Wabantu tumehamia Tanzania. Ikitokea watu fulani wakija wakasema tuwapishe Tanzania ni ardhi ya babu zao tutakubali?

Wewe unaeneza Misconception kila siku ukirekebishwa bado unaongea uongo ule ule. Hamas ndio ni waisilamu ila ni chama cha Gaza tena hapo Gaza kwenyewe kuna Vyama vingine, Palestina kuna vyama vingi mno kama Chama cha Secular kinaitwa Fatah cha Yasir Arafat ambacho kwa muda kinaongoza Nchi, Kuna Chama cha Wakristo PFLP kuna movement kibao ndani ya Palestina na sio Ugomvi wa Dini kama propaganda za Israel na chawa wao wanavyotuaminisha.

Hao Hamas wenyewe walianzishwa na wa israel kama Division ya wapalestina ili wapambane na Yasir Arafat.

Palestina inadai Nchi yao na sio dini, wanataka ardhi yao waliopokonywa wote waisilamu, Wakristo, wayahudi wanapigana na hio state.
 
Wapalestina wa sasa ndio hao hao walio kuwepo miaka 2000 ama 10000 ama 20,000 iliopita, tafiti kibao za sayansi zinathibitisha hili, kihistoria hakuna eneo Wa israel walikata ambalo halikua na waarabu.
 
Inategemea hilo kundi mfano Wangoni wamekuja Tanzania miaka ya 1800 wakati Prince wa Iran alikuja Kusini (Kilwa) miaka ya 1200 Takriban miaka 600 kabla ya Wangoni.

Leo Wa Iran waki claim hilo eneo je utakubali?
Wote n wa kuja tu
 
Hilo haliwezi kutokea maana jambo hili ni kwa ajili ya Taifa teule na nchi takatifu tu. Kwa hiyo hakuna haja ya kuumiza kichwa.
 
Wapalestina wa sasa ndio hao hao walio kuwepo miaka 2000 ama 10000 ama 20,000 iliopita, tafiti kibao za sayansi zinathibitisha hili, kihistoria hakuna eneo Wa israel walikata ambalo halikua na waarabu.
Wapalestina ni niniiii. Tafiti za ma - manipulators hao.
Kabla ya Waromi hawajatunga ilo jina palestine walikuwa wakitumia jina gani?.
Ikiwa hata jina tu si lao ni vipi Ardhi iwe yao?.
 
Na ww utajiuliza kwann hao watu wachague Tanzania tu kati ya nchi zote duniani?
 

ambacho hujui kabla ya 1947 hamna nchi ilikua inaitwa palestina wala watu wanaojiita wapalestina!!….
eneo la ardhi lilikua linaitwa palestine mandate ….. Lilitawakua chini ya Britain

Waisrael walikuepo na waarabu walikuepo ( siyo wapalestina)…..
Kuondoa mgogoro britishi ikagawa eneo sehemu mbili moja kwa ajili ya jews (hawataki kuchanganyika) na kwa ajili ya waarabu ndo wakajiita palestina lakin ni waarabu waliotoka Saudi arabia, misri, lebanone na Jordan…
 

🀣🀣
 
Wapalestina ni niniiii. Tafiti za ma - manipulators hao.
Kabla ya Waromi hawajatunga ilo jina palestine walikuwa wakitumia jina gani?.
Ikiwa hata jina tu si lao ni vipi Ardhi iwe yao?.
Hata Tanzania imeitwa Majina mengi, jina halina uzito wowote ule, Sababu Hapa kumebadilishwa toka Tanganyika kuja Tanzania basi ina maana watu wamekosa uhalali wa kuwa Watanzania?

Pia huzijui hizo tafiti, zijaziweka lakini tayari una jibu hizo tafiti zimekuwa manipulated, ina maana una majibu tayari ya kitu usichokijua.
 
Propaganda


Kama hakukua na Palestina hizi hela za 1927 na miaka ya 1930s zilitoka wapi?



Sababu Taifa lilitawaliwa na Taifa jengine haimaanishi hilo taifa haliku exist kabla, kwenye Tawala zote kuanzia Ummayid, Abbasid, Ottoman hadi British palestina Ipo.

Ukinitajia mwaka wowote unaotaka wewe nakutajia kiongozi wa Palestina alikua nani, watu wana Historia zao zenye ushahidi kabisa.
 
Jina halina nguvu ilhali hapa unatumia jina kama utambulisho wao!kwani Usitumie namna nyingine tu ya kuwa- describe na si kutumia jina?.
Turudi kuleee.
Upepo uliowaleta Waarabu wa Misri, Morocco, Sudan, Tunisia ndiyo upepo ule ule ndiyo uliopeleka hao wanaoijiita wapalestina.
Sasa imekuwaje hawa Waarabu wa Africa wabaki kuwa Waarabu ila Waarabu walioelekea Israel wabadilike kuwa Waisrael?.
Mfn:-
Meri mbili za watumwa zitweke toka Africa moja Iende Spain nyingine Iende ujerumani After certain decades useme walioelekea ujerumani wanavinasaba vya kejerumani ila walioenda Spain wamebaki kuwa waafrika. Uoni kuwa ni zaidi ya kujipinga kimantiki.
Ikiwa hao waarabu wanaojiita wapalestina ni waisrael basi hata akina Mo Sarah ni waisrael maana Asili ni moja.
 
Misri Morocco na Algeria si waarabu lakini wameitwa waarabu karibuni sababu wanaongea kiarabu, definition ya sasa ya Muarabu kaiweka Muingereza. Same kwa Palestina wanaitwa waarabu sababu tu wana Mila na wanaongea kiarabu. So hio hoja yako haimake sense yoyote hawa watu wameitwa waarabu hivi karibuni ila wana identity zao kabla ya kuitwa waarabu.

Kuna Copts Egpty ni Identity yao ila sasa wanaitwa waarabu, kuna Berbers na amazigh people Libya, Algeria na Morocco ila sasa wanaitwa waarabu,

Kwa Upande wa huo ukanda hao ni Levant, hio ni ancient civilization kuanzia zama za kawe historia yao inajulikana, unaongelea moja ya Civilization za kwanza kabisa duniani.


Kama lengo lako ni kuelewa Soma asili ya Levant hapo. Baada ya Empire za Kiisilamu kusambaa pia Wakawa na cultural ya kiarabu na baadae kuitwa waarabu ila kiasili sio waarabu kama zilivyo nchi nyengine kama Sudan, Morocco, Libya, Egpty etc.
 
Usiniletee link, andika ulichokielewa kwenye hiyo link.
However hakuna Kinachoonyesha kuwa hao wanajiita wapalestina ni waisrael.
 
Wakija na kitabu kitakatifu tutapigana kama Israel na Palestine.
 
Wakija na kitabu kitakatifu tutapigana kama Israel na Palestine.

Kigezo gani utatumia kugundua kitabu chao ni kitikatifu.

Wakituambia kwa mdomo kama ni kitakatifu kama wakoloni walivyotupatia biblia na Quran kisha wao wakabeba dhahabu zetu na kuwasainisha kina chifu mangungo mikataba huku hawajui kusoma wala kuandika.

Je tutakubali ?
 
Haiwezekani , πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€, waPalestina wasikubali kabisa!!!
 
Hatutoki ng'o.
 
Labda Warangi, hao wengine sijui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…