Waarabu Zanzibar na Watutsi maziwa makuu wote walikuwa walowezi wakoloni

Waarabu Zanzibar na Watutsi maziwa makuu wote walikuwa walowezi wakoloni

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,940
Reaction score
7,849
Ukoloni Zanzibar haukuanzia kwa waingereza bali kwa walowezi waarabu wa Omani ambao walihamia zanzibar pamoja na ndugu ya sultani wao ambapo walimuweka akawa sultani wa zanzibar na kuanzisha utawala wa ukoloni wa kilowezi wa kiarabu.

Waomani hao wakatawala eneo la zanzibar na pwani ya afrika mashariki huku wakiwabagua waafrika wenye nchi yao na wakiwashirikisha baadhi ya machotara wa kiarabu kwenye utawala. Shughuli kubwa ilikua ni biashara hususan ya watumwa.

Kwa upande wa watutsi wao ni waafrika wa mbari ya kihima na kwa asili ni wafugaji hadi leo wa kuhamahama. Asili yao walitokea kaskazini ya bara la Afrika nchi ambayo hivi leo ni Ethiopia hususan eneo la Oromo. Katika hali ya kuhamahama na mifugo yao kutafuta malisho hatimae kiasi cha karne nne zilizopita walijikuta Afrka ya mashariki maeneo ya maziwa makuu ambapo wenyeji wake walikua ni wa mbari ya kibantu.

Tofauti na wabantu watutsi wengi wao wana umbo la urefu wembamba na wenye sura ya upanga. Ni watu hodari wa vita vya kutumia mikuki na wanapenda sana ukuu hususan madaraka ya utawala. Popote walipopita eneo la maziwa makuu walipokonya madaraka ya jadi toka kwa wenyeji kwa nguvu au kwa kutumia hila na kuweka viongozi wa mbari yao ya kihima wakiitwa watemi.

Wao kama waarabu pia walikua wakoloni walowezi kwa sababu walihodhi madaraka na uchumi na walibagua watu wa mbari ya kibantu waliyowakuta wakiendesha tawala zao za kijadi.

Waingereza walipokuja zanzibar kuweka ukoloni wao waliingia mkataba wa kulinda utawala wa sultani na kushirikiana nae kutawala zanzibar.

Huko Rwanda na Burundi wabeljiji walipokuja kuweka ukoloni wao walikuta nchi hizo zinatawaliwa na falme za kitutsi ambapo wahutu wa mbari ya kibantu wakiwa sawa na watumwa kwa jinsi walivyokua hawana nguvu ya kiutawala.

Wale walikwenda shule kwenye ile miaka ya mwanzo baada ya tanganyika kupa uhuru watakumbuka kusomo katika historia somo la tawala za wahima tanganyika. Nyerere alikua na hekima sana kuzima kiu ya watawala wa kihima magharibi ya Tanganyika wasiweze kukwamisha juhudi za kupata uhuru.
Kama ilivyokua kwa sehemu zote afrika kulikokua na tawala za kilowezi shida ilitokea pale wakoloni wa kizungu walipokua tayari kuzipa nchi za kiafrika uhuru.

Walowezi waliyokua wameweka tawala za wachache waligombea wao kupewa uhuru wa nchi chini ya uongozi wao ambapo raia waliyo wengi walitaka kukomeshwa tawala za walowezi wachache.

Kule Afrika kusini tuliona waingereza mwaka wa 1910 wakitoa uhuru kwa makaburu, mwaka wa 1963 wakatoa uhuru kwa utawala wa walowezi wachache wa kiarabu zanzibar, na mwaka wa 1965 wakatoa uhuru kwa walowezi wachache wazungu Rhodesia.

Kwa zanzibar mara baada ya uhuru kutolewa kwa walowezi wa kiaraba haikuchukua muda. Baada ya miezi michache kukatokea mapinduzi ya kumwaga damu mwanzoni mwa 1964 yaliyofanywa na waafrika wabantu waliyo wengi wakatwaa madaraka na kuunganika na Tanganyika na kua nchi moja.

Kwa upande wa tawala za kilowezi za watutsi kwa kua walikua ni waafrika weusi tatizo la ukoloni wao lilikua limejificha kwa ulimwengu. Kule Burundi Ubeljiji ilikabidhi uhuru kwa utawala wa walowezi watutsi mwaka wa 1960 na baada ya hapo hali ikawa sio ya amani hadi miaka kadhaa wahutu wabantu walio wengi walipoweza kuondoa utawala wa kibaguzi wa watutsi.

Nchini Rwanda hali ilikua tofauti kwa wabeljiji kwani walifanikiwa kuwazuia walowezi wa kitutsi kutwaa nchi wakati wa uhuru mwaka wa 1960 na kuhakikisha waliyo wengi ndio wanatwaa madaraka. Hata hivyo watutsi wameendelea kufanya machafuko eneo lote maziwa makuu wakiamini licha ya uchache wao nchi za maziwa makuu ni milki yao ya jadi.

Jitihada zao hizo zimezaa ukosefu mkubwa wa amani hususan nchini Rwanda Burundi na Congo ya mashariki ambapo leo baada ya milioni kadhaa ya watu kupoteza maisha watutsi wakiongozwa na Paul Kagame wamefanikiwa kuweka utawala wa mbari ya kitutsi Rwanda na sehemu za Congo ya mashariki ikiwemo miji ya Goma na Bukavu.

Mtu hahitaji kupata shida kuona kwamba nchi ya rwanda inaongozwa na watutsi wachache ambao idadi yao ni kama asilimia 14 tu ya raia milioni 12 wa nchi hiyo.

Kwa kumaliza ningesema kwamba sababu kubwa ya kuandika huu waraka sio kuleta utengamamo ila ni kuweka uelewa wa nini ndio misingi ya migogoro inayoendelea eneo la maziwa makuu.

Maelezo aina hii kuna hawapendi kusikia kwani uongo ndio msingi wa madai yao ya kisiasa. Lakini uelewa kwa hakika ndio msingi wa kumaliza shida na tofauti zilizopo.
 
Unataka Watutsi warudi Ethiopia au
kama watutsi kubaki maeneo maziwa makuu wanadai lazima wao kutawala kama wanavyotawala rwanda itabidi warudi ethiopia ili maziwa makuu tupate amani. Huko watu wote wana pua refu kama watutsi. Si umeona zanzibar wale waarabu wasiokubali kuona walio wengi wanaongoza, au tuseme wasiotaka demokrasia ya wengi walirudi Oman na uarabuni.
 
Hapo ni pagumu sana washachanyikana sana na Wahaya sijui wanyambo ni ngumu sana Wanzibar wameanza kuwa na kiburi kuna sababu subiri awamu hiii ipite
 
Back
Top Bottom