Mataifa ya Magharibi Dunia ingekuwaje?

Waarabu wangepewa uwezo wa maarifa na silaha kama Mataifa ya Magharibi Dunia ingekuwaje?

Shetani haaminiki wameanza kuua watu upya hawa laanatullah, kumbe ilikua janja janja watoe mateka wao. Siku zote kafiri hana mkataba
Wewe kumbe ulikuwa hujui? Subiri sasa muone cha moto!!
 
WATUMWA WA WAARABU NA WAZUNGU MKIWATETEA MABWANA ZENU. Hivi muafrika unapata wapi muda wa kuwatetea hao watu?.

Anyway hao waarabu Nguvu na maarifa wanayo sana, isipokuwa wamefanyiwa ujanja na mzungu kwa kutawaliwa na kugawanywa kwa itikadi za kibaguzi zinazotokana na migongano ya kidini na upuuzi wa chuki wao kwa wao.

Alafu hao wazungu hawana maarifa acheni utoto dunia ya sasa kila kitu kiko wazi someni, America&Ulaya zimejengwa kwa nguvu/maarifa ya watu weusi kutoka Afrika na baadhi ya waAsia hasa wahindi,China, Pakistan, mpaka hao wairan na waarabu.

Nguvu ya mzungu ipo ktk propaganda tu, hivi ukiachana na utumwa walioufanya waarabu kuna ubaya gani mwingine walioufanya leo hii ukilinganisha na ushenzi anaoendelea kuufanya mzungu?.

Zunguka dunia nzima kila mgogoro/vita kuna mkono wa mzungu na sio mwarabu, ukiona mwarabu kahusika basi ujue ni wale wale puppets wa mzungu ambao wanafanya kazi mbele ya kivuli cha mzungu.

Migogoro yote Afrika imeletwa na mzungu na inachochewa na wazungu, kama Waarabu wangeungana na kuacha tofauti zao basi kusingekuwa na ukatili hapo Middle East unaofanywa na taifa la kishetani lililotumia history ya uongo kujipa utakatifu kwa malengo yake ya kisiasa.

Pia kungekuwa na balance of power na kuheshimiana kama vile ilivyo taifa la China na Russia hawa hawagusiki hovyo.

Mambo ya siasa za dunia huwezi kuyaelewa mpaka uweke kando mahaba&chuki zako kwa upande usioupenda.
 
"Kubadilisha Dini za watu kwa lazima" ni kauli ya kipropaganda. Uislam ulienea kwa Amani katika hizo Nchi baada ya Majeshi ya Kiislam kuwashinda katika vita dola zilizokuwa zikitawala hapo. Watu wenyewe walikuwa wakisilimu kwa wingi bila kulazimishwa. Na ndio maana katika madhehebu nyingi za kale zaidi za kikristo utazikuta sana nchi hizo zilizotawaliwa na Makhalifa wa Kiislam. Zile jamii za kale zaidi za kikristo zilizobaki utazikuta pale. Na ajabu ukisoma Historia utaona wakristo wa hizo Nchi walikuwa wakiwapokea Waislam na kushirikiana nao dhidi ya "ndugu" zao wa Byzantine. Mfano wa Koptiki wa Misr waliwapokea Waislam dhidi ya Byzantines na wakawaunga mkono kwa sababu walichoshwa na dhulma za ndugu zao.

Cha kushangaza pia Jews waliishi kwa amani zaidi chini ya zile Dola za Kiislam kitu kilichokuwa kigumu mno walipokuwa chini ya wakristo. Actually kuna wasomi wa kiyahudi wanasema ni Uislam ndio uliokoa mayahudi.

Baadae Wakati wa Crusades wakristo wa Ulaya walikuwa wakiua Waislam, Jews na ndugu zao Wakristo wa Mashariki ya kati na wakitaka kuimpose Ukristo wao wa kiulaya. Ironically Crusaders walichangia kuanguka zaidi kwa Ukristo wa mashariki ya kati uliovumiliwa na Waislam hapo kabla.

Waislam walipowashinda Crusaders, Wakristo wa asili wa Middle East na Jews waliishi tena kwa Amani zaidi.

Wakristo na mayahudi katika nchi za mashariki ya kati japo walishakuwa minority (sio kwa sababu ya upanga wa Waislam) ila walikuja tena kupungua kwa kasi zaidi hivi karibuni tu hapo kwa sababu za kisiasa wakati ambapo Dola za kiislam zilikuwa zishaanza kuanguka na nguvu za Waislam zimeondoka na wakoloni wa Ulaya wanazitawala nchi nyingi za mashariki ya kati tayari, na wakati masekula na nationalists walipoanza kuibuka na zionists walipoingia mashariki ya kati (Palestine kuna wakristo wengi wamekimbia baada ya Nakba) na ukanda kuanza kutawaliwa na machafuko.

Najua unajua ni idadi kubwa sana ya wakristo wa kale kabisa wameikimbia Iraq baada ya nchi kuwaka moto walipopelekewa zawadi ya democracy na ndugu zao kutoka Marekani.

Sasa kwanini the oldest denominations za Wakristo zilisurvive na utazikuta katika hizo nchi? Why?

Waislam kuua watu milioni 70 huko Indian Subcontinent pia ni propaganda.

And again Kule Afghanistan na Bara Hindi Uislam ulienea kwa Amani. Baada ya Dola ya Waislam kuanza kuifungua baadhi ya ile miji baada ya kushinda katika vita, Uislamu ulianza kuenea gradually kwa Amani kupitia biashara na interactions nyengine za kijamii na kiuchumi na sio kwa sababu ya upanga. Dola tofauti tofauti za Kiislam katika Bara Hindi zilipoendelea kuibuka na zilipokuwa zikishinda vita. Uislam uliendelea kukua kwa Amani taratibu taratibu na ndio maana utakuta kiwango cha conversion hakikuwa kikubwa kwenye heartland ya zile Empires za Kiislam kama Delhi Sultanate au Mughal Empire bali conversion ilikuwa kubwa mno ukingoni huko kama Bengal au Punjab magharibi ambapo tawala za Kiislam maeneo hayo zilikuja kuanzishwa baadae huko baada ya Uislam kuenea huko.

Uislam ulienea sana kwa Amani huko Bara Hindi, tena taratibu.

Huwezi kufananisha conquests za Waislam hasa Rashidun Conquests na conquests za watu wengine wowote wale wasiokuwa wao. Wewe cheki Jerusalem inachukuliwa na Waislam, transfer inafanyika kwa Amani kabisa. Wakristo wanahakikishiwa usalama wao, wa mali zao na sehemu zao za ibada. Mayahudi waliokuwa hawaruhusiwi hata kuingia Jerusalem na Byzantines wakaruhusiwa na Waislam kuingia na kuishi Jerusalem. Kumbuka hiyo ni karne ya 7 Miladia na tayari Waislam wana strict Rules of War ambazo huwezi kuzilinganisha na jamii yoyote kwa standards za wakati huo na hata sasa.

Ukatili ukitaka kuujua vizuri waulizie warumi, waajemi wa zamani (kabla ya Uislam), mongols na crusaders kama mfano tu. Utauona ule ukatili wenyewe kabisa.

Uislam ulienea kwa Amani. Na Uislam huwa unaenea zaidi katika Amani na utulivu. Watu wametulia na wakapata fursa wakausikia Uislam watauelewa kwa urahisi tu kwa sababu ni Dini inayoendana na ya maumbile yao, na mwisho utaenea tu miongoni mwao, haraka au taratibu.
Nini kiliwakuta wakristo ambao walikuwa ni majority kule middle east? Walipotelea wapi kama uvamizi wa kiislam ulikuwa wa amani sana? Coptic Christians walikuwa majority pale Misri,leo na less than 10%.

Wahindu na wabudha kule India subcontinent ndiyo ilikuwa balaa. Uislamu hauwatambui kama watu wa kitabu,wao walipewa option mbili tu (convert or die).

Wanawake wa kihindu walikuwa wanafanya kitu kinaitwa (Johar) ,wanajiua na watoto wao ili wasilazimishwe kuingia kwenye dini mpya.
 
Attachments

Hii nilishajibu kama umesoma vizuri hiyo comment yangu uliyoi quote.

Hii ni propaganda na oversimplification. Na nishaijibu pia. Uislam ulienea taratibu katika Bara Hindi kwa Amani na bila kulazimishwa.

Na kengine cha kuongezea pia kwakuwa kulikuwa na ubaguzi dhidi ma Buddha na wahindu wa madaraja ya chini (lower caste, kumbuka wahindu wana madaraja ya kijamii ambapo watu wanagawanywa kwa madaraja tena wanarithi hayo madaraja yaani mtu akizaliwa tu katika caste fulani ndio yuko humo maisha yake yote na hawawezi kubadilisha na wanabaguliwa kwa madaraja hayo hata katika ndoa wanaoana kwa caste). Waislam walipokuja maBuddha wengi na Wahindu wa caste za chini waliwapokea Waislam na majeshi yao. Na Uislam ukaenea taratibu kwa njia za Amani.

Na Jauhar ilikuwa ni katika mila za kihindu ambapo wanawake wa kihindu wa Rajput kshatriya walijichoma moto na watoto wao pale walipoelekea kushindwa vita. Kshatriya ni caste ya kihindu ya mashujaa wa vita na watawala na ni katika caste za juu. Rajput ni koo ndani ya Kshatriya caste. Sasa wanawake wa kihindu wa Rajput kshatriya walikuwa na mila ya kujichoma moto wao na watoto wao pale walipokuwa wakielekea kushindwa katika vita ili wasiingie kwenye mikono ya adui. Jauhar ina uhusiano na mila nyengine ya kihindu inaitwa Sati ambapo mjane alijichoma moto pamoja na mwili wa mumewe.

So Jauhar haikufanywa kwa sababu eti Waislam waliwavamia ndio wakaanza kufanya hivyo au walilazimishwa kuufuata Uislam ndio maana wakafanya. Hiyo Jauhar waliifanya ni mila yao na ilifanywa na wanawake wa Rajput kshatriya (jamii katika caste ya watawala na mashujaa wa vita) na walifanya hivyo walipokuwa wanaelekea kushindwa vita hata walipokuwa wakipigana wahindu wenyewe kwa wenyewe.

Imefanya nimekumbuka mila ya Seppuku huko Japan.

Seppuku ilifanywa ni mila huko Japan ambapo shujaa wa vita alijiua kwa mtindo fulani ili kulinda heshima yake, mashujaa wa kivita kwao kuliko wasalimu amri kwa adui walifanya Seppuku. Zamani ilikuwa ikifanywa na Samurai.

Na wakati mwengine Seppuku iliweza kufanywa kama adhabu ya kifo pale ambapo Samurai alifanya makosa makubwa kama ubakaji, uhaini na makosa mengine ambayo kwao yalistahiki kifo, Samurai (shujaa wa kivita zamani wa Japan) alilazimishwa kufanya Seppuku kama adhabu kwake.

Na wake za samurai au wanawake wa familia za daraja/class ya Samurai pia walikuwa na ritual suicide (jigai/jisatsu); pale Samurai (mumewe) akifanya Seppuku, au pale mwanamke wa class ya Samurai anapoharibu heshima ya familia alifanya jigai/jisatsu ku prevent dishonor kwa familia., au pale ambapo adui amevamia na wanashindwa, walifanya jigai/jisatsu ili kuzuia wasiingie katika mikono ya adui.

Ni mila potofu tu walizokuwa nazo
 
I agree

I agree to disagree chief,ukiwa muislam lazima uone Islamic conquest in positive note. Bahati mbaya wahanga wa Islamic conquest wana maoni tofauti.

Pale Jerusalem caliph Al-Hakim bi-Amr Allah wa Fatimid caliphate alitoa amri kabisa takatifu la waroma livunjwe mwaka 1009. Kule Uturuki Hagia Sofia ambalo ni kanisa la kale sana wa waroma limegeuzwa msikiti. Kama modern times tu waturuki wanataifisha kabisa je zamani ilikuwaje?
 
Back
Top Bottom