Wabara ondoeni shaka, ardhi ya SMZ Bagamoyo si sehemu ya Zanzibar. SMZ haina hati; limetelekezwa miaka 45 ila Zanzibar inamiliki kihalali

Ardhi sio issue ya muungano, Zanzibar ina Ardhi yake na Tanzania bara ina Ardhi yake.
P
Maana yake wazanzibar wana ardhi yao na watanganyika wana ardhi yao. Na mmoja akienda kwingine kumiliki ardhi anakuwa kama muwekezaji wa kigeni, siyo? Maana unaposema nchi/Serikali unazungumzia wananchi wa nchi hizo.
 
Acha bla bla mheshimiwa Paskali.
Huwezi miliki ardhi kwenye nchi ya jirani.
Full Stop!
 
afadhali kuna watu kama nyinyi munaosoma historia na kueleza kisawasawa, hawa wengine ni kupiga kelele bila ya kufanya reference ya mambo yaliyopita. Na hasa hao waliotoka mabara ya Tanganyika ndiyo wanajifanya nchi hii ni yao bila ya kuijua historia yake.

Ila hiyo ya kulitelekeza kwa miaka 45 siyo kweli kwani kwa kumbukumbu zangu kulikuwa na wafanyakazi wa ranchi mpaka kwenye miaka ya tisini, walikuwa wanahamishwa Zanzibar na kupelekwa Bagamoyo. Miaka ile ilikuwa ukipelekwa Bagamoyo ni kama ulikuwa unapelekwa Kigoma kikazi.
 
Hata mjengo wa Ikulu ya Magogoni, imejengwa na Sultan of Zanzibar,
Mbona hapa Mayala inaelekea kama umesema uwongo. Tunavyojua ni kwamba ikulu ya Magogoni ilijengwa na waingereza mwaka 1919 chini ya usimamizi wa Gavana Horace Byatt. Hata jiwe la msingi lililopo hapo Magogoni limeandikwa jina hilo la Horace Byatt.

 
Eneo walilopewa ni ekari 6000, Zanzibar walishindwa kulitumia hata robo, likabaki kuwa pori tuu!. Hata serikali yetu ilipoamua kulimega kuwapa wawekezaji, serikali iliwaarifu SMZ, hawakuonyesha pingamizi yoyote, hivyo kuhesabiwa they are not interested. Hiyo Ranchi ya Makurunge imetumia kama 1/10 ya eneo!. Hekari 6,000 is huge!, eneo hilo ni theluthi ya Zanzibar!.
P
 
PM.
Umedurusu historia kwa kiasi chako ulichoweza.

My take:-

1. Hatuwezi kamwe kuegemea historia ya aliyoyafanya Sultani kwa kuwa kabla ya kuja Sultani EA tulikuwa na historia yetu.

2. Kuacha historia yetu na kuipa adhama historia ya Sultani ni kuthibitisha kwamba bado tuko kwenye utumwa wa Kiarabu na kwamba Mapinduzi siyo matukufu bali ni Mapinduzi-dhambi yaliyofanya dhambi kumpindua Sultani, hivyo Waznz wote 1.8 ml wanastahili kushitakiwa na kunyongwa kwa kufanya uhaini dhidi ya utawala halali (unaodumu) wa Sultani Jamshid.

3. Uhalali wa Sultani unatokana na fikra ulizowasilisha za kumuenzi Jahili Sultani ila uko sahihi kidogo kutokana na kwamba Znz imeendelea kuenzi ustaarabu wake ikiwemo dini aliyoleta Znz (Znz haina utamaduni wa kitaifa wa Kiznz, inahitaji Mapinduzi ya pili ya kitamaduni kama walivyofanya Wachina, Wagiriki, Warumi (waliokuwa chini ya Mesopotamia pia), Wamarekani, Wafaransa, Warusi, Wajapani, Wajerumani, Wareno na Wayahudi)

4. No.3 hapo juu inathibitisha kwamba Znz ilipindua tu serikali ya Sultani lakini haikupindua tunu, mila na desturi za Sultani alizopandikiza Znz. Hii inafanya Mapinduzi kutokuwa matukufu na yanapoteza dhima yake pia kwa kutengeneza Masultani uchwara (Masultani mbadala) wa Kiznz ambao kinyume na Masultani Majid Bin Said na Jamshid Bin Abdullah waliojenga Znz; wao Masultani uchwara hawa wanabomoa Znz na kuhamishia milki Oman na pia kumrejeshea kinyemela visiwa 52 nk kwa jina la wawekezaji. Yaani walimpindua Jamshid na sasa wanamrejeshea milki zake Oman na humu humu Znz. Duh! Maskini Field Marshal John Okello bora Nyerere alikunyima kuishi Tz maana haya yangekuumiza mtima wako.

"I found city of Rome in bricks and left it in carrara marble Augustus Caesar 27 BC"

5. Mapinduzi ya Znz na Uhuru wa Tanganyika vinafuta mipaka dhalimu ya Kisultani iliyowekwa kati ya Znz na Tanganyika na Sultani Majid Bin Said na kuendelezwa na Sultani Jamshid Bin Abdullah. Hii inachagiza suala la Makurunge RAZABA kutazamwa upya.

6. Nadhani hatupaswi na hatulazimiki kuendelea kuwa Watumwa wa Utumwa.

Sitaki kuamini tulikulupuka kumpindua Sultani Znz.

Bitter truth live it or leave it.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
nadhani muhimu ni kukaa na kufanya majadiliano tu
 
Kama unakiri serikali zote mbili zinafanya makosa kwenye hili jambo, kwanini usiseme ukweli kwamba wamekosea, badala yake nakuona unalazimisha waonekane hawana makosa.

Sheria inatakiwa kufuatwa kwa yule ambaye hataendeleza eneo lake bila kujali yeye ni nani, badala ya kumjulisha kwa kulimega eneo husika, na jingine kumuachia, unayajua haya kwasababu umesoma sheria, lakini unayapuuza kwa interest zako tu, unaacha siasa iingizwe kwenye mambo ya sheria.

Unakiri kwenye majibu yako kwamba serikali haikufuata taratibu rasmi kulitwaa eneo hilo, kwa nini? hakuna aliyepo juu ya sheria Tanzania hii, ndio maana unatakiwa kuomba radhi kwa hiki ulichoandika hapa, lakini ajabu zaidi ndio unadai unatoa elimu!.
 
Wazungu wametufanya vibaya sana!, wameongopa!. Ukweli ni kuwa Mjengo wa Ikulu ulijengwa na Sultan of Zanzibar, ili uwe makao makuu ya Uislamu Africa Mashariki. Jengo hilo liliitwa Dursalaam.

Enzi hizo a 10 miles za coastline ilikuwa chini yavSultan of Zanzibar. Humo ndani kulikuwa na msikiti na makaburi ya wana Sultani.

Wajerumani waliponunia ukanda huo ile 1890 kupitia mkataba wa Hellingoland, The Zanzibar Treaty, wakabadili msikiti kuugeuza kanisa!. Wakayahamisha makaburi, baadhi ya makaburi ya manguli wao, yakawagomea kuhamishika.

Waingereza walipoichukua Tanzania, ile 1918, ndio wakaweka hicho kibao cha uongo kuonyesha ni wao walijenga!. Ni waongo!. Ila walichofanya ni kuiboresha na kuongeza mjengo. Wazungu ni waongo sana, ila kwa vile ukweli wetu haujaandikwa, na wao uongo wao wameuweka kwenye maandishi, then uongo wao ndio unaonekana ni ukweli!.

Hata Ziwa Victoria, lilikuwepo kabla wakoloni hawajaja likiwa na jina la kiasili, wakalibatiza jina Queen Victoria, hivyo Ziwa hilo ni Ziwa Victoria mpaka leo!.

Story ya kweli ya Ikulu yetu iko hapa Kwa Simulizi za Mwana JF, Maalim Mohammed Said, Sio Mtu wa Kubezwa, Mengine ni Ukweli Mchungu!, Ila Pia Sio Mtu wa Kupuuzwa!.
P
 
tunataka tujue alipewa Kama mwekezaji au ni nchi ndani ya nchi nyingine!!??
Nyerere alimpa Jumbe eneo hilo bure ile 1971, kwenye the spirit of sisi ni nchi moja. Hivyo SMZ ilipewa kama eneo lao ndani ya Tanzania bara kama mtu au taasisi yoyote anavyoweza kumiliki Ardhi mahali popote. Kwa Zanzibar kumiliki eneo Tanzania bara, haimanishi kuwa eneo hilo ni sehemu ya Zanzibar!. Eneo hilo bado ni eneo la Tanzania bara mpaka mwisho wa dunia!.
P
 
Basi sio vibaya , Hilo eneo lirudi serikalini (bara)kwa kuwa walipewa kwa matumizi ya ufugaji , ili iwe rahisi kwa wao ku suply nyama kwao zbar. nakwakuwa walishindwa hakuna haja liendelee kushikiliwa na zbar with no plofit , NOR utilization!! Halafu wananchi wa bagamoyo wanashida na ardhi , na Hata Kama. wakienda kutafuta maisha zbar hawaruhusiwi kwa sheria za zbar kumiliki ardhi huko, Basi si warudishiwe ardhi yao iwafae maishani!!??

Huu muungano ni kichomi !! Na anaeumia ni Tanzania asili na sio wa zbar, 90% huu muungano unawa farvour wa zbar na sio watanzania (bara).

Hata hivyo wa Zanzibar wakiwa ughaibuni hawapendi kujitambulisha wao ni watanzania !!

Muungano huu ni very bias.
 
Ni ngumu sana kuelewa

Wao wanafikiri jambo hilo limeanza leo

Ova
 
Basi sio vibaya , Hilo eneo lirudi serikalini (bara)kwa kuwa walipewa kwa matumizi ya ufugaji , ili iwe rahisi kwa wao ku suply nyama kwao zbar. nakwakuwa walishindwa hakuna haja liendelee kushikiliwa na zbar with no plofit , NOR utilization!!
It's true ndio maana serikali yetu iliishalimega hilo eneo kuwamegea wawekezaji.
Halafu wananchi wa bagamoyo wanashida na ardhi , na Hata Kama. wakienda kutafuta maisha zbar hawaruhusiwi kwa sheria za zbar kumiliki ardhi huko, Basi si warudishiwe ardhi yao iwafae maishani!!??
Ni kweli na hili ndio linakwenda kutimizwa kwa SMZ kufutiwa kibali chao, maana hawana hati ya umiliki, na eneo hilo kukabidhiwa kwa halmashauri, kuwagawia wananchi.
Huu muungano ni kichomi !! Na anaeumia ni Tanzania asili na sio wa zbar, 90% huu muungano unawa farvour wa zbar na sio watanzania (bara).
Ni kweli kwasababu Tanzania bara na Tanzania Visiwani hazilingani!. Zanzibar ni the minority, siku zote the minority are favoured.
Hata hivyo wa Zanzibar wakiwa ughaibuni hawapendi kujitambulisha wao ni watanzania !!
Ni kweli, ila hata kama hawapendi kujitambulisha kama Watanzania, the facts ni Watanzania, hakuna mtu yoyote duniani anayetambulika kimataifa kama Mzanzibari, kwasababu Zanzibar sio nchi, Zanzibar ni sehemu ya JMT, tuna uraia mmoja tuu, uraia wa JMT.
Muungano huu ni very bias.
True
P
 
Umesahau miaka ya nyuma wafungwa walikuwa wanatoka zenji
Na kuja kufanya kazi kwenye ranchi hiyo
Kulikuwa na mpaka gereza lao

Ova
 
Tanzania bara yenyewe inasemekana
Nao huko unguja wana sehemu yao pia

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…