Waarabu wangepewa uwezo wa maarifa na silaha kama Mataifa ya Magharibi Dunia ingekuwaje?

Shetani haaminiki wameanza kuua watu upya hawa laanatullah, kumbe ilikua janja janja watoe mateka wao. Siku zote kafiri hana mkataba
Wewe kumbe ulikuwa hujui? Subiri sasa muone cha moto!!
 
WATUMWA WA WAARABU NA WAZUNGU MKIWATETEA MABWANA ZENU. Hivi muafrika unapata wapi muda wa kuwatetea hao watu?.

Anyway hao waarabu Nguvu na maarifa wanayo sana, isipokuwa wamefanyiwa ujanja na mzungu kwa kutawaliwa na kugawanywa kwa itikadi za kibaguzi zinazotokana na migongano ya kidini na upuuzi wa chuki wao kwa wao.

Alafu hao wazungu hawana maarifa acheni utoto dunia ya sasa kila kitu kiko wazi someni, America&Ulaya zimejengwa kwa nguvu/maarifa ya watu weusi kutoka Afrika na baadhi ya waAsia hasa wahindi,China, Pakistan, mpaka hao wairan na waarabu.

Nguvu ya mzungu ipo ktk propaganda tu, hivi ukiachana na utumwa walioufanya waarabu kuna ubaya gani mwingine walioufanya leo hii ukilinganisha na ushenzi anaoendelea kuufanya mzungu?.

Zunguka dunia nzima kila mgogoro/vita kuna mkono wa mzungu na sio mwarabu, ukiona mwarabu kahusika basi ujue ni wale wale puppets wa mzungu ambao wanafanya kazi mbele ya kivuli cha mzungu.

Migogoro yote Afrika imeletwa na mzungu na inachochewa na wazungu, kama Waarabu wangeungana na kuacha tofauti zao basi kusingekuwa na ukatili hapo Middle East unaofanywa na taifa la kishetani lililotumia history ya uongo kujipa utakatifu kwa malengo yake ya kisiasa.

Pia kungekuwa na balance of power na kuheshimiana kama vile ilivyo taifa la China na Russia hawa hawagusiki hovyo.

Mambo ya siasa za dunia huwezi kuyaelewa mpaka uweke kando mahaba&chuki zako kwa upande usioupenda.
 
Nini kiliwakuta wakristo ambao walikuwa ni majority kule middle east? Walipotelea wapi kama uvamizi wa kiislam ulikuwa wa amani sana? Coptic Christians walikuwa majority pale Misri,leo na less than 10%.

Wahindu na wabudha kule India subcontinent ndiyo ilikuwa balaa. Uislamu hauwatambui kama watu wa kitabu,wao walipewa option mbili tu (convert or die).

Wanawake wa kihindu walikuwa wanafanya kitu kinaitwa (Johar) ,wanajiua na watoto wao ili wasilazimishwe kuingia kwenye dini mpya.
 

Attachments

Nini kiliwakuta wakristo ambao walikuwa ni majority kule middle east? Walipotelea wapi kama uvamizi wa kiislam ulikuwa wa amani sana? Coptic Christians walikuwa majority pale Misri,leo na less than 10%.

Hii nilishajibu kama umesoma vizuri hiyo comment yangu uliyoi quote.



Hii ni propaganda na oversimplification. Na nishaijibu pia. Uislam ulienea taratibu katika Bara Hindi kwa Amani na bila kulazimishwa.

Na kengine cha kuongezea pia kwakuwa kulikuwa na ubaguzi dhidi ma Buddha na wahindu wa madaraja ya chini (lower caste, kumbuka wahindu wana madaraja ya kijamii ambapo watu wanagawanywa kwa madaraja tena wanarithi hayo madaraja yaani mtu akizaliwa tu katika caste fulani ndio yuko humo maisha yake yote na hawawezi kubadilisha na wanabaguliwa kwa madaraja hayo hata katika ndoa wanaoana kwa caste). Waislam walipokuja maBuddha wengi na Wahindu wa caste za chini waliwapokea Waislam na majeshi yao. Na Uislam ukaenea taratibu kwa njia za Amani.

Na Jauhar ilikuwa ni katika mila za kihindu ambapo wanawake wa kihindu wa Rajput kshatriya walijichoma moto na watoto wao pale walipoelekea kushindwa vita. Kshatriya ni caste ya kihindu ya mashujaa wa vita na watawala na ni katika caste za juu. Rajput ni koo ndani ya Kshatriya caste. Sasa wanawake wa kihindu wa Rajput kshatriya walikuwa na mila ya kujichoma moto wao na watoto wao pale walipokuwa wakielekea kushindwa katika vita ili wasiingie kwenye mikono ya adui. Jauhar ina uhusiano na mila nyengine ya kihindu inaitwa Sati ambapo mjane alijichoma moto pamoja na mwili wa mumewe.

So Jauhar haikufanywa kwa sababu eti Waislam waliwavamia ndio wakaanza kufanya hivyo au walilazimishwa kuufuata Uislam ndio maana wakafanya. Hiyo Jauhar waliifanya ni mila yao na ilifanywa na wanawake wa Rajput kshatriya (jamii katika caste ya watawala na mashujaa wa vita) na walifanya hivyo walipokuwa wanaelekea kushindwa vita hata walipokuwa wakipigana wahindu wenyewe kwa wenyewe.


Imefanya nimekumbuka mila ya Seppuku huko Japan.

Seppuku ilifanywa ni mila huko Japan ambapo shujaa wa vita alijiua kwa mtindo fulani ili kulinda heshima yake, mashujaa wa kivita kwao kuliko wasalimu amri kwa adui walifanya Seppuku. Zamani ilikuwa ikifanywa na Samurai.

Na wakati mwengine Seppuku iliweza kufanywa kama adhabu ya kifo pale ambapo Samurai alifanya makosa makubwa kama ubakaji, uhaini na makosa mengine ambayo kwao yalistahiki kifo, Samurai (shujaa wa kivita zamani wa Japan) alilazimishwa kufanya Seppuku kama adhabu kwake.

Na wake za samurai au wanawake wa familia za daraja/class ya Samurai pia walikuwa na ritual suicide (jigai/jisatsu); pale Samurai (mumewe) akifanya Seppuku, au pale mwanamke wa class ya Samurai anapoharibu heshima ya familia alifanya jigai/jisatsu ku prevent dishonor kwa familia., au pale ambapo adui amevamia na wanashindwa, walifanya jigai/jisatsu ili kuzuia wasiingie katika mikono ya adui.

Ni mila potofu tu walizokuwa nazo
 
I agree
I agree to disagree chief,ukiwa muislam lazima uone Islamic conquest in positive note. Bahati mbaya wahanga wa Islamic conquest wana maoni tofauti.

Pale Jerusalem caliph Al-Hakim bi-Amr Allah wa Fatimid caliphate alitoa amri kabisa takatifu la waroma livunjwe mwaka 1009. Kule Uturuki Hagia Sofia ambalo ni kanisa la kale sana wa waroma limegeuzwa msikiti. Kama modern times tu waturuki wanataifisha kabisa je zamani ilikuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…