ngulyabhule
JF-Expert Member
- Apr 5, 2020
- 344
- 712
Binafsi ni mtumishi wa serikali, katika kupambana na kujiongeza nilijaaliwa kuwa na mashine ya kukoboa na kusaga nafaka kwa sababu ya muda kuwa limited ikanibidi kuwa na mtu wa kuendesha mradi huu awali nilisimamia mwenyewe kwa takribani siku 18 baada ya kuwa likizo sasa siku za likizo zilipo karibia kuisha nikampata kijana ambaye niliamini angekuwa anapiga mzigo. IKUMBUKWE wakati nipo mwenyewe maombi ya vijana na jamaa wenye ndugu yalikuwa mengi sana ya kutaka kazi maana waliajua mi ni mtumishi.
Basi yule dogo kwa siku kama kumi hivi nipo naye mambo yakawa fresh nilipo anza kazi nikawa napata muda wa jioni tu kumpiga sapoti lakini ndani ya siku tano tu nikagundua huyu dogo hakuwa mwaminifu nikapiga chini! Akaja kijana wa pili wa tatu wa nne wote ni wale wale mbaya zaidi nilikuwa nawatoa mikoa tofauti tofauti lakini tabia ni zile zile (WIZI) sasa huyu nne ndiye aliye sababisha hadi mimi kufunga kwa muda mashine nilidumu naye kwa miezi tisa!
Huyu wizi wake ulikuwa wa kisomi yaani nikinunua umeme na kuingiza naye akawa ananua wakwake anaingiza sasa anapiga kazi pesa inakuwa yake me nikienda nakuta umeme umetumika kidogo na dogo ananipa pesa ile ile sawa na umeme ulivyo tumika kumbe kazi imepigwa ya maana kwa umeme wake! ingawa sasa maombi na malalamiko ya wanakijiji yakawa mengi kuwa nimewakatili sana! Ingawa maumivu na machungu yangu hawakuyajua!
Jamaa mmoja akanisanua kuwa nijaribu kumtafuta mmalawi na kwa vile tukuyu na malawi ni jirani basi jamaa akanipa connection dogo akapatikana awali mashine nikawa nafungua kuanzia saa tisa ingawa pale pale mashineni ndo palikuwa na geto hivyo asubuhi dogo kazi yake ilikuwa kukusanya nafaka na kupanga then jioni tunaamsha motor japo wananchi walikuwa wakimind but lengo langu hawakulijua!
Basi siku, mwezi zilikatika mpaka yule dogo akaanza kuelewa hata kiswahili mwaka wa kwanza wa pili hadi wa tatu dogo tunaenda poa mwaka wa nne likaja wazo la kuwa na banda la ufugaji nikafanikiwa nikawa na ng'ombe na kuku!
Nikapata tena kijana wa kibongo mambo yakawa yale yale nilianza na kuku wadogo ila ng'ombe nilinunua anaye kamuliwa bwana eh kijana hakulaza damu akawa ananipiga maziwa! Hapa sikulaza damu nikameuleza mmalawi wangu tunapataje mtu akasema boss mbona wengi tuu basi bwana ijumaa moja akashuka malawi j pili jioni dogo akatimba na mwenzake!
Kwa ufupi hawa vijana kwa kazi na uaminifu wao sitaki tena kusikia watanzania kwenye project yangu yoyote hata siku za usoni! Hii tabia ya wizi kwa wabongo nimeamini na haitupi sifa nzuri!