Umejitahidi.
Mwanzo nilitaka kupuuza, lakini kadri nilivyosoma mada nikaona kweli umechanganyikiwa na siasa zilivyo Kenya.
Mkuu 'sepema', hakuna tofauti kati yetu na Kenya katika mambo ya msingi. Wote ni fursa tu kwa wanaojvisha kilemba cha uanasiasa.
Kama unataka kutafuta tofauti kati yao na sisi, tazama sehemu hizi mbili muhimu:
1. Ukabila
2. CCM
Tofauti zetu kubwa kwa sasa ni katika mambo haya mawili.
Hapa kwetu bila uwepo wa CCM, nasi pia tungekuwa na vyama vingi vinavyoibuka kila wakati wa uchaguzi ili kutafuta maslahi. Ila kwa kuwa bado ipo CCM inayounganisha wenye maslahi yao, basi tupo tofauti na Kenya. Wanaojiita viongozi wamejazana huko CCM wakijua maslahi yao huko ndiko yalipo; kwa nini wahangaike na kuanzisha vyama vingine?
Kenya, jambo muhimu kuliko yote ni kabila. Hata katika uchaguzi huu unaoonekana kuwa kama wa mfano kwa wengine, bado ukabila ndio msingi mkuu, na kila kiongozi anayetaka kuongoza ni lazima aweke kabila mbele, hasa kwa wakikuyu na Kalenjin na waluo. Ili ushindi upatikane ni lazima Kikuyu wakubali. au Kalenjini wakubali.
Kwa hiyo hivi vikabila vingine vyote, viongozi wa huko wanaunda tuvyama ili waweze kuungana na kile kinachoongozwa na Mkikuyu au Kalenjini au Mluo ili kutafuta maslahi
Hizi ni siasa za kilaghai, kama zilivyo zile za CCM hapa kwetu.
Sasas nimalizie kwa tahadhari: Tanzania nao tunaelekea kwenye miunganiko ya tuvyama, kama ilivyo Kenya. Hivi vyama vya mfukoni vinabebwa na CCM na huenda CHADEMA nao wakawa njiani kujiingiza ili na wao waweze kuingia serikalini wapate ulaji (maslahi). Bila shaka Samia na Mbowe bado wanalipika hili jinsi litakavyopakuliwa.
Uganda ni mali ya M7 kama Rwanda ilivyo mali ya Kagame kupitia kwenye vyama vyao vya kijeshi.