Wabobezi wa siasa za Kiafrika nisaidieni; kwanini Kenya ina siasa za kipekee ndani ya Afrika Mashariki?

The deep state wenyewe wapigaji wapo kimaslahi unategemea nn?
 
Miaka ya 80's alisema mwakasege alikua anatoka Kenya anakuja Tanzania akakaribia Namanga ghafla akaona anapotoka Kenya Kuna mwanga anapoelekea mbele ya boda Namanga Kuna Giza mpaka hapo utaelewa kwanin Kenya wapo tofauti na wengine
Kwa hiyo ndo kusema Tanzania shetan ametamalaki na Kenya Mungu ametamalak?
 
Siasa zetu za kipekee hizi hapa👇😁😁😁
Your browser is not able to display this video.
 
Kwa hiyo ndo kusema Tanzania shetan ametamalaki na Kenya Mungu ametamalak?
Kenya wakimaliza uchaguzi kwa amani Kama ilivyo saivi,utakua miongoni mwa chaguzi bora kabisa kuwahi kutokea hapa Africa.Pengine na nchi zingine zinaweza kujifunza kupitia Kenya.Narudia,Kama uchaguzi ukimalizika kwa amani Kama walivyopiga kura
 
Kwa sababu wamejifunza kupitia njia ngumu (2013, 2017). They know the consequences by personal experience.
Hapa ulimaanisha 2007? Maana 2017 hakukuwa na shida lakini 2007 ndiyo kuliwaka moto hadi kupelekea Serikali ya mseto
 
Tanzania ukabila bado upo sana, ila tunaita kanda- utasikia kanda ya ziwa, kanda ya kaskazini, kanda ya nyanda ya juu kusini. Haya mambo hayakwepeki, po pote pale yapo. Hata huko Marekani kuna majimbo na chama chao. Ila mfumo wa Kenya naupendaga hata kama kama ukabila; angalia Afrika Mashariki - Uganda, Rwanda na Tanzania demokrasia iko wapi. ubabe ubabe tu.
Tanzania tuna shida kubwa ni Tanganyika na Zanzibar. Hakuna Tanganyika yetu; sisi tunatawalia na siasa za ajabu ambazo hazipo katika nchi yo yote duniani. Nchi zinaungana lakini hakuna iliyoungana nayo.
 
Kiujumla sikubaliani nawe.

Huo ukabila wa Tanzania unachochewa tu sasa hivi na hawa viongozi hafifu.

Tanzania tulishaachana na ukabila siku nyingi tu. Hawa wanaotafuta kuurudisha ninahakika hawatafanikiwa.
Umegusia siasa za Marekani? Huzijui. Achana na vitu usivyokuwa na ujuzi navyo.

Sasa usinielewe vibaya, sijasema siasa za huko ndizo bora, la hasha. Zinao upungufu mwingi tu, lakini siyo kama hizi za ki-CCM inayoteka taifa zima na raia zake kuwa kama mali yao.
 
Siasa za Kenya ni za kipuuzi. Hatuna cha kuiga huko zaidi ya ukabila.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…