Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mimi suala hili limenifikirisha sana.Ndio Mkuu. Tunaweza kuhitimisha kwa kusema ni muhimu sana mtu kutafuta kujiongezea maarifa mengi zaidi kwenye haya maisha. Watu tusiishie kuwa na maarifa ya careers zetu pekee. Bali tutafute na maarifa mengine mengi yanayohusu maisha ya mwanadamu hapa duniani. Ukiangalia anachokilalamikia ndugu mleta mada ni matokeo ya watu kutokuwa na maarifa ya maisha. Usipokuwa na maarifa ndio utamchukia mtu, unakuwa mtu mwenye wivu, utaseng'enya sana, utakuwa muongo muongo, mpika majungu, mbabaishaji, usiyeaminika n.k.
Ni bahati mbaya sana kwamba watu wengi hawapendi kujiongezea maarifa.
Wengi wameona kwamba kwenda nje ndiyo mafanikio. In a very desperate way.
Kwa namna fulani tumeshakubali kwamba nchi yetu imeoza.
Na hata sisi tulio nje wengi hatutaki kurudi kwetu.
Kwa sababu tumekubali nchi yetu imeoza.
Kwa namna fulani tushakubali kwamba hatuwezi kuibadilisha nchi yetu iwe nzuri vya kutosha, tusione kwamba ni lazima tukimbilie ughaibuni.
Haya ni mambo ya aibu kwa kweli.
Inawezekana nikaonekana nafanya falsafa za mpataji, lakini, kimsingi, mimi kama mpenzi wa "questioning the premise" ni maswali ya kufikirisha sana.
Kwa nini Watanzania wengi wasiweze kufurahia mafanikio nchini mwao, mpaka waone maisha mazuri yanapatikana ughaibuni tu?