OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Moja kwa moja kwenye hoja
Nimeshangazwa sana na mazingira aliyotekwa kiongozi wa Chadema. Sishangazwi kwa sababu ni kiongozi wa upinzani bali ni mazingira aliyotekwa.
Mimi sikuwepo, lakini najaribu kufikiria tu, iliwezekanaje? Otherwise aliyekuwepo anisahihishe.
Najaribu kuwaza hivi....kuna taharuki ya utekaji imeenea. Polisi wakilaumiwa. Viongozi wa dini wamesema. Kule Busega waliandamana mpaka mtu akauliwa na polisi. Katika hali kama hiyo maana yake wananchi tulitakiwa kulindana sisi kwa sisi. Kwamba hatutakuwa tayari kuruhusu mtu akitwaliwa katika mazingira yasiyoeleweka. Lazimu tuzuie hilo tukio kwa hali na mali hata kama damu itamwagika.
Lakini watu wameingia kwenye bus wakamshusha yule jamaa wakaondoka naye. Sifikirii kama alitulia tu, obvious alikomaa kwanza na kujisanua. Mwisho watekaji wakafanikiwa kumteka mbele ya abiria.
Maana yake kwenye jamii kama hii ambayo serikali haina habari na ulinzi na usalama wa raia wake, unapaswa wewe mwenyewe binafsi kujilinda. Usijekusubiri maraia watapika kelele wakati unatekwa. Wao watasubiri kupiga kelele mitandaoni na Jamiiforums tu. Muda huo umeshachezea kichapo kikali na hata kifo.
Na hiki chama kinachoteka watu kuweni na huruma basi. Kweli unamteka mtu kwa sababu tu kakukosoa?