Wabobezi wa siasa za Kiafrika nisaidieni; kwanini Kenya ina siasa za kipekee ndani ya Afrika Mashariki?

Wabobezi wa siasa za Kiafrika nisaidieni; kwanini Kenya ina siasa za kipekee ndani ya Afrika Mashariki?

MKUU

Deep state yao ina maono Sana!haikukubabali ujinga wetu wa huku!eti huku wamefumba macho wakiona ufisadi ukijua Hadi kukita mizizi!walishindwa hata kumchagua member ndani yao the state aanzishe chama na kishike dola kama mbadala wa CCM!wakaiacha NCHI itopee kwenye UFISADI na wakamuingiza jpm mkenge akaingia katikati ya moto mkali wa mapambano makali akapigwa propaganda za kitoto na kuchonganishwa na wananchi na kuchukiwa Sana na wananchi!!Hata kama ni mimi mzalendo ningekuwa jpm ningefanya vilevile co hamna namna!Sasa walamba asali wametapakaa wakijipandishia mafuta wanavotaka huku the state INAVUMILIA eti muda ufike ndio wafanye maamuzi wakati WANAJUA watu wanaumia Sana KWA mdororo wa uchumi uliopo!!!


The state Kati ya kosa kubwa mmelifanya ni kuruhusu nchi kuongozwa na chama kimoja KWA muda mrefu kiasi kwamba ufisadi umekuwa kama SHERIA ya asili hapa nchini akija mzalendo anapata shida kuongozwa nchi iliyooza kwq ufisadi Hadi anachukiwa na wananchi KWA propaganda za kitoto!!!

Shame on you Tanzania The state for this!!! CCM imeumiza wengi Sana na kuua wengi Sana Ili ibaki madarakani kuliko hata mngeleta chama mbadala cha kupokezana nayo angalau mngeponyesha Taifa KWA ukatili uliojitokeza miaka yote hii!!
The deep state wenyewe wapigaji wapo kimaslahi unategemea nn?
 
Miaka ya 80's alisema mwakasege alikua anatoka Kenya anakuja Tanzania akakaribia Namanga ghafla akaona anapotoka Kenya Kuna mwanga anapoelekea mbele ya boda Namanga Kuna Giza mpaka hapo utaelewa kwanin Kenya wapo tofauti na wengine
Kwa hiyo ndo kusema Tanzania shetan ametamalaki na Kenya Mungu ametamalak?
 
Siasa zetu za kipekee hizi hapa👇😁😁😁
 
Kwa hiyo ndo kusema Tanzania shetan ametamalaki na Kenya Mungu ametamalak?
Kenya wakimaliza uchaguzi kwa amani Kama ilivyo saivi,utakua miongoni mwa chaguzi bora kabisa kuwahi kutokea hapa Africa.Pengine na nchi zingine zinaweza kujifunza kupitia Kenya.Narudia,Kama uchaguzi ukimalizika kwa amani Kama walivyopiga kura
 
Kwa sababu wamejifunza kupitia njia ngumu (2013, 2017). They know the consequences by personal experience.
Hapa ulimaanisha 2007? Maana 2017 hakukuwa na shida lakini 2007 ndiyo kuliwaka moto hadi kupelekea Serikali ya mseto
 
Umejitahidi.

Mwanzo nilitaka kupuuza, lakini kadri nilivyosoma mada nikaona kweli umechanganyikiwa na siasa zilivyo Kenya.

Mkuu 'sepema', hakuna tofauti kati yetu na Kenya katika mambo ya msingi. Wote ni fursa tu kwa wanaojvisha kilemba cha uanasiasa.

Kama unataka kutafuta tofauti kati yao na sisi, tazama sehemu hizi mbili muhimu:
1. Ukabila
2. CCM

Tofauti zetu kubwa kwa sasa ni katika mambo haya mawili.

Hapa kwetu bila uwepo wa CCM, nasi pia tungekuwa na vyama vingi vinavyoibuka kila wakati wa uchaguzi ili kutafuta maslahi. Ila kwa kuwa bado ipo CCM inayounganisha wenye maslahi yao, basi tupo tofauti na Kenya. Wanaojiita viongozi wamejazana huko CCM wakijua maslahi yao huko ndiko yalipo; kwa nini wahangaike na kuanzisha vyama vingine?

Kenya, jambo muhimu kuliko yote ni kabila. Hata katika uchaguzi huu unaoonekana kuwa kama wa mfano kwa wengine, bado ukabila ndio msingi mkuu, na kila kiongozi anayetaka kuongoza ni lazima aweke kabila mbele, hasa kwa wakikuyu na Kalenjin na waluo. Ili ushindi upatikane ni lazima Kikuyu wakubali. au Kalenjini wakubali.

Kwa hiyo hivi vikabila vingine vyote, viongozi wa huko wanaunda tuvyama ili waweze kuungana na kile kinachoongozwa na Mkikuyu au Kalenjini au Mluo ili kutafuta maslahi

Hizi ni siasa za kilaghai, kama zilivyo zile za CCM hapa kwetu.

Sasas nimalizie kwa tahadhari: Tanzania nao tunaelekea kwenye miunganiko ya tuvyama, kama ilivyo Kenya. Hivi vyama vya mfukoni vinabebwa na CCM na huenda CHADEMA nao wakawa njiani kujiingiza ili na wao waweze kuingia serikalini wapate ulaji (maslahi). Bila shaka Samia na Mbowe bado wanalipika hili jinsi litakavyopakuliwa.

Uganda ni mali ya M7 kama Rwanda ilivyo mali ya Kagame kupitia kwenye vyama vyao vya kijeshi.
Tanzania ukabila bado upo sana, ila tunaita kanda- utasikia kanda ya ziwa, kanda ya kaskazini, kanda ya nyanda ya juu kusini. Haya mambo hayakwepeki, po pote pale yapo. Hata huko Marekani kuna majimbo na chama chao. Ila mfumo wa Kenya naupendaga hata kama kama ukabila; angalia Afrika Mashariki - Uganda, Rwanda na Tanzania demokrasia iko wapi. ubabe ubabe tu.
Tanzania tuna shida kubwa ni Tanganyika na Zanzibar. Hakuna Tanganyika yetu; sisi tunatawalia na siasa za ajabu ambazo hazipo katika nchi yo yote duniani. Nchi zinaungana lakini hakuna iliyoungana nayo.
 
Tanzania ukabila bado upo sana, ila tunaita kanda- utasikia kanda ya ziwa, kanda ya kaskazini, kanda ya nyanda ya juu kusini. Haya mambo hayakwepeki, po pote pale yapo. Hata huko Marekani kuna majimbo na chama chao. Ila mfumo wa Kenya naupendaga hata kama kama ukabila; angalia Afrika Mashariki - Uganda, Rwanda na Tanzania demokrasia iko wapi. ubabe ubabe tu.
Tanzania tuna shida kubwa ni Tanganyika na Zanzibar. Hakuna Tanganyika yetu; sisi tunatawalia na siasa za ajabu ambazo hazipo katika nchi yo yote duniani. Nchi zinaungana lakini hakuna iliyoungana nayo.
Kiujumla sikubaliani nawe.

Huo ukabila wa Tanzania unachochewa tu sasa hivi na hawa viongozi hafifu.

Tanzania tulishaachana na ukabila siku nyingi tu. Hawa wanaotafuta kuurudisha ninahakika hawatafanikiwa.
Umegusia siasa za Marekani? Huzijui. Achana na vitu usivyokuwa na ujuzi navyo.

Sasa usinielewe vibaya, sijasema siasa za huko ndizo bora, la hasha. Zinao upungufu mwingi tu, lakini siyo kama hizi za ki-CCM inayoteka taifa zima na raia zake kuwa kama mali yao.
 
Siasa za Kenya ni za kipuuzi. Hatuna cha kuiga huko zaidi ya ukabila.
 
Back
Top Bottom