Wabongo tunahitaji mabadiliko makubwa sana ya kifikra, bila hivyo...

Wabongo tunahitaji mabadiliko makubwa sana ya kifikra, bila hivyo...

Mbwilimbwili

Senior Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
183
Reaction score
282
Salamaleko ndugu wa JF, niende moja kwa moja kwenye mada, kufuatia kitu kinachoendelea kutawala anga la habari kwa Tanzania yetu kwa sasa(ajali ya Precision Air), kwanza nitoe pole kwa wote walioguswa moja kwa moja na pia watz wote.

Kilichonisukuma kuandika huu uzi, baada ya tukio la ajali maoni yamekua mengi, mawazo yamekua mengi, ila shida kubwa tupo nayo sisi kama Watanzania, naomba niseme tu kwa uchungu mkubwa sisi ni 'MALIMBUKENI!' na tunahitaji mabadiliko makubwa sana kwenye fikra zetu, hawa viongozi tunaowalalamikia kwa uzembe hawatoki uvunguni, wanatoka kwenye jamii zetu hizihizi!!

Si ajabu kesho mtu anakua kiongozi akafanya yaleyale wanayofanya aliokua anawalalamikia!, mifano ipo mingi kwa matukio kutokea na sisi kujikuta tunarudia makosa yaleyale!!

Shida kubwa wabongo sisi ni watu wagumu kuchukua hatua kwenye jambo lolote lile, kisiasa tunapigwa, kiuchumi tunapigwa, kila kitu.

Nisibwabwaje sana, ila
  • Tuwe watu wa kufanya reasoning (ujinga ni mtaji wa wanasiasa!)
  • Tupende kujifunza kila siku
  • Tumtafute Mungu
  • Tukatae unyonge (Huu ndio umetufikisha hapa!)

La mwisho: KAZI YA MJINGA NI KUUMIA!!

Kwenu studio
 
Mkuu wew Ni kiboko haswaaa umeiba I'd na kuifananishaa na ya gentamycine[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Safi Sana uko vzr

GENTAMYCINE njoo muone pacha wako
 
Back
Top Bottom