Wabongo wengi ukiwasaidia wanaamini kuna kitu unapata. Hivyo usimsaidie MTU burebure

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
WABONGO WENGI UKIWASAIDIA WANAAMINI KUNA KITU UNAPATA. HIVYO USIMSAIDIA MTU BUREBURE

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Wabongo wengi wanaamini huwezi kuwasaidia burebure.

2. Wanaamini wanastahili uwasaidie kwani nawe unakitu utapata unapowasaidia.

3. Kwamba wewe ndio unashida kuliko wao. Au tuseme hata wewe unashida ambayo itaondoka ukiwasaidia.

4. Ndio maana ya kauli ya tenda Wema Uende zako. Kwa maana asilimia tisini ya utakaosema uwasaidie hawaamini unawasaidia burebure. Lazima kuna kitu unapata au utapata utakapowasaidia.

5. Ukitaka kujua ukweli huu. Angalia waombaji wengi. Wanapokuomba kuna maneno ambayo kisaikolojia yanaashiria hata wewe hauwasaidii Burebure. Kwamba nao ni valuable ukiwasaidia utapatamo chochote kitu.

6. Mfano, Watakuambia Nisaidie na Mungu atakubariki. Huo ni utapeli.
Ni dalili na kiashiria kuwa muombaji haoni Msaada wako kwake ni yeye tuu atafaidika Bali hata wewe utapata faida.
Hivyo hata ukimsaidia hawezi ona uzito wa ulichokifanya. Hawezi kukushukuru.

7. MTU yeyote anayekuomba Msaada alafu akakuambia Mungu atakubariki usimpe huo msaada. Usimpe! Usimpe! Huyo ni muongo, tapeli na Hana shukrani.

8. Anajaribu kukueleza kuwa hata wewe unauhitaji. Hata wewe utafaidika na msaada unaompa. Jambo ambalo sio kweli.

9. MTU yeyote anayekuambia Leo kwako Kesho kwake. Huyo usimsaidie. Kwani anajua umemsaidia kwa sababu wew Kesho yako huijui na utamtegemea naye akurudishie.

10. Mtu yeyote anayemleta Mungu wakati anakuomba Msaada au anayekuletea misemo ya Kiswahili ili umsaidie. Huyo usimsaidie. Kwani haamini kwamba wewe unaweza kumsaidia burebure, haamini kwamba wewe unamoyo wa kusaidia wengine bila kutegemea chochote. Haamini kwamba unamoyo QA huruma.

11. Anakuona kwamba bila kukuambia Baraka za Mungu hautampa. Bila kukutishia kwamba ya Kesho huyajui huwezi MPA.

12. MTU akija kuomba msaada akikuletea mambo ya Mungu mwambie moja kwa moja huna au huwezi kumsaidia.
Au mwambie huamini katika Baraka za Mungu. Hata kama unaamini. Imani yako haipo kwenye maneno yako.

13. Ndio maana hupaswi kufikiri unamsaidia Single mothers kulea watoto wasiowako. Kwani yeye anaona ni halali uwalee kwani nawe kuna kitu unakipata kutoka kwake(mama MTU).

14. Kusaidia mtu kuna kanuni zake. Ambazo ni kama ifuatavyo;
a) Saidia MTU aliyeomba Msaada na ambaye haoni kwamba utapata faida kwa msaada uliompa.
Watu hawa Kwanza hawamtaji Mungu popote.
Watu hawa hawamlaumu mtu yeyote kutokana na matatizo yao.
Watu hawa wakija kwako wataenda direct kwenye pointi wakielezea shida yao.
Hata ukiwasaidia hawatakuwa na maneno mengi. . Sura na body language yao ndio vitaongea kuliko mdomo.

Ukiona MTU analaumu wazazi wake Kwa kumtelekeza ndio anatumia kama hoja ya kumsaidia usimsaidie.
Ukiona Single mothers analaumu Aliyemzalisha huku akijiweka safe side piga pin usimsaidie.
Usisaidie wanaolaumu wengine wakati walishiriki pamoja.

b) Usisaidie MTU ambaye hafanyi wajibu wake.
Saidia MTU anayekazana, anayepambana lakini mazingira yanamuangusha. Mtu anayeonyesha uwezo wake lakini Hana sapoti.

Kijana amesoma lakini anapambana kufanya kazi za hapa na pale kama bodaboda, saidia fundi, kuimba kwenye club au mitandaoni ilimradi kufurukuta. Huyo akiomba Msaada MPE. Lakini kanuni ya Kwanza usiisahau. Sio anaonyesha juhudu lakini hajakuomba msaada.

Usilee mtoto asiyewako yaani wa single mother ambaye hajishughulishi. Yaani no mwanamke mvivu mvivu. Anayesubiria kuolewa akae nyumbani kama mdoli. Huyo usithubutu. Ni hatari kwa future ya furaha yako. Hatari Sana.
Usiwe mjinga. Jiheshimu.
Ni jukumu la Mama kulea watoto wake iwe ameolewa au hajaolewa. Iwe ni mjane au sio mjane. Na hapaswi kumpa majukumu mwanaume asiyehusika.

Mwanamke yeyote anayekuambia ukipenda ua penda na ua lake. Huyo pigs Chini. Hakuna mtu hapo. Upendo wa lazima ni kupenda kulicho chako kama watoto au wazazi. Upendo wa mke na mume ni hiyari. Upendo wa kupenda watoto wa kambo ni hiyari sio lazima.

C) Saidia Kwa Moyo wako bila kuhitaji fadhila.
Kimsingi hakuna msaada usiohitaji fadhila. Kiutu Kila anayetoa msaada hutegemea kushukuriwa.

Kuna Ile unaamua kutoa kwa sababu moyo wako umetokea kuingiwa na huruma au upendo kwa MTU au Jambo Fulani. Na ukifanya hivyo utajihisi furaha. Toa.

Ila upendo lazima udhibitiwe na Akili ili kuepusha majanga huko mbeleni. Ndio maana vigezo vingine hapo juu lazima uvizingatie.

15. Hata hivyo unaweza kutoa kingi ili upate kidogo hiyo pia ni sehemu ya kutoa.

16. Kuna kutoa kidogo ili upate kingi hiyo ni biashara.

17. Ukikutana na watu wasio na shukrani na wasiowajibika. Wasaidie kidogo pata kingi. Hiyo ni kanuni. Siku zote utakuwa salama.

18. Hata ukitafuta mwanamke. Kamwe usikubali kuwa na mwanamke asiye na pesa. Au chochote ambacho utakipata kutoka kwake hasa wanawake wa Zama hizi. Hao waachie Beta Male. Hakuna cha maana utakachopata huko zaidi ya mateso. Na watakuimbia zile nyimbo za wajinga kwamba wanaume wameumbwa mateso kumbe ni Wanaume dhaifu(Beta Male). Alpha male hawana huo mtazamo wa wajinga.

19. Alpha male wanatumia kanuni ya watajiumiza na kujitoa sehemu wanayopata Faida tena faida zinazoonekana kama pesa au Mali. Na sio utamu sijui vitu gani. Ujitese kisa utamu tena wa dakika kumi huo kama sio wendawazimu ni kitu gani. Tena utamu mnapata wote alafu unayeteseka ni wewe tuu. Huo ujinga waachie wajinga.

Mimi acha ni nipumzike.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Chief maneno mengi kama msaada upo ndani ya uwezo wako na hauwezi kuasili alakati zako ww saidia mengine achana nayo kama huwezi kusaidia usitoe msaada na pia usipende kutoa ahadi ambayo unajua kabisa huwezi kutimiza
 
Pumba tupu.
 
Back
Top Bottom