Moronight walker
JF-Expert Member
- Aug 3, 2021
- 3,103
- 4,704
Kumbe unajua kuwa siraha za kisasa sio ishu Sana kwenye war, japo zinamsaada wake pia.Huo sio unafiki, sheria zao zinawataka ufanye disclosure ya mteja wa silaha unayemuuzia na wanajadiliana kama anastahili kuuziwa. Ndio maana deals nyingine wanakataa, Kenya ilikataliwa kununua helikopta kipindi cha Obama ila Trump akakubali baada ya sababu ya kupambana na Al Shabaab kuonekana nzito.
Na kila anayeenda kununua anajua kwamba atatajwa, vigezo na masharti kuzingatiwa kama hutaki nunua uko mafichoni. Alafu unadhani ukijua nchi fulani inamiliki silaha fulani ndio guarantee ya kushinda vita. Vita mnaanza mkijua almost silaha zote za adui ila kama mlikuwa wa kupigwa mtapigwa tu. Na kama huna uchumi hata ukijua Saudi Arabia kanunua silaha za $30 billion utatoa wapi hela kununua kama yeye
Unanikumbusa Vietnam war marekani walivyokuwa wanapitisha ndege zao za kivita angani hata kuhesabu unashidwa ila kiliwapata nn, waliondoka wenyewe.