Wabara ondoeni shaka, ardhi ya SMZ Bagamoyo si sehemu ya Zanzibar. SMZ haina hati; limetelekezwa miaka 45 ila Zanzibar inamiliki kihalali

Wabara ondoeni shaka, ardhi ya SMZ Bagamoyo si sehemu ya Zanzibar. SMZ haina hati; limetelekezwa miaka 45 ila Zanzibar inamiliki kihalali

No sio wako nyuma, bali ni watu wa ajabu sana!. Utakuta hapa wanapiga kulele kusikia Zanzibar ina eneo bara, lakini kuna ma settles walikuwa na maeneo kama yule Mzungu Steyn mwenye ushamba ya ngano kule Malbadawi Hanang, Mashamba ya chai ya Mufindi yanamilikiwa na Brookebond, Pale Kisarawe Luna eneo la hectares 27,000 ni shamba la Sun Biofuels, walalima mibono kaburi kuzalisha Biofuels. Kule Machame Luna mzungu na mkewe, Silverdales, wamedhulumiwa shamba lao, no one complains lakini Mzanzibari kuwa na eneo bara... nongwa!.
P
Nadhani unachanganya mambo.

Settlers siyo nchi, Znz ni nchi. Hoja hapa ni nchi siyo mtu (mwekezaji). Wapemba wamejazana bara wanamiliki mashamba na maghorofa lkn hawajawahi kulalamikiwa na wabara.

Suala ni nchi siyo mtu, Znz ni nchi maana ina serikali kamili.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Nadhani unachanganya mambo.

Settlers siyo nchi, Znz ni nchi. Hoja hapa ni nchi siyo mtu (settler/mwekezaji). Wapemba wamejazana bara wanamiliki mashamba na maghorofa lkn hawajawahi kulalamikiwa na wabara.

Suala ni nchi siyo mtu, Znz ni nchi maana ina serikali kamili.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
PM
Nadhani ukijivua kwenye utumwa wa historia potofu utakuwa huru kuelewa uhalisia wa dhana nzima ya sovereignty ya nchi.

Jukumu la kwanza kabisa linalofanyika kipaumbele cha kwanza cha rais yeyote wa nchi huru ni ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi na raia wake. Ndiyo maana ndiye M'kiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Taifa.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Nadhani unachanganya mambo.

Settlers siyo nchi, Znz ni nchi. Hoja hapa ni nchi siyo mtu (mwekezaji). Wapemba wamejazana bara wanamiliki mashamba na maghorofa lkn hawajawahi kulalamikiwa na wabara.

Suala ni nchi siyo mtu, Znz ni nchi maana ina serikali kamili.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Hii ndio essence ya bandiko hili elimishi, kuwaelimisha watu kama nyinyi kuwa SMZ kumiliki eneo Tanzania bara, SMZ ni wamiliki tuu kama wamiliki wengine wowote, na umiliki wao wa eneo hilo hakulifanyi eneo hilo kuwa ni sehemu ya Zanzibar!, eneo hilo bado ni eneo la Tanzania bara milele!.

Na kwa msio jua pale mpakani Rusumo, Tanzania tumewapa eneo Rwanda, Burundi na DRC wajenge ICD zao. Maeneo hayo hayawi sehemu ya Rwanda, Burundi or DRC!. Maeneo yote ya Balozi mbalimbali tumewapa, hakuyafanyi yasiwe nchi yetu!. Tanzania tunamiliki maeneo ya balozi zetu mbalimbali, hakuyafanyi kuwa sehemu ya Tanzania!.
P
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huja na kwa maslahi ya taifa.

Maslahi ya leo ni hii issue ya SMZ kumiliki eneo la ekari 6000 Bagamoyo. Tangazo la SMZ Zanzibar: Hekta 6,000 zilizopo Bagamoyo ni mali yetu
limeleta taharuki na sintofahamu kubwa kwenye mitandao ya kijamii hadi baadhi ya watu kutoa povu!.

Kuna watu wanatafsiri potofu kuwa sehemu ya Ardhi ya Tanzania Bara ni sehemu ya Zanzibar!.

Ukweli ni huu
Anza na bandiko hili la mwaka 2014 iujue historia ya eneo hilo lilimilikiwa vipi na Zanzibar Zanzibar ndani ya Tanganyika ilianzia huku kisha soma majadiliano ya Bunge ya miaka ya nyuma kuhusu issue hii.

View attachment 2644793

Shamba la Mifugo Linalomilikiwa na SMZ huko Bagamoyo

MHE. MOSSY SULEIMANI MUSSA
aliuliza:-

Kwa kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliwahi kuwa na shamba kubwa la mifugo (ng’ombe) ranchi huko Bagamoyo:-

(a) Je, Serikali ya SMZ bado inamiliki shamba hilo?
(b) Je, hadi kufikia kuboreshwa kwa shamba hilo SMZ ilitumia shilingi ngapi?

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na uvuvi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mossy Suleimani Mussa Mbunge wa Mfenesini lenye vipengele (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika kwa kuzingatia Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA) iliyoko Makurunge katika Wilaya ya Bagamoyo inamilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ranchi hiyo ilianzishwa mwaka 1976 baada ya kupata kibali kutoka kwa Kamishna wa Ardhi chenye kumbukumbu namba LD/70254/12/TBR cha tarehe 24/09/1971, hivyo kwa taarifa hizo Wizara yangu bado inaamini shamba la RAZABA bado ni mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hata hivyo kwa vile swali linaloulizwa na Mheshimiwa Mbunge linahusu mali zilizo chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi sio Wizara ya Muungano napenda kumjulisha Mheshimiwa kuwa Wizara yangu haiwajibiki kujua kama Serikali ya Mapinduzi Zanzibar bado inamiliki au haimiliki shamba hilo.

(b) Mheshimiwa Spika, Wizara yangu haijui kama shamba hilo ambalo liko chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lilitumia shilingi ngapi katika kuliboresha, namshauri Mheshimiwa Mbunge akapate majibu ya takwimu hizo Wizara inayohusika katika Serilkai ya Mapinduzi Zanzibar.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI:

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri naomba kutoa maelezo ya nyongeza kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, shamba hilo ambalo ni kweli kama alivyosema Naibu Waziri lilimilikishwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lakini kwa miaka mingi sana karibu 30 halitumiki, kwa hivi karibuni Serikali imemega sehemu na kuwapa wawekezaji, watawekeza katika mambo ya biofuel na Sehemu bado inaendelea kuwa mali ya SMZ.

View attachment 2644761

My Take
  1. Wabara ondoeni shaka kuhusu umiliki wa SMZ eneo Bagamoyo, SMZ inalimiliki eneo hilo kihalali kabisa kwa vile walipewa na Mwalimu Nyerere.
  2. Kitendo cha SMZ kumiliki eneo huku Tanzania bara, hakulifanyi eneo hilo kuwa sehemu ya Zanzibar, ni eneo halali la SMZ ila ardhi ni ya Tanzania bara.
  3. Nchi yoyote inaweza kumiliki eneo nchi nyingine yoyote, umiliki huo haulifanyi hilo eneo kuwa sio sehemu ya nchi husika.
  4. Japo SMZ inalimiliki eneo hilo lililokuwa hekta 6,000, kwanza SMZ, haina hati ya umiliki bali ina kibali cha umiliki No. LD/70254/12/TBR cha tarehe 24/09/1971.
  5. SMZ ililitelekeza eneo hilo kwa miaka 45, hivyo serikali ikalimega kumpa mwekezaji, Halmashauri ya Bagamoyo imelipima viwanja inaviuza.
  6. Kwa vile ni eneo halali la SMZ, na sasa SMZ imeibuka kuonyesha ina interest na eneo lake, then itarudi serikalini kuelezea hiyo interest, serikali itakwenda kulipima limebakia kiasi gani, SMZ itapimiwa upya na kugawa.
  7. Iwapo SMZ bado italihitaji eneo lote la awali la ekari 6,000, then italazimika kuwalipa fidia watu wote waliomegewa kihalali.
  8. Kama pia limevamiwa na wananchi, then sheria yetu ya Ardhi ya Vijiji No. 5 ya mwaka 1999 will apply kwa mtu aliyetelekeza eneo lake kwa miaka 45, wale wavamizi wana haki fulani.
  9. Ikionekana madhara ya kuwaondoa wavamizi ni makubwa kuliko kuirejeshea SMZ eneo hilo, then kile kibali cha umiliki wa SMZ kinafutwa, wananchi wanapimiwa, na SMZ wanapewa eneo jingine, tuna mapori kibao ya kumwaga, hata wakitaka heka 10,000 wanapewa.
  10. Hii ya kuwagaiya wavamizi imefanyika sana kwenye maeneo ya jeshi na maeneo ya RTD, wavamizi wamepimiwa na kuhalalishiwa!.
Hivyo Watanzania wenzangu isiwe na wasiwasi kabisa kuhusu hili, after all eneo lote la Zanzibar ni sehemu ya JMT hakuna sababu ya watu kutoa povu, Wanzanzibari kuniliki Ardhi Bara lakini Wabara hawewezi kumiliki ardhi Zanzibar, kwasababu Wazanzibari ni Watanzania wenzetu wana haki zote za Utanzania, ila Zanzibar ni the minority, visiwa vyao ni very tiny, tukiruhusu kila Mtanzania kumiliki ardhi Zanzibar, itaelemewa na kuvizamisha visiwa vile!.

Wakati wa kuumbika nchi, Zanzibar ilikuwa eneo la bara likamegeka kwa sea erosion, hivyo Visiwa vya Zanzibar ni sehemu halali ya Tanzania bara ndio maana dhima ya muungano wetu adhimu ni udugu, sisi ni ndugu moja, Waarabu walipokuja Zanzibar ile 1732 Sultan Seyyid Said alipohamoshia Sultanet take toka Oman kuja Zanzibar, aliwakuta wenyeji halisi ni Wahadimu, kutoka Bara, alivitwaa visiwa hivyo toka ukoo wa Mwinyimkuu, na waliompindua Sultan kwenye yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni wajukuu wa Mwinyimkuu wenye Zanzibar yao, ndio maana slogan ya Mapinduzi Daima ipo, na baada ya muungano tumekuwa kitu kimoja, ndio maana slogan ya muungano ni tutaulinda kwa gharama yoyote.

Miongoni mwa gharama hizo ni kumsamehe madeni, kumpa 4.5% ya fedha za mikopo na misaada, ajira na hata kumpa eneo lolote Wazanzibari watakalotaka.

Watanzania bara tujifunze kuwa na shukrani, tushukuru sana Zanzibar, ukanda wa eneo la maili 10 ya Pwani ya ya bahari ya hindi, lilikuwa eneo la Zanzibar, ikatugawia!, miji yote ya Pwani kuanzia Dar, Tanga, Bagamoyo imejengwa na Sultan of Zanzibar!

Hata mjengo wa Ikulu ya Magogoni, imejengwa na Sultan of Zanzibar, hata ile replica ya Ikulu pale Chamwino ni mjengo wa Kiarabu!, mbona watu mnakosa shukrani kwa mambo mazuri kama haya, mnaona nongwa Zanzibar kumiliki eneo huku Bara!

Mapinduzi Daima
Muungano Tutaulinda kwa gharama yoyote!.

Paskali.
Taja faida zake Ili uweze kutuambia utaulinda kwa Gharama zote!
 
Hao wamekuja kama wawekezaji wa kigeni. Na pengine wengine ni raia kamili. Sasa sisi na Zanzibar tulipoungana tulikubaliana kuwa kila mtu atabaki na ardhi yake. Kuwa ardhi siyo suala la Muungano. Ukitaka kwenda kwa mwingine utaenda kuwekeza kama raia wa kigeni. Hivyo ndivyo inavyotakiwa. SMZ inawakilisha raia wote wa Zanzibar. Wakitaka ardhi Tanganyika lazima waje kama wawekezaji wa kigeni.
No it's not that, japo ni kweli ardhi sio jambo la muungano, lakini uraia wa JMT tuu ni jambo la muungano, hivyo Wazanzibari wote ni Watanzania, wana haki zote za Utanzania ikiwemo kumiliki ardhi, na taasisi zote za Zanzibar ikiwemo SMZ, wana haki ya kumiliki ardhi Tanzania bara kwa Utanzania wao, ila ulaazi wa Zanzibar sio wa muungano, ni kwa Wanzanzibari pekee, hivyo Mtanzania wa bara au taasisi ya bara, ikitaka kumiiki ardhi Zanzibar, inamilikishwa kama mwekezaji.
P
 
Waliotemwa wako mtaani na umri mdogo sasa Hata kulima hawawezi.
 
Attachments

  • CCEFEDC0-200C-4C93-892D-A3BEB6C59968.jpeg
    CCEFEDC0-200C-4C93-892D-A3BEB6C59968.jpeg
    32.9 KB · Views: 6
Wengine amefukuzwa wamekimbilia mahakamani.
Brother P, jitume utoona majibu na Matokeo mazuri kimaisha
 
Attachments

  • 51FBDDF6-EB31-4529-95A1-4F6169D7A925.jpeg
    51FBDDF6-EB31-4529-95A1-4F6169D7A925.jpeg
    186.7 KB · Views: 5
Brother P, ukiamua kujituma kiakili na kifkra unaweza kuwa bilionea ukaachana na kusifia kisichosifika.

Udc salary ni basic 3.8m utaipeleka wapi wakati una kichwa chenye uwezo wa kuzalisha mabilioni kwa mwezi?
Kiukweli Peno, watu tunadharauliana sana humu!. Mimi nikiwa New Delhi, niliajiriwa CFO kama LE-1, nikawa posted BHC Dar es Salaam, take home ni 7 figure!, niliacha mwenyewe voluntarily na kuwa busy na PPR, sasa mtu kunifikiria nautafuta u DC ni kama kunitukana!.
P
 
No it's not that, japo ni kweli ardhi sio jambo la muungano, lakini uraia wa JMT tuu ni jambo la muungano, hivyo Wazanzibari wote ni Watanzania, wana haki zote za Utanzania ikiwemo kumiliki ardhi, na taasisi zote za Zanzibar ikiwemo SMZ, wana haki ya kumiliki ardhi Tanzania bara kwa Utanzania wao, ila ulaazi wa Zanzibar sio wa muungano, ni kwa Wanzanzibari pekee, hivyo Mtanzania wa bara au taasisi ya bara, ikitaka kumiiki ardhi Zanzibar, inamilikishwa kama mwekezaji.
P
Kuwa raia wa JMT si guarantee ya kuwa utapata ardhi popote ndani ya Tanzania. Ndiyo maana Zanzibar ni sehemu ya JMT lakini raia kamili kutoka Mwanza au Kigoma hawezi kumiliki ardhi Zanzibar. So wazanzibar kuwa raia wa JMT si kigezo cha wao kuwa na "haki zote za Utanzania na kupata ardhi popote."

Kwa mantiki yako ni kwamba watu wa Tanzania bara hawana haki zote za Utanzania kwa sababu hawaruhusiwi kumiliki ardhi katika baadhi ya sehemu za nchi yao!!!
 
Hii ndio essence ya bandiko hili elimishi, kuwaelimisha watu kama nyinyi kuwa SMZ kumiliki eneo Tanzania bara, SMZ ni wamiliki tuu kama wamiliki wengine wowote, na umiliki wao wa eneo hilo hakulifanyi eneo hilo kuwa ni sehemu ya Zanzibar!, eneo hilo bado ni eneo la Tanzania bara milele!.

Na kwa msio jua pale mpakani Rusumo, Tanzania tumewapa eneo Rwanda, Burundi na DRC wajenge ICD zao. Maeneo hayo hayawi sehemu ya Rwanda, Burundi or DRC!. Maeneo yote ya Balozi mbalimbali tumewapa, hakuyafanyi yasiwe nchi yetu!. Tanzania tunamiliki maeneo ya balozi zetu mbalimbali, hakuyafanyi kuwa sehemu ya Tanzania!.
P
Why are you speaking with such authority mkuu? Wewe ni Msemaji wa Serikali ya SMZ? Nani kakupa ruksa ya kutoa matamshi kwa niaba ya SMZ? Yaani unataka kusema haya yote uliyoandika umefanya hivyo kama mfuatiliaji binafsi wa mambo?
 
Kuwa raia wa JMT si guarantee ya kuwa utapata ardhi popote ndani ya Tanzania. Ndiyo maana Zanzibar ni sehemu ya JMT lakini raia kamili ktoka Mwanza au Kigoma hawezi kumiliki ardhi Zanzibar. So wazanzibar kuwa raia wa JMT si kigezo cha wao kuwa na "haki zote za Utanzania na kupata ardhi popote."
Hoja nyingine zinatia hasira!. Uraia wa JMT ni uraia wa aina moja!. Haki za kiraia kwa Mtanzania zinafanana kabisa!, kuna Watanzania bara wanajidhania wana haki zaidi kuliko Wanzanzibari!, ni wajinga tuu.
P
 
No it's not that, japo ni kweli ardhi sio jambo la muungano, lakini uraia wa JMT tuu ni jambo la muungano, hivyo Wazanzibari wote ni Watanzania, wana haki zote za Utanzania ikiwemo kumiliki ardhi, na taasisi zote za Zanzibar ikiwemo SMZ, wana haki ya kumiliki ardhi Tanzania bara kwa Utanzania wao, ila ulaazi wa Zanzibar sio wa muungano, ni kwa Wanzanzibari pekee, hivyo Mtanzania wa bara au taasisi ya bara, ikitaka kumiiki ardhi Zanzibar, inamilikishwa kama mwekezaji.
P
Kwa sababu ardhi ya visiwani Zanzibar ni ndogo sana sioni kama kuna tatizo wao kumiliki ardhi huku bara !
 
Why are you speaking with such authority mkuu? Wewe ni Msemaji wa Serikali ya SMZ? Nani kakupa ruksa ya kutoa matamshi kwa niaba ya SMZ? Yaani unataka kusema haya yote uliyoandika umefanya hivyo kama mfuatiliaji binafsi wa mambo?
Umelisoma bandiko hili tangu mwanzo?, hukuona the authority niliyoitumia?. Sii wengi wanajua kuwa sisi watu wa media we are an authority of our own!. Sisi ni mhimili!, the fourth Estate or the Fourth Protocol!.
P
 
Hii ndio essence ya bandiko hili elimishi, kuwaelimisha watu kama nyinyi kuwa SMZ kumiliki eneo Tanzania bara, SMZ ni wamiliki tuu kama wamiliki wengine wowote, na umiliki wao wa eneo hilo hakulifanyi eneo hilo kuwa ni sehemu ya Zanzibar!, eneo hilo bado ni eneo la Tanzania bara milele!.

Na kwa msio jua pale mpakani Rusumo, Tanzania tumewapa eneo Rwanda, Burundi na DRC wajenge ICD zao. Maeneo hayo hayawi sehemu ya Rwanda, Burundi or DRC!. Maeneo yote ya Balozi mbalimbali tumewapa, hakuyafanyi yasiwe nchi yetu!. Tanzania tunamiliki maeneo ya balozi zetu mbalimbali, hakuyafanyi kuwa sehemu ya Tanzania!.
P
1. Malawi Cargo Dar.

2. Zambia Cargo Dar na Mtwara.

3. Kumbe ndiyo maana Magufuli alikuwa mjanja akamgomea Museveni kwamba lazima JMT nayo imiliki EACOP Bomba la Mafuta la Hoima Chongoleani badala ya Uganda pekee. Urefu wa bomba 1443 km, 80% ikimilikiwa (iko) JMT na 20% Uganda.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom