Waasi wa M23 Wamedhibiti mji wa Bunagana uliopo Mpakani mwa DRC na Rwanda

Kumbe unajua kuwa siraha za kisasa sio ishu Sana kwenye war, japo zinamsaada wake pia.
Unanikumbusa Vietnam war marekani walivyokuwa wanapitisha ndege zao za kivita angani hata kuhesabu unashidwa ila kiliwapata nn, waliondoka wenyewe.
 
T14 Armata

Mkuu Dunia mzima inajua kuwa technology inabadilika Sana na hata majeshi yote dunia hata la hapa kwetu wanajua Hilo kuwa hizi siraha zimepita na wakati tunahitaji zingine , wanajua Sana so Hakuna jeshi dunia lililokaa tuu na mabadiliko haya na dunia ya Sasa .
 
Kama ningekuwa Rais wa Tanzania basi bila kuchelewa ningeingia makubaliano na DRC hasa ya kibiashara, ikumbukwe DRC wanatumia Bandari yetu kwa kiasi kikubwa, hivyo kukosa amani maeneo hayo ni kutingisha uchumi wetu.

Ningepeleka kikosi si cha kulinda amani bali kuzichapa mazima na hao M23.

Wakati mwingine nchi huingilia nchi nyingine kwa maslahi mapana.

Rwanda hata awe vizuri vipi hawaiwezi Tanzania kwa kila kitu.

Ningeingia mazima kuwaondoa M23 afu mnakubaliana kwenye usafirishaji wa madini na bidhaa muhimu zipitie TZ
 
hahahaaaa mikataba bro , ukiona mtu katangazwa ujue kaingia makubaliano
 
M23 wanapigania haki gani? Kwamba Rwanda inawafadhili kwa kuwa wanaonewa sana nchini Congo
hao ni wakongo wanapigania haki zao kama wakongo , fuatilia acha kumezeshwa hz propaganda za kuwa wanapigania serikali ya Rwanda ( inaeza kuwa kweli ila tukimaliza primary cause then hiyo secondary cause hawatokuwa nayo )
 
Mkuu Tanzania hiyo Mig-29 haipo. Hakuna nchi inanunua ndege mbili au tatu zikiwa fighters, labda ziwe maritime patrol, EW, CIWS au transport. Ukinunua ndege chache gharama za servicing ni kubwa mno haileti maana, na kufungua support facilities ni vigumu.

Saddam kuangusha ndege za Marekani vitani sio ajabu, hakuna ndege Marekani inatengeneza ikisema haitowahi kudondoshwa dunia hii. Mbona hujasema B-52 ambazo zimeundwa mwanzoni mwa miaka ya 1950 ila bado zilishiriki kudondosha mabomu Iraq na bado ziko kazini hadi 2030s uko. Na pia kalinganishe ndege ngapi za Marekani zilikuwa shotdown na za Iraq uone tofauti kubwa. Wewe unataka vita iwe ya upande mmoja kwamba mmoja anapigwa na mwingine ni immortal
 
hao ni wakongo wanapigania haki zao kama wakongo , fuatilia acha kumezeshwa hz propaganda za kuwa wanapigania serikali ya Rwanda ( inaeza kuwa kweli ila tukimaliza primary cause then hiyo secondary cause hawatokuwa nayo )
Narudia tena, haki gani wanazopigania?
Huhitaji kuwa baridi moto kuitetea Rwanda kwenye hili, Rais wa Congo sio mwehu kwamba aanze tu kuishutumu Rwanda.

Huyu Rais ameingia juzi tu lakini kuna Reports za UN zinazothibitisha uhusika wa Rwanda kwenye wizi wa rasilimali za Congo, anza na ya 2002 inayoonesha namna jeshi la Rwanda(RPA) linavyoiba madini ya Congo, pia kuna report ya 2012 ya Baraza la Usalama imeelezea kwa kina wakiambanisha na ushahidi juu ya uhusika wa Rwanda sio tu kwenye ufadhili wa hili kundi (M23)ila pia hata kwenye uanzishwaji wake na kuna Report nyingine ya mwaka jana(2021).

Unaweza kusema hizo Reports za UN ni propaganda za mabeberu, nieleweshe hili tukio la Laurent Nkunda kushikiliwa Rwanda, Unaona ni tukio la kawaida?
 

Hakuna vita isiyokuwa na maslahi ya upande mmoja
Kagame amevuna sana Congo na bado wanamchekea Yaani hao wakongo 95m wameshindwa kuungana wakatetea ardhi yao
Lakini mwizi mkubwa hapo ni Mfaransa huyu hata Algeria wamemshindwa ni jambazi linalotumia njia nyingi kwa kuwafadhili waasi na hata wenyewe kwa wenyewe

France hakuanza leo kuiibia africa na raslimali zetu
 
Great ..na ndivyo inakuja kuwa
 
Wafaransa ni tatizo, hawa wamegoma kabisa kuyaacha makoloni yao yawe na uhuru wa kweli.
 
Sasa hizo rasimali Kama zinaweza kuifaidisha Rwanda zinashindwaje kuifanya Congo ikawa tajiri?
 
Naona huyu yupo JF kupoteza muda kwa kubisha bisha..hajui hata anachozungumza..mpuuze..ukisoma hoja zake utajua anatakiwa akasome kwanza
 
Cha kusikitisha

UN wako kimya,
EU wako kimya,
NATO wako kimya[emoji848]
Ukraine wako kimya[emoji848]
USA wako kimya[emoji848]
UK wako kimya[emoji848]
Na Urusi pia kimyaaaa. Yani Kagame anaogopwa.
 
Sasa hizo rasimali Kama zinaweza kuifaidisha Rwanda zinashindwaje kuifanya Congo ikawa tajiri?

Mkuu Ndio maana unaona machafuko hayaishi
Wanachonganishwa na France yuko nyuma mali zinaenda Paris Mkuu

Siku wakijielewa wataungana na kuzuia mali zao ili ziwafaidishe na wao
Dunia hii
Magogo yanamalizwa kwenda Ulaya na sasa China
Angalia YouTube wanavyosomba mali

Hawa France hawajui mwisho wao wamejimilikisha tangu 1800 nchi nyingi na mpaka leo wanavuna taratibu

Hawawezi kuifanya Congo tajiri kwa sababu ya ujinga wao na kukubali kuchonganishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…