Wabongo mkija majuu au ughaibuni acheni unafiki, majungu na ukora mnaliabisha Taifa lenu

Wabongo mkija majuu au ughaibuni acheni unafiki, majungu na ukora mnaliabisha Taifa lenu

Mkuu Kiranga nakuja Marekani kukuhubiria neno uokoke,ukishaokoka nakubatiza hapo ziwa michigan baada ya hapo nakupakia kwenye kontena safari ni moja hadi bongo kwa mzee wa Upako ukawe mpanga viti[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Yote hayo unajitakia.

Fanya kazi, maliza nenda restaurant kamata msosi sepa nyumbani.

Ukiendekeza usela ndo upuuzi unapoanzia.

Lakini, wabongo tufanye vitu halali. Hata wakiwashtua polisi, huna cha kuogofya. Lakini kama una mapindo pindo yako ndiyo utaumia.

Upuuzi mtupu.
 
Boundaries is a foreign concept.

Si ndiyo unaona mpaka hapa JF mtu hakujui anajipa uhuru kwamba anakujua sana mpaka kukuita muongo.

Kwa watu wanaojua kufikiri hilo ni tusi kubwa sana.

Halafu kituko, huyo anayekuita muongo kiholela ndiye anayelalamika kuwa Watanzania hawana msaada.

Ninaweza kuelewa kwa nini watu hawamsaidii mtu asiye na adabu hivi. Mtu mwenye a false sense of entitlement hivi. Mtu mwenye mawazo negative hivi.

Achague moja, kuomba msaada au kufanya ujeuri.

Viwili hivi haviendi pamoja.
Mtu wa namna hio anatia mashaka au hayupo serious bali kutafuta attention kwa watu.
 
Kuna level fulani ya mazoea inabidi iwepo ku maintain maisha mazuri na jamii, yani mtu kujikata kabisa ni vigumu na haifai.

Na pia, mazoea yakizidi sana inakuwa tatizo.

Kwa hivyo hapo inabidi mtu kujua kuweka balance nzuri, asizoeleke sana na pia asijitenge sana.

Mimi nilikuwa na deal na mtu mmoja tu ambaye yupo katikati ya jumuiya ya wabongo anayejua kila kitu kinachoendelea, na kitu chochote muhimu nitapata kutoka hapo.

Zaidi ya hapo BBQ za jamii kidogo tu, kujua nani kaja na nani kaondoka etc.

Vinginevyo nduki kubwa sana kwenye mambo yangu.

Siku hizi hata hizo community BBQ siendi nafanya BBQ zangu mwenyewe on my deck.
Mimi nilishindwa kabisa kuwa karibu na ndugu zangu wakibongo mkuu.

Niliishi kwenye jamii ya wazungu tupu ngozi nyeusi nilikua mim tu hadi nikipita unakuta mtoto ananishangaa ananinyooshea kidole🤣.Mwanzoni niliona upweke na nilimiss kuongea kiswahili na mtu wa kula nae ugali wa kulumangia🤣.

Nikahangaika mpaka nikapata rafiki wa kitanzania.Siku ya siku akanipeleka kwenye party ya kitanzania ila ile party ilinivunja moyo na nikaapa sitaenda tena party za wabongo.Kwanza kwenye ile party kulikua na team mbili za maadui.Kulikua na vitu vya ajabu ajabu vinaendelea kule ndani.Mtu wa kundi A akipita kundi B wanamcheka na kuchamba (Buza style).Mtu wa kundi B akinyanyuka kucheza kundi A anaenda kujiganya anacheza then anamkanyaga makusudi wanazozana wanatulia kidogo ila mwishowe zogo kubwa likatokea jikoni,watu wakamwagiana uji wa ugali.Zogo likawa kubwa likaja mpaka ukumbini.Watu wakaanza kurushiana viti na chupa.Kipande kikanikata chini ya jicho.Nguo zote zikaloa damu.Hadi leo nina alama🤣.
Nilipomuuliza rafik yangu ile vita ilisababishwa na nin nikawa hata simuelew anachonieleza.Mara yule mama mweusi mnene alimleta bwanake kutoka bongo ila alivyopata makaratas tu akamuacha akaenda kumuoa yule msichana ambae ni shangaz wa yule alomkanyaga yule kaka kwa makusud.Mara yule dada ni mmbea sana anatoa siri za mwenzake wakat mwenzake kamsaidia wakat hana pa kukaa.Mara unamuona yule mdada mweupe anajidai kweli halafu anadanganya watu anavaa designer staff kumbe mafeki akiambiwa anakua mkali.Mara yule kamchomea kaka yake yule mpaka akarudishwa bongo.

Baada ya muda nikaona mim na huyo rafiki yangu hatuendani kwa mambo mengi nikamkatia na sikuwa tena na ukaribu na wabongo.
Na hata ningefia kule hakuna mbongo angekuja kwenye mazishi yangu.Ningezikwa na wazungu,wanigeria,waserbia na wa Iran.
Nilijitenga sana na hakuna mbongo aliyenijua.
 
Lengo la hilo swali dhumuni lake ni lipi hasa?
Lengo ni kujua kama ni kweli mwenza anayekusaidia au unayemsaidia kupata permit ni mwenza wako kweli au ni mchongo.Ukisema ulipiga goli tatu mwenza akasema nne au moja inakua tabu.Wanauliza hadi rangi ya mswaki au perfume au chochote tu ambacho huwezi kujua kama huishi na huyo mtu
 
Lengo la hilo swali dhumuni lake ni lipi hasa?

Sijawahi kusikia hilo swali. Ila maswsli mengine ni ya kizushi kumpima mtu tu.

Kuna dada mdogo wangu alienda kuomba visa ubalozi wa US, kuja US kututembelea ndugu zake likizo.

Yule Consular akawa analeta maswali invasive ambayo mdogo wangu aliona yanamvunjia utu.

Yule mdogo wangu akamwambia Consular naomba passport yangu niondoke sasa hivi, na hiyo safari yenyewe nishaghairi, naenda kusalimia tu si safari ya lazima hivyo.

Ikabidi Consular amuombe msamaha na kumgongea visa.

Kuanzia siku hiyo hajapata tatizo visa ya Marekani.

Mara nyingine tunavyoyachukulia haya maswali kuwa ni lazima kuyajibu kama yalivyoulizwa inatusababishia matatizo zaidi.

Yule dada yangu mdogo kwa kumuonesha Consular kwamba hayupo desperate hivyo kwenda Marekani, na kwamba ni mtu mwenye confidence ya kuishi maisha vizuri bila kwenda Marekani, alimtoa yule Consular wa ubalozi wa US wasiwasi kwamba, huyu akienda Marekani atarudi Tanzania?

Hilo swali ni swali kubwa sana wanalofikiria kabla ya kutoa visa.

Yule dada mdogo alionekana kujiamini sana na maisha yake Tanzania, na alionekana ana logical consistency kwamba anaenda Marekani kusalimia tu, akimaliza anarudi Tanzania, so it's not a big deal, mpaka Consular akamuomba msamaha kwa kuuliza maswali invasive yaliyomvunjia heshima kwa kutoamini kwamba akienda Marekani atarudi Tanzania.
 
Nonsense.

Huwezi kuchomwa kama mambo yako yapo clean. Huwezi kuwa unafanya legal business na upo documented afu uchomwe. Uchomwe kwa misingi gani? Hadi uchomwe ina maana haupo clean. Nje hushikwi kiboya boya kama police hawana grounds za kukushika. Hilo haliwezekani.

Kama watu unaokaa nao wana tabia za majungu na umbea hapo tatizo ni wewe mwenyewe. Watu wambea wapo kwenye kila jamii ni wewe unavyochagua kuishi nao. Kama hutaki umbea huwezi kupata umbea. If you don't tolerate majungu hutosikia majungu. Tunaishi na wabongo wenzetu kwa amani na upendo, kwenye shida na raha bila shida yeyote ile. Nyie mabaharia mnachaguana masela mavi ndo maana hampatani afu mnakuja kutukana wabongo wote. Kama hutaki kujumuika na wabongo wenzio it's all good hakuna kinachoongoezeka wala kupungua.
 
Lengo ni kujua kama ni kweli mwenza anayekusaidia au unayemsaidia kupata permit ni mwenza wako kweli au ni mchongo.Ukisema ulipiga goli tatu mwenza akasema nne au moja inakua tabu.Wanauliza hadi rangi ya mswaki au perfume au chochote tu ambacho huwezi kujua kama huishi na huyo mtu
Noma sana.
 
Sijawahi kusikia hilo swali. Ila maswsli mengine ni ya kizushi kumpima mtu tu.

Kuna dada mdogo wangu alienda kuomba visa ubalozi wa US, kuja US kututembelea ndugu zake likizo.

Yule Consular akawa analeta maswali invasive ambayo mdogo wangu aliona yanamvunjia utu.

Yule mdogo wangu akamwambia naomba passport yangu niondoke sasa hivi, na hiyo safari yenyewe nishaghairi, naenda kusalimia tu si safari ya lazima hivyo.

Ikabidi Consular amuombe msamaha na kumgongea visa.

Kuanzia siku hiyo hajapata tatizo visa ya Marekani.

Mara nyingine tunavyoyachukulia haya maswali kuwa ni lazima kuyajibu kama yalivyoulizwa inatusababishia matatizo zaidi.

Yule dada yangu mdogo kwa kumuonesha Consular kwamba hayupo desperate hivyo kwenda Marekani, na kwamba ni mtu mwenye confidence ya kuishi maisha vizuri bila kwenda Marekani, alimtoa yule Consular wa ubalozi wa US wasiwasi kwamba, huyu akienda Marekani atarudi Tanzania?

Hilo swali ni swali kubwa sana wanalofikiria kabla ya kutoa visa.

Yule dada mdogo alionekana kujiamini sana na maisha yake Tanzania, na alionekana ana logical consistency kwamba anaenda Marekani kusalimia tu, akimaliza anarudi Tanzania, so it's not a big deal, mpaka Consular akamuomba msamaha kwa kuuliza maswali invasive yaliyomvunjia heshima kwa kutoamini kwamba akienda Marekani atarudi Tanzania.

Kuna watu washaulizwa hilo swali na mengine mengi kama hayo mkuu.
Kwa kigezo cha kwenda kusalimia ni lazima wapate uhakika kuwa utarudi na alichofanya mdogo wako kilikua kizuri sana kisaikolojia ila angekua anaomba visa kwa kigezo cha kwenda kuishi na mwenza hilo swali lazima angetakiwa alijibu mkuu na iwapo angepanick au angekataa kisaikolojia ingekua sio nzuri kwake.
 
Siyo vizuri kuwa kisiwa. Ni vizuri kushosolaiz na kujichanganya kigumu hivyo hivyo.

Kuna nature kama kifo na kuuguwa. Japo mibongo mingi ni mitambo ya umbea hivyo hivyo tu itasaidia.

Lakini tabia zetu mtoni ni mbofumbofu na kukera.
Kweli wabongo wengi ni mipuzi mipuzi sana wakiwa huku mamtoni. Ndio maana tunaogopa kuwakaribisha magetoni kwetu kuepuka fedheha.

Acha niendelee kula porpcon hapa Venice Beach, Walatino midemu kama wote vile. Baadae nipitie mitaa ya kubarizi Santa Monica.

Wengi watasema wabongo tuliopo huku tuna roho mbaya, kumbe tabia zetu zimepinda.
 
Yaani wabongo ni watu wa ajabu sana yaani wao wamekalia majungu, chuki, unafiki na ukora tu yaani wao wakiona mwenzao amewazidi kwa chochote kile wanaanza kukupiga majungu nasema hii tabia mkiendelea nae nitamuua mtu hivi hivi kwa ujinga na uzandiki wenu

Ndio maana mie huwaga napenda kujitenga na wabongo aisee yaani ni watu ambao wamekalia majungu, unafiki, uzandiki pamoja na ukora tu.

Juzi kuna watu wabongo wajinga wamemchoma mwenzao mpaka ameenda kwa sello kisa jamaa mambo yake yanaenda na anapiga hela nyingi kwahiyo wajamaa wameamua kumchoma upuuzi! Nyie wabongo tabia yenu ya kipuuzi huko kwenu ukimani [emoji1005] muiachane huko huko [emoji205]

[emoji205] [emoji205] [emoji205] [emoji205] [emoji205] [emoji1005] [emoji1005] [emoji1005] [emoji1005] [emoji1005]
Kuna kaukweli fulani hivi kwa zaidi ya 80%.
 
Sijawahi kusikia hilo swali. Ila maswsli mengine ni ya kizushi kumpima mtu tu.

Kuna dada mdogo wangu alienda kuomba visa ubalozi wa US, kuja US kututembelea ndugu zake likizo.

Yule Consular akawa analeta maswali invasive ambayo mdogo wangu aliona yanamvunjia utu.

Yule mdogo wangu akamwambia naomba passport yangu niondoke sasa hivi, na hiyo safari yenyewe nishaghairi, naenda kusalimia tu si safari ya lazima hivyo.

Ikabidi Consular amuombe msamaha na kumgongea visa.

Kuanzia siku hiyo hajapata tatizo visa ya Marekani.

Mara nyingine tunavyoyachukulia haya maswali kuwa ni lazima kuyajibu kama yalivyoulizwa inatusababishia matatizo zaidi.

Yule dada yangu mdogo kwa kumuonesha Consular kwamba hayupo desperate hivyo kwenda Marekani, na kwamba ni mtu mwenye confidence ya kuishi maisha vizuri bila kwenda Marekani, alimtoa yule Consular wa ubalozi wa US wasiwasi kwamba, huyu akienda Marekani atarudi Tanzania?

Hilo swali ni swali kubwa sana wanalofikiria kabla ya kutoa visa.

Yule dada mdogo alionekana kujiamini sana na maisha yake Tanzania, na alionekana ana logical consistency kwamba anaenda Marekani kusalimia tu, akimaliza anarudi Tanzania, so it's not a big deal, mpaka Consular akamuomba msamaha kwa kuuliza maswali invasive yaliyomvunjia heshima kwa kutoamini kwamba akienda Marekani atarudi Tanzania.
Angekuwa kijana wa kiume na temper ipo karibu ngumi ingerushwa😂
 
Kuna watu washaulizwa hilo swali na mengine mengi kama hayo mkuu.
Kwa kigezo cha kwenda kusalimia ni lazima wapate uhakika kuwa utarudi na alichofanya mdogo wako kilikua kizuri sana kisaikolojia ila angekua anaomba visa kwa kigezo cha kwenda kuishi na mwenza hilo swali lazima angetakiwa alijibu mkuu na iwapo angepanick au angekataa kisaikolojia ingekua sio nzuri kwake.
Kwa Marekani Visa ya kwenda kuishi na mwenza ni rahisi kuliko visa ya kusalimia au kusoma.

Kwa sababu visa ya kwenda kuishi na mwenza ni immigrant visa, si non immigrant visa.

Immigrant visa unakuwa ushaazimia kuwa unaenda kuishi Marekani, hivyo hapo hakuna swali kama utarudi Tanzania au la. Visa yenyewe ni ya kwenda kuishi Marekani na kuhamia huko.

Labda hii visa inaweza kuwa tatizo kwenye nchi zinazojulikana kwa utapeli kama Nigeria.

Kwanza Tanzania visa hizo si nyingi, pili wanakuwa wana deal na mtu wao ambaye mara nyingi anakuwa raia wao, vitu muhimu watakavyohitaji ni uwe certified na wizara ya mambo ya ndani kuwa huna uhalifu, huyo mwenza awe na documents za kulipa kodi miaka mitatu na awe na uwezo wa kuku support, na sanasana watauliza kama unajua Kiingereza vizuri.

Hapo wakileta uzushi wanajua wana deal na raia wao ambaye anaweza kuwadhibiti Kimarekani huko kwao.
 
Kwa asili, mwanadamu ni kiumbe mwenye chuki dhidi ya mwanadamu mwingine pengine kuliko viumbe wengine. Katika mazingira ya kawaida, kuwa makini sana unapoishi (interact) na wanadamu wengine. Isipokuwa, mwanadamu huyu anaweza kuzidhibiti hizi chuki na kujitengeneza upya kwa kujiongezea maarifa ya namna ya kuachana na hizi chuki.

Mie huko nyuma kuna watu nimewahi kuwachukia bila hata sababu za msingi kabisa.. Mfano: kwa sababu tu mtu mmoja alipata fursa flani bila ya kunishirikisha na mimi, nikawa nimechukia. Yaani nikafanya kuwa jambo la yeye kunishirikisha ni jambo la lazima na si hiyari yake, na wakati huo huo sikuwahi hata kumuuliza wala kumuomba msaada. Baada ya kuongeza maarifa nikauona upumbavu wangu na kuamua kubadilika. Nilikuwa mpumbavu sana huko nyuma. Sanasana ukiwa maskini wa maarifa unakuwa mpumbavu zaidi - usipokuwa makini (si maskini wote lakini).
 
Back
Top Bottom