Wabongo mkija majuu au ughaibuni acheni unafiki, majungu na ukora mnaliabisha Taifa lenu

Ndio Mkuu. Tunaweza kuhitimisha kwa kusema ni muhimu sana mtu kutafuta kujiongezea maarifa mengi zaidi kwenye haya maisha. Watu tusiishie kuwa na maarifa ya careers zetu pekee. Bali tutafute na maarifa mengine mengi yanayohusu maisha ya mwanadamu hapa duniani. Ukiangalia anachokilalamikia ndugu mleta mada ni matokeo ya watu kutokuwa na maarifa ya maisha. Usipokuwa na maarifa ndio utamchukia mtu, unakuwa mtu mwenye wivu, utaseng'enya sana, utakuwa muongo muongo, mpika majungu, mbabaishaji, usiyeaminika n.k.
Ni bahati mbaya sana kwamba watu wengi hawapendi kujiongezea maarifa.
Mimi suala hili limenifikirisha sana.

Wengi wameona kwamba kwenda nje ndiyo mafanikio. In a very desperate way.

Kwa namna fulani tumeshakubali kwamba nchi yetu imeoza.

Na hata sisi tulio nje wengi hatutaki kurudi kwetu.

Kwa sababu tumekubali nchi yetu imeoza.

Kwa namna fulani tushakubali kwamba hatuwezi kuibadilisha nchi yetu iwe nzuri vya kutosha, tusione kwamba ni lazima tukimbilie ughaibuni.

Haya ni mambo ya aibu kwa kweli.

Inawezekana nikaonekana nafanya falsafa za mpataji, lakini, kimsingi, mimi kama mpenzi wa "questioning the premise" ni maswali ya kufikirisha sana.

Kwa nini Watanzania wengi wasiweze kufurahia mafanikio nchini mwao, mpaka waone maisha mazuri yanapatikana ughaibuni tu?
 
Mkuu,

Ogopa sana mtu anayeamini uwepo wa Mungu.

Nitakupa story moja.

Siku moja tulikuwa tunapiga story group la Whatsapp la shule.

Ghafla, mwenzetu mmoja akawa analalamila kuwa anaumwa sana.

Sasa, katika lile group, watu karibu wote wanasema wanaamini Mungu. Watu wakaanza yale maneno yao ya imani. Yale maneno ya "tunakuweka katika maombi" "Mungu atakulinda" na maneno kama hayo.

Huko yule mwenzetu anaumwa sana, anatokwa na damu.

Basi mimi nisiyeamini katika uwepo wa Mungu, nikasema Mungu hawezi kusaidia hapa, kwa sababu hayupo.

Nikasema ni wajibu wetu kusaidiana wenyewe sisi watu.

Nikatuma muamala kwa dada mmoja yeye alikuwa ana muda wa kuzunguka chapchap. Akachukua gari, akaenda kwa yule rafiki yetu. Akampeleka hospitali, tena kulikuwa na rafiki yetu humo humo kwenye group daktari hospitali kubwa tu.

Kufika hospitali, yule rafiki yetu daktari akamsaidia mgonjwa, zile hela nilizotuma zikawapa motisha na wale wengine wa "tutakuombea dua" na "Mungu atakuponya" wafuatishe kuchangia, yule rafiki yetu akakatiwa bima ya afya.

Yule rafiki yetu daktari alisema huyu mtu tungechelewa kidogo tu angetuacha, angeaga dunia.

Yani hapo unaweza kuona kabisa imani ya Mungu inavyoweza kuhatarisha maisha ya mtu. Kuna kazi inatakiwa kufanywa na watu, watu wanamuachia kazi Mungu.

Mimi nilikataa ujinga huo wa kumuomba Mungu nikasema hii ni kazi yetu, tuache kumtegea Mungu ambaye hayupo.

Mungu angekuwepo hata magonjwa yasingekuwepo.

Kwa hiyo, ogopa sana mtu anayeamini Mungu.

Anaweza kukuona unakufa kwa kuhitaji msaada, akamuachia Mungu kazi ya kukusaidia. Akasema tu "nakuombea kwa Mungu" na "Mungu atakusaidia".

Sent from my SM-S908U1 using JamiiForums mobile app
Hapo ulikuwa sahihi kabisa

Tatizo letu sisi wa Africa tuna tatizo la kukwepa majukumu yetu na kumwachia Mungu, kitu ambacho sio sahihi
 
Ila wabongo wanachomana sana. Wanawapigia hadi polisi na migration kukuchongea eti urudishwe.

Halafu kuna katabia na hulka flani ka umaskini wabongo wanayo hadi mton. Msosi mtoni siyo big deal lakini eti wanashindana kujaza friji msosi na kuringishiana unabaki kushangaa tu Wtf!

Watu gani hao unaokaa nao hadi mnaringishiana misosi kwenye fridge? Hii tabia hata bongo haipo. This says more about you kuliko hao watu.
 
Mpuuzi wewe na hao wabongo wenzako, Waarabu wa Pemba hujuana kwa Vilemba.

Exactly. If you don't tolerate majungu na umbea huwezi letewa majungu. Hawa watu wenyewe wanapenda majungu na umbea ndo maana wanakutana na wenzao wenye hizo tabia.

Tunaishi na wabongo wenzetu vizuri tu kwa amani na upenda hamna majungu wala umbea.
 
Watanzania wengi hawana akili

Nimewahi kusema hapa ya kwamba huko nje kuna fursa kibao ila huwezi ona watanzania waishio huko akiwemo Kiranga wanakusanua kuhusu hilo,wao wamekalia ujinga na uzwazwa tu.

Ukiuliza fursa huko utaambiwa maisha ni magumu kwa kulipa bills,yaani kila ukiluza utaambiwa bills ni tatizo.

KWA KIFUPI.

WATANZANIA WENGI WAISHIO NJE HUKO HASA MAREKANI NI WAJINGA NA MAZUMBUKUKU

Wewe mwenye akili umefika wapi? Kwanini usitumie akili zako kufika nje bila msaada wa mtu?

Nani mwenye akili zaidi wewe uliyeshindwa kufikia malengo yako ya kufika nje au aliyefika nje bila kushikwa mkono?

Kama wengine wamefika bila kushikwa mkono wewe kwanini hujafika?

Unaweza pewa information zote at the end of the day ni kazi yako kupambana na hali yako. Hamna mtu ataenda kukuombea PP, visa au kukukatia ticket ya ndege. Information zote zipo online na tume-share sana information humu JF. Kazi kwako.

Yaani wabongo ni watu wa ajabu sana, yaani wao wamekalia majungu, chuki, unafiki na ukora tu. Yaani wao wakiona mwenzao amewazidi kwa chochote kile wanaanza kukupiga majungu, nasema hii tabia inakera.

Ndio maana mie huwa napenda kujitenga na wabongo, aisee yaani ni watu ambao wamekalia majungu, unafiki, uzandiki pamoja na ukora tu.

Juzi kuna watu wabongo wajinga wamemchoma mwenzao mpaka ameenda kwa sello kisa jamaa mambo yake yanaenda na anapiga hela nyingi, kwahiyo wajamaa wameamua kumchoma, upuuzi! Nyie wabongo tabia yenu ya kipuuzi huko kwenu muiachane huko huko.
LE Mutuz kafufuka?
 
Hapo ulikuwa sahihi kabisa

Tatizo letu sisi wa Africa tuna tatizo la kukwepa majukumu yetu na kumwachia Mungu, kitu ambacho sio sahihi
Kuna wakati nilikuwa nafikiri labda ni suala la uwezo wa kiuchumi.

Kwamba mtu ambaye hawezi kutuma muamala akistukizwa, akitaka kuonesha ushirikiano, ndiyo anatoa dua zake. Mungu anakuwa ni kama kihadithi fulani cha kuunganisha jamii.

Lakini baadaye nikaona kuna ubinafsi pia, haiwezekani watu wote muwe hamko sawa.

Sasa, ironically, ikatokea kwamba, wale wanaojinadi kuwa wacha Mungu wameshindwa kuonesha upendo unaohubiriwa na dini, halafu mtu mmoja ambaye haamini kabisaa katika uwepo wa Mungu, haamini katika thawabu na dhambi kidini, ndiye akaanzisha kuonesha upendo huo kwa vitendo.

Ndiyo maana na challenge habari za "ogopa mtu asiyeamini Mungu"

Dunia ina mambo sana hii.
 
Hao walimsingizia Mungu sababu ya uchoyo tu wakumsaidia mgonjwa,

coz hata doctor alikaa kimya wakati yeye ilitakiwa awe wa kwanza kutoa msaada,

Kuhusu uwepo wa Mungu ni mjadala mpana sana mkuuu kiranga, tuuache tuu

But mi naamini yupo, ila siiamini dini yoyote ile
 
Nawaulumia washindi wa green lottery wakibugi step tu wamepotea aisee
Okay, safi sana, uzuri wa wanaopata green lottery wanapata mafunzo kidogo wakifika huko. Lakini ni vyema sana nasi kama tunawafahamu tuwakumbushe kama hayo niliyoyafahamisha hapo juu.

Binafsi nimeishi maisha ya ujana wangu wote nchi za nje, nafahamu ninachokishauri.
 
Kote kote wanaangalia hivyo vitu kwenye suala la kwenda kuishi na mwenza ila (sijui kwa marekani) kwa nchi za Scandnavia ukishapata visa ya kwenda kuishi na mwenza wako sio kama ndio ushamalizana nao bali baada ya miaka miwili wewe na mwenza wako mtaitwa kwenye interview ya mwisho yenye lengo la kuwapatia permanent residence permit.
Na iwapo imetokea mmeachana kabla ya hiyo miaka miwili mgeni anaweza kurudishwa nchini kwao.
Hilo swali sio la kawaida na ndo mana nimelitumia kama mfano na walioulizwa hilo swali hawakupewa hiyo permit.

Wanaouliza hayo maswali wanacheza zaidi na saikolojia na kila swali wanalouliza wanakua na sbb ya kuliuliza na huwa hawazingatii majibu tu wanaangalia vitu vingi.
Hata Marekani wana system ya kuuliza, na wanafanya interview baada ya miaka miwili, ingawa mara nyingi wana iondoa (waive).

Ila sidhani kama wana maswali kama hayo ya ndani kabisa. Marekani wana sheria kali sana za sexual harassment na maswali ya mnapigana bao ngapi hayo ni zaidi ya uzushi hayo yanakwenda kuondoa dignity ya mtu sasa.

Wanauliza tu vacation mnaenda wapi? Mara ya mwisho kwenda out mmeenda wapi? Na maswali kama hayo. Kama hujawapa sababu ya kuwa suspicious wana assume kwamba mko pamoja kweli.

Kuna jamaa mmoja MSenegal alioa Mmarekani mmoja matata sana, akaja kugombana na mkewe kabla ya miaka miwili kuisha, akahama kabisa pale kwake. Ila alitumiwa green card palepale akaenda kuichukua, hata hawakumuita kwenye interview. Baadaye akamtaliki mkewe.

Na miaka kadhaa baadaye alikwenda ku renew green card baada ya kumtaliki mkewe, wala hawakumuuliza kuhusu mke wake kwa sababu huko green card ilikuwa yake.

So, kwa mimi nilivyoona, Wamarekani kama hujawapa sababu ya kukufuatilia, na ndoa haina police/ court cases, huwa hawafuatilii sana.
 
Mimi suala hili limenifikirisha sana.

Wengi wameona kwamba kwenda nje ndiyo mafanikio. In a very desperate way.

Kwa namna fulani tumeshakubali kwamba nchi yetu imeoza.

Na hata sisi tulio nje wengi hatutaki kurudi kwetu.

Kwa sabau tumekubali nchi yetu imeoza.

Kwa namna fulani tushakubali kwamba hatuwezi kuibadilisha nchi yetu iwe nzuri vya kutosha, tusione kwamba ni lazima tukimbilie ughaibuni.

Haya ni mambo ya aibu kwa kweli.

Inawezekana nikaonekana nafanya falsafa za mpataji, lakini, kimsingi, mimi kama mpenzi wa "questioning the premise" ni maswali ya kufikirisha sana.

Kwa nini Watanzania wengi wasiweze kufurahia mafanikio nchini mwao, mpaka waone maisha mazuri yanapatikana ughaibuni tu?
Sikutaka kuzungumza kwa undani sana juu ya hili ulilosema Mkuu. Ila itoshe kusema kuwa unachosema ni sahihi kabisa na nimekuwa nikikisema sana kwa jamaa zangu wanaopenda sana kufika ughaibuni ili watoboe kimaisha. Ukiwaambia hali halisi ili wafanye maamuzi kulingana na uhalisia ulivyo wanaishia kusema ' wewe hupendi wenzako wafanikiwe ndio maana hutaki wafike ughaibuni'.

Wao wanapenda kuambiwa mambo rahisirahisi tu. Mfano kwa sasa Ulaya kuna wimbi kubwa la wakimbizi na hata hizo kazi za box zimekuwa za taabu. Nchi kama Netherlands ni very innovative kwenye job creation ila kazi za box zimeanza kuwa ngumu. Nchi nyingi zinaendelea kuweka masharti magumu ya kuingia ili kudhibiti mafuriko ya watu wanaoingia. Juzi tu UK wameweka bans kwa Nigerians wanaoenda kusoma kuleta wenza wao kuanzia January mwakani.

Ila eti unakuta mtu yupo tayari kutumia karibia 20-50M ili afike ughaibuni. Hajui akifika anafanya kazi gani na atafanikiwa baada ya muda gani. Yeye anachotaka ni kufika tu Ulaya. Wakati akiwa na hizo pesa anaweza kubakia nyumbani na akafanya jambo na akatoboa vizuri tu. Kisha akawa anakuja Ulaya kutalii ama kufanya biashara endapo atakuwa na mtaji wa kutosha. Hivi mfano ukitumia 20M kununua Ng'ombe wa maziwa nyumbani labda wawe Ng'ombe 20, baada ya miaka mitano utakuwa katika hali gani? Badala watu walete mada tushirikishane maarifa ya namna ya kutumia fursa za nyumbani kujiletea maendeleo wao wamekariri stories za miaka ya 90's kwamba maisha yapo ughaibuni pekee.

Wakati watu wanaishia kuishi maisha ya kuunga unga na hawana uhakika hata wa kuhuisha resident permits zao zinapoisha muda wake. Mwishowe wanaishia kuwa scammers kama wafanyavyo Nigerians. Mie nitamuelewa jobless pekee aliyeko bongo na akafanyiwa mpango wa kufika ughaibuni ili angalau afike na afanye hizo kazi za vibarua ambazo bongo hazipo. Ila nitam-challenge huyo mtu endapo zitatumika pesa zaidi ya 20-30M kumsaidia ili afike tu ughaibuni. Sasa unakuta mtu mzima mwenye familia anateketeza karibia 50M afike Ulaya ambako hata uhakika wa kazi ya kufanya hana. Yaani kakariri tu kwamba akifika Ulaya tayari anatoboa maisha. Huku ndiko kudhani kila mzungu anafahamu English sawasawa. Ama kila Mzungu ni tajiri. Kumbe na wao kuna walio choka tu.

Sasa unamwambia mtu, ughaibuni unakosema si lelemama kama unavyodhani. Si jambo lakufika na kufanikiwa kwa muda mfupi unaodhani. Ukweli ni kuwa watu wanaofika ughaibuni, wanaotoboa ni wachache ukilinganisha na wenye maisha ya kuunga unga. Na ndio maana watu wengi hawapendi kabisa kuja hata nyumbani. wanaishia tu kupiga picha za kwenye barabara nzuri na majengo mazuri wakati wa summer ili waonekane wanaishi pazuri huku usiku unapofika anaenda kulala kwenye chumba kimoja cha kubanana watu zaidi ya wanne. Yaani unakuta watu wengi wanaishi maisha ya kawaida tu na pesa zao zinaishia kulipa bills kama mdau mmoja aliyesema hapo juu. Watu wengi waliotoboa ni wale walioishi miaka mingi na wakapata nafasi ya kupata kazi nzuri sehemu nzuri. Sio hizi za vibarua vya kuunga unga ambavyo utaishia kulipia bills tu. Labda kwa Marekani maana sijawahi kufika. Ila siyo kwa Ulaya nilikofika.
 
Sikutaka kuzungumza kwa undani sana juu ya hili ulilosema Mkuu. Ila itoshe kusema kuwa unachosema ni sahihi kabisa na nimekuwa nikikisema sana kwa jamaa zangu wanaopenda sana kufika ughaibuni ili watoboe kimaisha. Ukiwaambia hali halisi ili wafanye maamuzi kulingana na uhalisia ulivyo wanaishia kusema ' wewe hupendi wenzako wafanikiwe ndio maana hutaki wafike ughaibuni'.

Wao wanapenda kuambiwa mambo rahisirahisi tu. Mfano kwa sasa Ulaya kuna wimbi kubwa la wakimbizi na hata hizo kazi za box zimekuwa za taabu. Nchi kama Netherlands ni very innovative kwenye job creation ila kazi za box zimeanza kuwa ngumu. Nchi nyingi zinaendelea kuweka masharti magumu ya kuingia ili kudhibiti mafuriko ya watu wanaoingia. Juzi tu UK wameweka bans kwa Nigerians wanaoenda kusoma kuleta wenza wao kuanzia January mwakani.

Ila eti unakuta mtu yupo tayari kutumia karibia 20-50M ili afike ughaibuni. Hajui akifika anafanya kazi gani na atafanikiwa baada ya muda gani. Yeye anachotaka ni kufika tu Ulaya. Wakati akiwa na hizo pesa anaweza kubakia nyumbani na akafanya jambo na akatoboa vizuri tu. Kisha akawa anakuja Ulaya kutalii ama kufanya biashara endapo atakuwa na mtaji wa kutosha. Hivi mfano ukitumia 20M kununua Ng'ombe wa maziwa nyumbani labda wawe Ng'ombe 20, baada ya miaka mitano utakuwa katika hali gani? Badala watu walete mada tushirikishane maarifa ya namna ya kutumia fursa za nyumbani kujiletea maendeleo wao wamekariri stories za miaka ya 90's kwamba maisha yapo ughaibuni pekee.

Wakati watu wanaishia kuishi maisha ya kuunga unga na hawana uhakika hata wa kuhuisha resident permits zao zinapoisha muda wake. Mwishowe wanaishia kuwa scammers kama wafanyavyo Nigerians. Mie nitamuelewa jobless pekee aliyeko bongo na akafanyiwa mpango wa kufika ughaibuni ili angalau afike na afanye hizo kazi za vibarua ambazo bongo hazipo. Ila nitam-challenge huyo mtu endapo zitatumika pesa zaidi ya 20-30M kumsaidia ili afike tu ughaibuni. Sasa unakuta mtu mzima mwenye familia anateketeza karibia 50M afike Ulaya ambako hata uhakika wa kazi ya kufanya hana. Yaani kakariri tu kwamba akifika Ulaya tayari anatoboa maisha. Huku ndiko kudhani kila mzungu anafahamu English sawasawa. Ama kila Mzungu ni tajiri. Kumbe na wao kuna walio choka tu.

Sasa unamwambia mtu, ughaibuni unakosema si lelemama kama unavyodhani. Si jambo lakufika na kufanikiwa kwa muda mfupi unaodhani. Ukweli ni kuwa watu wanaofika ughaibuni, wanaotoboa ni wachache ukilinganisha na wenye maisha ya kuunga unga. Na ndio maana watu wengi hawapendi kabisa kuja hata nyumbani. wanaishia tu kupiga picha za kwenye barabara nzuri na majengo mazuri ili waonekane wanaishi pazuri huku usiku unapofika anaenda kulala kwenye chumba kimoja cha kubanana watu zaidi ya wanne. Yaani unakuta watu wengi wanaishi maisha ya kawaida tu na pesa zao zinaishia kulipa bills kama mdau mmoja aliyesema hapo juu. Watu wengi waliotoboa ni wale walioishi miaka mingi na wakapata nafasi ya kupata kazi nzuri sehemu nzuri. Sio hizi za vibarua vya kuunga unga ambavyo utaishia kulipia bills tu. Labda kwa Marekani maana sijawahi kufika. Ila siyo kwa Ulaya nilikofika.
Mkuu,

Shukurani sana kwa kuweka sawa. Inabidi tusikie pande zote.

50M mtaji mkubwa tu kwa mtu anayejua kuzungusha hela bongo.

Ila unafikiri kuwa tuna matatizo ya kijamii yaliyopita hata kiuchumi tu, kwamba watu wanaona rushwa, kuoneana, unapigwa kodi na TRA kabla hujaanza biashara, nchi haina uhuru, etc, na mambo haya yanakuwa yanawaelemea hata watu wenye mitaji kama huo wa 50M, wakipiga jura zinavurugwa, wanaona bora wapige kura kwa miguu tu kutafuta maisha nje ya nchi?
 
Hata Marekani wana system ya kuuliza, na wanafanya interview baada ya miaka miwili, ingawa mara nyingi wana iondoa (waive).

Ila sidhani kama wana maswali kama hayo ya ndani kabisa. Marekani wana sheria kali sana za sexual harassment na maswali ya mnapigana bao ngapi hayo ni zaidi ya uzushi hayo yanakwenda kuondoa dignity ya mtu sasa.

Wanauliza tu vacation mnaenda wapi? Mara ya mwisho kwenda out mmeenda wapi? Na maswali kama hayo. Kama hujawapa sababu ya kuwa suspicious wana assume kwamba mko pamoja kweli.

Kuna jamaa mmoja MSenegal alioa Mmarekani mmoja matata sana, akaja kugombana na mkewe kabla ya miaka miwili kuisha, akahama kabisa pale kwake. Ila alitumiwa green card palepale akaenda kuichukua, hata hawakumuita kwenye interview. Baadaye akamtaliki mkewe.

Na miaka kadhaa baadaye alikwenda ku renew green card baada ya kumtaliki mkewe, wala hawakumuuliza kuhusu mke wake kwa sababu huko green card ilikuwa yake.

So, kwa mimi nilivyoona, Wamarekani kama hujawapa sababu ya kukufuatilia, na ndoa haina police/ court cases, huwa hawafuatilii sana.
Hata kwa nchi ninazofahamu mimi wanaheshimu utu wa mtu kwenye maswali ila kama nilivyoeleza mwanzo hao walioulizwa hilo swali hawakupewa hiyo permit na nina imani aliyewauliza hilo swali kuna reaction alikua anaitafuta kutoka kwao sbb kwanza waliharibu wakiwa waiting room.

Walikua ni partner fake na walikua hata hawaishi pamoja so walichoharibu ni mmoja wao alikua na kikaratasi cha majibu na maswali common ambayo parnters huulizwa akawa anakisoma pale na mtahini wao akaona na kuhisi anachokisoma ni vitu walivyoambiana kuhusu wao.

Nahisi hiyo ilifanya aachane na maswali yote common na kuwajia na maswali kama hayo.
 
Aaah,

Basi huyo aliamua kufanya UMagufuli tu kumbe.
 
Sikutaka kuzungumza kwa undani sana juu ya hili ulilosema Mkuu. Ila itoshe kusema kuwa unachosema ni sahihi kabisa na nimekuwa nikikisema sana kwa jamaa zangu wanaopenda sana kufika ughaibuni ili watoboe kimaisha. Ukiwaambia hali halisi ili wafanye maamuzi kulingana na uhalisia ulivyo wanaishia kusema ' wewe hupendi wenzako wafanikiwe ndio maana hutaki wafike ughaibuni'.

Wao wanapenda kuambiwa mambo rahisirahisi tu. Mfano kwa sasa Ulaya kuna wimbi kubwa la wakimbizi na hata hizo kazi za box zimekuwa za taabu. Nchi kama Netherlands ni very innovative kwenye job creation ila kazi za box zimeanza kuwa ngumu. Nchi nyingi zinaendelea kuweka masharti magumu ya kuingia ili kudhibiti mafuriko ya watu wanaoingia. Juzi tu UK wameweka bans kwa Nigerians wanaoenda kusoma kuleta wenza wao kuanzia January mwakani.

Ila eti unakuta mtu yupo tayari kutumia karibia 20-50M ili afike ughaibuni. Hajui akifika anafanya kazi gani na atafanikiwa baada ya muda gani. Yeye anachotaka ni kufika tu Ulaya. Wakati akiwa na hizo pesa anaweza kubakia nyumbani na akafanya jambo na akatoboa vizuri tu. Kisha akawa anakuja Ulaya kutalii ama kufanya biashara endapo atakuwa na mtaji wa kutosha. Hivi mfano ukitumia 20M kununua Ng'ombe wa maziwa nyumbani labda wawe Ng'ombe 20, baada ya miaka mitano utakuwa katika hali gani? Badala watu walete mada tushirikishane maarifa ya namna ya kutumia fursa za nyumbani kujiletea maendeleo wao wamekariri stories za miaka ya 90's kwamba maisha yapo ughaibuni pekee.

Wakati watu wanaishia kuishi maisha ya kuunga unga na hawana uhakika hata wa kuhuisha resident permits zao zinapoisha muda wake. Mwishowe wanaishia kuwa scammers kama wafanyavyo Nigerians. Mie nitamuelewa jobless pekee aliyeko bongo na akafanyiwa mpango wa kufika ughaibuni ili angalau afike na afanye hizo kazi za vibarua ambazo bongo hazipo. Ila nitam-challenge huyo mtu endapo zitatumika pesa zaidi ya 20-30M kumsaidia ili afike tu ughaibuni. Sasa unakuta mtu mzima mwenye familia anateketeza karibia 50M afike Ulaya ambako hata uhakika wa kazi ya kufanya hana. Yaani kakariri tu kwamba akifika Ulaya tayari anatoboa maisha. Huku ndiko kudhani kila mzungu anafahamu English sawasawa. Ama kila Mzungu ni tajiri. Kumbe na wao kuna walio choka tu.

Sasa unamwambia mtu, ughaibuni unakosema si lelemama kama unavyodhani. Si jambo lakufika na kufanikiwa kwa muda mfupi unaodhani. Ukweli ni kuwa watu wanaofika ughaibuni, wanaotoboa ni wachache ukilinganisha na wenye maisha ya kuunga unga. Na ndio maana watu wengi hawapendi kabisa kuja hata nyumbani. wanaishia tu kupiga picha za kwenye barabara nzuri na majengo mazuri ili waonekane wanaishi pazuri huku usiku unapofika anaenda kulala kwenye chumba kimoja cha kubanana watu zaidi ya wanne. Yaani unakuta watu wengi wanaishi maisha ya kawaida tu na pesa zao zinaishia kulipa bills kama mdau mmoja aliyesema hapo juu. Watu wengi waliotoboa ni wale walioishi miaka mingi na wakapata nafasi ya kupata kazi nzuri sehemu nzuri. Sio hizi za vibarua vya kuunga unga ambavyo utaishia kulipia bills tu. Labda kwa Marekani maana sijawahi kufika. Ila siyo kwa Ulaya nilikofika.
Ahsante sana, umeelezea vizuri sana hii. Watakusoma na kusikia.
 
Mkuu,

Shukurani sana kwa kuweka sawa. Inabidi tusikie pande zote.

50M mtaji mkubwa tu kwa mtu anayejua kuzungusha hela bongo.

Ila unafikiri kuwa tuna matatizo ya kijamii yaliyopita hata kiuchumi tu, kwamba watu wanaona rushwa, kuoneana, unapigwa kodi na TRA kabla hujaanza biashara, nchi haina uhuru, etc, na mambo haya yanakuwa yanawaelemea hata watu wenye mitaji kama huo wa 50M, wakipiga jura zinavurugwa, wanaona bora wapige kura kwa miguu tu kutafuta maisha nje ya nchi?
Ni kweli kabisa Mkuu.

Rushwa, kodi za manyanyaso, watu kujifanya miungu watu, kuoneana kusiko kuwa na tija na kubadilika badilika kwa sera zetu ni miongoni mwa mambo yanayochangia kwa kiasi kikubwa sana kurudisha harakati za mafanikio za hasa vijana. Changamoto hizi utaziona sanasana unapotoka na kukaa nje ya nchi. Kwa sasa Watawala wanaonesha dalili za kutotaka kukubaliana na jambo la mabadiliko makubwa ya mfumo wa kiutawala kutokana na maslahi yao binafsi maana mfumo wa sasa unawanufaisha wao kwa kiasi kikubwa. Ila naamini ipo siku tu hawatakuwa na namna na hayo mabadiliko yatafanyika. Ni suala la muda tu.

Pamoja na hayo, bado kuna watu wamefanikiwa na ninaamini wengine wengi wanaweza kufanikiwa kwa kutumia fursa vizuri zilizopo nyumbani kujiletea mafanikio ya kiuchumi kwa njia halali kabisa pamoja na changamoto zilizopo nyumbani. Na ikumbukwe mie sipingi watu kuzamia ughaibuni kutafuta maisha, ila mtu afanye utafiti wa kutosha kujiridhisha kabla hujafanya maamuzi hayo. Hasahasa pale mtu anapotaka kuzika karibia 50M ili afike tu ughaibuni na tena hana uhakika wa kazi anayotaka kwenda kufanya. Utaishia kudharirisha utu wako na ni bora zaidi ungebakia nyumbani ukatumia hiyo pesa na ukapanga kwenda ughaibuni kupata exposure kwa kutalii au kufanya biashara endapo mtaji wako utaruhusu huko mbeleni.

Jambo kubwa kabisa naloweza kuhitimisha nalo ni kuwa, watu tupende kujitafutia maarifa kuhusu suala zima la maisha. Jipatie maarifa kwa kila jambo unalotaka kufanya. Kama ni shughuli ya kiuchumi, jipe muda wa kutosha kupata maarifa ya jambo hilo kabla hujalifanya. Ukiwa na maarifa ya kutosha, unaweza kupunguza risks kwa kila jambo kwa kiasi kikubwa zaidi. Unakuta mtu anaanza kufuga kuku wa mayai ila hajui hata basics za magonjwa ya kuku, hajui kuku wanahitaji kula nini waweze kutaga vizuri mayai. Hajui vifaranga wanalelewaje na chanjo za kuku zipo aina ngapi na wapatiwe kuku kila baada ya muda gani. Yeye anadhani kufahamu haya mambo ni mpaka ukasomee darasani. Mwishoni anaishia kupata hasara na kusema 'kilimo na ufugaji vina wenyewe'. Mara anasema ' Mpaji ni Mungu'.

Unakuta mtu changamoto yake kwenye maisha ni namna ya kujipatia kipato, lakini kila akiingia JF anashinda jukwaa la MMU. Wakati Jukwaa la Biashara na Ujasiriamali lina madini ya kutosha sawa na chuo kikuu kabisa. Huwezi kujikwamua kwa namna hii.
 
Sikutaka kuzungumza kwa undani sana juu ya hili ulilosema Mkuu. Ila itoshe kusema kuwa unachosema ni sahihi kabisa na nimekuwa nikikisema sana kwa jamaa zangu wanaopenda sana kufika ughaibuni ili watoboe kimaisha. Ukiwaambia hali halisi ili wafanye maamuzi kulingana na uhalisia ulivyo wanaishia kusema ' wewe hupendi wenzako wafanikiwe ndio maana hutaki wafike ughaibuni'.

Wao wanapenda kuambiwa mambo rahisirahisi tu. Mfano kwa sasa Ulaya kuna wimbi kubwa la wakimbizi na hata hizo kazi za box zimekuwa za taabu. Nchi kama Netherlands ni very innovative kwenye job creation ila kazi za box zimeanza kuwa ngumu. Nchi nyingi zinaendelea kuweka masharti magumu ya kuingia ili kudhibiti mafuriko ya watu wanaoingia. Juzi tu UK wameweka bans kwa Nigerians wanaoenda kusoma kuleta wenza wao kuanzia January mwakani.

Ila eti unakuta mtu yupo tayari kutumia karibia 20-50M ili afike ughaibuni. Hajui akifika anafanya kazi gani na atafanikiwa baada ya muda gani. Yeye anachotaka ni kufika tu Ulaya. Wakati akiwa na hizo pesa anaweza kubakia nyumbani na akafanya jambo na akatoboa vizuri tu. Kisha akawa anakuja Ulaya kutalii ama kufanya biashara endapo atakuwa na mtaji wa kutosha. Hivi mfano ukitumia 20M kununua Ng'ombe wa maziwa nyumbani labda wawe Ng'ombe 20, baada ya miaka mitano utakuwa katika hali gani? Badala watu walete mada tushirikishane maarifa ya namna ya kutumia fursa za nyumbani kujiletea maendeleo wao wamekariri stories za miaka ya 90's kwamba maisha yapo ughaibuni pekee.

Wakati watu wanaishia kuishi maisha ya kuunga unga na hawana uhakika hata wa kuhuisha resident permits zao zinapoisha muda wake. Mwishowe wanaishia kuwa scammers kama wafanyavyo Nigerians. Mie nitamuelewa jobless pekee aliyeko bongo na akafanyiwa mpango wa kufika ughaibuni ili angalau afike na afanye hizo kazi za vibarua ambazo bongo hazipo. Ila nitam-challenge huyo mtu endapo zitatumika pesa zaidi ya 20-30M kumsaidia ili afike tu ughaibuni. Sasa unakuta mtu mzima mwenye familia anateketeza karibia 50M afike Ulaya ambako hata uhakika wa kazi ya kufanya hana. Yaani kakariri tu kwamba akifika Ulaya tayari anatoboa maisha. Huku ndiko kudhani kila mzungu anafahamu English sawasawa. Ama kila Mzungu ni tajiri. Kumbe na wao kuna walio choka tu.

Sasa unamwambia mtu, ughaibuni unakosema si lelemama kama unavyodhani. Si jambo lakufika na kufanikiwa kwa muda mfupi unaodhani. Ukweli ni kuwa watu wanaofika ughaibuni, wanaotoboa ni wachache ukilinganisha na wenye maisha ya kuunga unga. Na ndio maana watu wengi hawapendi kabisa kuja hata nyumbani. wanaishia tu kupiga picha za kwenye barabara nzuri na majengo mazuri ili waonekane wanaishi pazuri huku usiku unapofika anaenda kulala kwenye chumba kimoja cha kubanana watu zaidi ya wanne. Yaani unakuta watu wengi wanaishi maisha ya kawaida tu na pesa zao zinaishia kulipa bills kama mdau mmoja aliyesema hapo juu. Watu wengi waliotoboa ni wale walioishi miaka mingi na wakapata nafasi ya kupata kazi nzuri sehemu nzuri. Sio hizi za vibarua vya kuunga unga ambavyo utaishia kulipia bills tu. Labda kwa Marekani maana sijawahi kufika. Ila siyo kwa Ulaya nilikofika.
Mkuu umeongea kitu kizuri sana.Laiti kila mtu angesema huu ukweli watu wangefunguka macho wakatafuta maisha hapa hapa bongo.
Mim namuheshimu sana mtu asiyeshobokea ughaibuni.Raha ya ulaya ni uende kutembea na urudi bongo.
Watu hawajui tu unaweza ukatumia 30M kufika ulaya ila ukafika huko halafu ukakaa miaka hata 10 bila kuwa na uwezo wa kurudisha hiyo hela wala kuwa na sehemu yako ya kuishi.Unazeeka huna nyuma wala mbele na kurudi bongo unatamani ila huwezi.
 
Ni kweli kabisa Mkuu.

Rushwa, kodi za manyanyaso, watu kujifanya miungu watu, kuoneana kusiko kuwa na tija na kubadilika badilika kwa sera zetu ni miongoni mwa mambo yanayochangia kwa kiasi kikubwa sana kurudisha harakati za mafanikio za hasa vijana. Changamoto hizi utaziona sanasana unapotoka na kukaa nje ya nchi. Kwa sasa Watawala wanaonesha dalili za kutotaka kukubaliana na jambo la mabadiliko makubwa ya mfumo wa kiutawala kutokana na maslahi yao binafsi maana mfumo wa sasa unawanufaisha wao kwa kiasi kikubwa. Ila naamini ipo siku tu hawatakuwa na namna na hayo mabadiliko yatafanyika. Ni suala la muda tu.

Pamoja na hayo, bado kuna watu wamefanikiwa na ninaamini wengine wengi wanaweza kufanikiwa kwa kutumia fursa vizuri zilizopo nyumbani kujiletea mafanikio ya kiuchumi kwa njia halali kabisa pamoja na changamoto zilizopo nyumbani. Na ikumbukwe mie sipingi watu kuzamia ughaibuni kutafuta maisha, ila mtu afanye utafiti wa kutosha kujiridhisha kabla hujafanya maamuzi hayo. Hasahasa pale mtu anapotaka kuzika karibia 50M ili afike tu ughaibuni na tena hana uhakika wa kazi anayotaka kwenda kufanya. Utaishia kudharirisha utu wako na ni bora zaidi ungebakia nyumbani ukatumia hiyo pesa na ukapanga kwenda ughaibuni kupata exposure kwa kutalii au kufanya biashara endapo mtaji wako utaruhusu huko mbeleni.

Jambo kubwa kabisa naloweza kuhitimisha nalo ni kuwa, watu tupende kujitafutia maarifa kuhusu suala zima la maisha. Jipatie maarifa kwa kila jambo unalotaka kufanya. Kama ni shughuli ya kiuchumi, jipe muda wa kutosha kupata maarifa ya jambo hilo kabla hujalifanya. Ukiwa na maarifa ya kutosha, unaweza kupunguza risks kwa kila jambo kwa kiasi kikubwa zaidi. Unakuta mtu anaanza kufuga kuku wa mayai ila hajui hata basics za magonjwa ya kuku, hajui kuku wanahitaji kula nini waweze kutaga vizuri mayai. Hajui vifaranga wanalelewaje na chanjo za kuku zipo aina ngapi na wapatiwe kuku kila baada ya muda gani. Yeye anadhani kufahamu haya mambo ni mpaka ukasomee darasani. Mwishoni anaishia kupata hasara na kusema 'kilimo na ufugaji vina wenyewe'. Mara anasema ' Mpaji ni Mungu'.

Unakuta mtu changamoto yake kwenye maisha ni namna ya kujipatia kipato, lakini kila akiingia JF anashinda jukwaa la MMU. Wakati Jukwaa la Biashara na Ujasiriamali lina madini ya kutosha sawa na chuo kikuu kabisa. Huwezi kujikwamua kwa namna hii.
Mkuu,

Nimekupata vizuri. Ume balance vizuri sana.

Hapo kwenye kumsingizia Mungu tunaongoza sana.

Yani kungekuwa na mchezo wa kumsingizia Mungu kwenye Olympics tungechukua gold medal.

Pia kwenye kuishi na intentionality, hapo tuna mtihani mkubwa. Watu wanaishi kwa kubutua butua tu, hawajiulizi nataka nini, nafanya nini nipate ninachotaka, nifanye mkakati gani, na habari uliyosema ya kukusanya maarifa inaonekana ujinga.

Halafu wengine wakifulia wanakuja kupiga domo kulaumu wabongo walio ughaibuni.

Kuna huyu jamaa mlalamishi sana hapo juu aliandika "Mimi najiandikia tu". Yani mtu anaona sawa kabisa kuwa hivyo. Nikamwambia hili ndilo tatizo, unajiandikia tu, badala ya kuandika kwa malengo maalum.

Wengi wetu hatuna intentionality, tunaamini kubahatisha bahatisha, kudra za Mungu na uchawi.

Wakati wenzetu wanapanga kabisa mambo yao. Yani hata kama kuna bahati, unajitengenezea mazingira mazuri bahati ikuangukie wewe kwa kuwa na vigezo vyote.
 
Back
Top Bottom