Marie Antoinette
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 426
- 412
Nimependa ustaarabu wako. Sorry kwa kauli niliyotumia. Ni baada tu ya kuona umekwazika lakini huwezi kuwakabili jamaa watekaji,maana hujui wana nini,ja hata likiwa basi zima kulifyeka hawaoni taabu.Kwani humu mtandaoni watu wanapiga kelele au wanabadilishana mawazo? Sheria za nchi zinasema kuna uhuru wa kutoa maoni ila hautakiwi kuvunja sheria na ndiyo tunautumia.
Ningekuwa navunja sheria ningekuwa nishakamatwa ,hapa tunaeleweshana tu ,issue ya kufanya lolote ,hivi unaweza ukaleta purukushani kwa watu zaidi ya watatu mbavu waliokuja na mitutu? Kama wao wanajiamini waje man to man mtu mmoja kwa mmoja na si Mobb huku wakiwa na silaha.
Haya mambo yapo toka enzi,na karibia nchi zote ulimwengu mzima. Kihisia,kiubinadamu,utagundua watu wana roho mbaya,si kila kosa linastahili adhabu ya kifo.
Lakini pia,kumbuka hiyo roho ya kupigania haki za wenzako,unayo wewe. Na kuna wengine,wanaona kuna kikwazo. Hivyo huandaa mazingira ya kuondoa kikwazo. Bahati mbaya hawaji wao,wanatumwa watu. Kwa gharama yoyote. Mtu kawekeza milioni zake kufanikisha uovu wake, mwingine awekeze mdomo! Duniani hakuna haki.