Wabara ondoeni shaka, ardhi ya SMZ Bagamoyo si sehemu ya Zanzibar. SMZ haina hati; limetelekezwa miaka 45 ila Zanzibar inamiliki kihalali

OK! Kwa kuwa hawana Hati Milki ya Ardhi hiyo, binafsi nimeridhika! Hata Muungano ukivunjika eneo hilo linabaki ni eneo la Bara.
 
Yaani hapa ndio ilitakiwa watanzania waende wakanikatie maeneo maana eneo limetelekezwa Kwa mda mrefu Sasa hivyo wavamizi Wana uhalali
 
Katoliki kumbe nayo ni nchi?
 
Pascal sheria inasemaje unapotelekeza eneo? Tujikite hapa
 
P kumbuka 7 figure inaanzia Millioni Moja Kwa hizi pesa zetu za madafu
 
Hapa Paskali unaweza kutuweke proof? Dhana ya kwamba Unguja/Pemba zilikuwa Part ya Ardhi ya Tanganyika before erosion au ndiyo Elimu ya kukariri "Big Bang Theory"?
No sio the Big Bang Theory!, ni the Tectonic theory, it's very unfortunately kwenye mitaala ya elimu yetu, hakuna topic ya Tectonic!. Mimi mwenyewe nimesoma HGL, kwenye vitabu vya physical geography, topic ya Tectonic ipo ila haifundishwi, hivyo Watanzania wala Wazanzibari hawajui inchi yao iliumbika vipi na ilimegeka kutokea wapi.

Karibu ujiongezee maarifa kuhusu tectonics

Plate Tectonics​

Plate tectonics is the study of the lithosphere, the outer portion of the Earth consisting of the crust and part of the upper mantle. The lithosphere is divided into about a dozen large plates which move and interact with one another to create earthquakes, mountain ranges, volcanic activity, ocean trenches and many other features. Continents and ocean basins are moved and changed in shape as a result of these plate movements.
Na kinachofuata miaka milioni ijayo ni hiki
Kazi ya kumegeka inaendelea and no one can do anything!.
Visiwa vitazama kwa kuzidiwa na nini?
Hayo ya visiwa kuzidiwa na kuzama, ni haya na yale ya Pasco, ila sometimes kwa watu wazito kuelewa unaweza kujikuta unaitwa mahali kuhojiwa!. Kwenye lile bandiko langu humu kuhusu Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi? kuna line nilisema "Baadhi ya Wabunge wa viti maalum, wako pale kutimiza tuu yale mahitaji ya kijamii ya kibinaadamu", Spika alikuja juu!, nilipoitwa Dodoma kuhojiwa na kama kamati, niliwafafanulia. Kuna baadhi ya hoja zangu naziwasilisha kwa kutumia tamathali za semi, mfano bandiko hili Tahadhari ya hatari: CCM Imepania Kufanya Kinyume cha Maumbile! watu walishtuka!. Hata nilipopandisha bandiko hili Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe? Wanzanzibari walikuja juu kuuliza kwenye hii ndoa ya muungano, nani mke nani mume?, nikawaambia mke ni aliyeposwa, mume ni aliyelipa mahari, mume ni anayechuma, mke ni golikipa anayepokea!.
Hiyo erosion ilitokeaje? Hivi unajua kwamba maji yakitoka ardhi ya Unguja/Pemba kuja Tanga/Dsm ni flat tu wala hakuna bonde? Na yakijaa unaweza kuzamisha hata minazi mitatu kwenda chini?
Hili kiukweli silijui, ninachojua ni Zanzibar ilikuwa sehemu ya Tanganyika, ikamegeka!. Mwarabu akavamia visiwa vyetu, akajifanya ni vyake, mwaka 1964, wanamume wakaingia kazini kwenye yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, wakaikomboa nchi yao, hivyo Mapinduzi Daima, na muungano wetu huu adhimu tutaulinda kwa gharama yoyote!.
P
 
Kwani wewe ni msemaji wa SMZ?
Watu lazima mjifunze kusoma authority!. Bandiko hili limeanza kwa a very high authority!. Taarifa ya Zanzibar kumiliki eka 6,000 Bagamoyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo, data za bandiko hili zimetolewa kwenye Mhimili!.
P
 

Shukrani Paskali kwa Elimu ya Tectonic plate na tamathali za semi 😀 😀.
 
Katoliki kumbe nayo ni nchi?
Vatican ina serikali inaitwa Holy See, inaendeshwa na Theokrasia badala ya Demokrasia.

Ila hakuna nchi inaitwa Swaziland, kuna Eswatini. Lesotho na Eswatini ni falme na jamhuri (kwa mtiririko huo) kamili zinazotambuliwa na Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola, SADC na AU. Mfano huu haufiti kwenye hoja.

Vatican, Taiwan, Tibet na Kosovo ndizo nchi pekee zisizotambuliwa na UN kati ya nchi 197 za dunia hii. Kosovo, Taiwan na Tibet zinashiriki UN kama watazamaji tu.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
PM

Kijiolojia na kama muungano utadumu, Znz ina kila sababu ya kupewa ardhi bara ili isipotee na ikipotea basi hakuna muungano tena maana Znz haitakuwepo kwy atlas ya dunia, itabidi Tanganyika irudishwe.

Wanajiolojia na wanameteorolojia wameridhika kwamba ifikapo mwaka 2100 visiwa vyote vya Znz na Mafia vitazama (vitaliwa na maji na kwisha kabisa), bado miaka 77 tu ambayo ni muda mfupi sana kuanzia hapa 2023. https://allafrica.com/stories/200805120694.html

Kujipanga na tukio hilo lililo karibu sana kutukia na kukata mzizi wa mgogoro kuhusu ardhi kati ya Znz na bara napendekeza serikali ya SMZ izindue mpango mkakati wa land fill au ocean reclamation ambao umeokoa UAE iliyoelemewa na population.

SMZ itafute uwezo wa kutekeleza mradi huu wa land fill na ikibidi iombe UN iiongezee eneo la bahari ya kimataifa ili kutanua mpaka wake.

Kwa njia hii mgogoro unaodhaniwa kuwepo wa Znz kuchukuwa ardhi ya bara utaisha asilani na hata Wabara wengi watahamia Znz kununua hiyo ardhi ya land fill.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
PM

Majibu yako yatapandisha watu pressure humu na kudondoka. Majibu yako yanaibua kero mpya ya muungano. Fanya mpango na media wadau twende kwenye mdahalo mubashara, huenda tukasikika zaidi ya humu jamvini.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Mbona mafuta walikataa kwamba siyo ya muungano wakati sisi tukiuza rasilimali za bara wanapata 4.5%? Rasilimali za muungano ni zipi kumbe? Nauliza kwa nia ya kujifunza.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Tulipoungana kwa mujibu wa hati za muungano, tulikuwa na mambo 11 tuu ya muungano, hati zikatamka sheria, taratibu na kanuni za kuongeza au kupunguza jambo lolote la muungano.
Mambo 11 original ya muungano ni haya

a) Katiba na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
b) Mambo ya nchi za nje
c) Ulinzi
d) Polisi
e) Mamlaka yanayohusika na hali ya hatari
f) Uraia
g) Uhamiaji
h) Mikopo na biashara ya nchi za nje
i) Utumishi katika Jamhuri ya Muungano.
j) Kodi ya mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na idara ya forodha
k) Bandari, mambo yanayohusu usafiri wa anga, Posta na Simu

Sisi tukayaongeza kutoka 11 mpaka 22 bila kufuata ule utaratibu rasmi. Kwa vile ardhi sio jambo la muungano, macao ya ardhi hayakupaswa kuwa mambo ya muungano. Gesi na mafuta ni miongoni mwa mambo yaliyoingizwa kuwa ya muungano kinyume cha utaratibu na ni miongoni mwa kero za muungano.

Karume akamuomba Kikwete tuyaondoe, tukayaondoa vile vile tulivyoyaingiza.

Hoja ya rasilimali za muungano ni changamoto, ndio maana mfuko wa pamoja wa fedha, umeishaundwa ila is not functioning!. Dawa pekee ya hili ni serikali moja au serikali 3. Mimi ni mtu wa Nyerere, ni muumini wa serikali moja, hivyo tunakuwa ni nchi moja, chini ya serikali moja na rais mmoja Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!"
P
 

[emoji1635]
 
Kujipanga na tukio hilo lililo karibu sana kutukia na kukata mzizi wa mgogoro kuhusu ardhi kati ya Znz na bara napendekeza serikali ya SMZ izindue mpango mkakati wa land fill au ocean reclamation ambao umeokoa UAE iliyoelemewa na population.
Naunga mkono hoja.
SMZ itafute uwezo wa kutekeleza mradi huu wa land fill na ikibidi iombe UN iiongezee eneo la bahari ya kimataifa ili kutanua mpaka wake.
Hakuhitajiki ombi lolote UN kufanya land fill,
ile hoteli ya Bakhresa Zanzibar imejengwa kwenye landfill. Kwa kadri tunavyo fanya landfill, mpaka wetu wa bahari unasogea automatically to the standard of 10 nautical miles.
Kwa njia hii mgogoro unaodhaniwa kuwepo wa Znz kuchukuwa ardhi ya bara utaisha asilani na hata Wabara wengi watahamia Znz kununua hiyo ardhi ya land fill.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Naunga mkono hoja
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…